Mkuu, umehitimisha vizuri.
Pia ukisoma hii sehemu ya Bageni kujitetea utaona wapi alipatwa na hatia.
Utetezi wa bageni;
Jaji: Mshitakiwa, hebu kwanza nikuulize, hii ripoti ya daktari hapa mimi bado inanisumbua kidogo, Kwanza umesema ulipokwenda katika ukuta wa Posta ulipopelekwa na James hamkukuta damu
Bageni: Ni kweli
Jaji: Jana yake siku mliyokwenda ama asubuhi yake kulikuwa na mvua?
Bageni: Hapana hapakuwa na mvua.
Jaji:Umesema ukutani uliona matundu sita yalidaiwa kuwa ni ya risasi, lakini hawa marehemu walikuwa ni wanne je hizi risasi sita zilitoka wapi au baada ya kupigwa waliendelea kupanda ukuta?
Bageni:Mtukufu Jaji. mimi sikuwepo lakini mapambano mengine zinaweza kupigwa risasi nyingi zikajeruhi chache tu.
Jaji:Na kwa nini hapakuwa na damu?
Bageni: Mtukufu Jaji,hata mimi sijui kuwa ilikuwaje.
Jaji:Umesema matundu yale jinsi yalivyokuwa ukutani inaonekana yalipigwa kutokea pembeni, je katika hali hiyo inawezekanaje kumpiga mtu kisogoni? Alihoji Jaji na kumuelekeza Bageni aegemee ukuta na kisha kumtaka eleze mtu akipiga risasi kutokea upande wa kushoto kwake ni jinsi gani inaweza kumpata kisogoni.
Bageni: Mtukufu Jaji hapa zitampiga hapa,alisema Bageni akionyesha sehemu za begani.
Jaji:Umesema ulipelekewa maganda ya risasi baada ya siku tatu, nne je uliuliza kuwa maganda hayo waliyapata wapi?
Bageni: Niliuliza wakasema waliyatoa Sinza eneo la tukio.
Jaji:Waliya-collect siku hiyohiyo?
Bageni: Nadhani maana askari akipiga risasi lazima a-collect maganda.
Jaji:Kama pale ukutani kulikuwa na matundu sita na walikuletea maganda tisa je haya matatu uliuliza waliyatoa wapi?
Bageni: Ni kawaida Mtukufu Jaji kuwa unaweza kulenga risasi ikapita juu ya kitu ulichokusudia.
Jaji:Kwa maelezo ya James (mkuu wa upelelezi kituo cha Urafiki) ni askari wangapi waliopiga risasi siku hiyo?
Bageni: Hakunieleza ni wangapi.
Jaji:Balistic (Mtaalamu wa masuala ya silaha na milipuko) alisema ni silaha mbili tu ndizo zilizopia ya Saad na ya mshtakiwa wa 12 ,una ‘comment’ yoyote kwa hilo?
Bageni: Mtukufu Jaji, yeye ndiye mtaalamu.
Jaji:Umeeleza kuwa mshtakiwa wa kwanza alikushauri lini mbadili taarifa ya kwenda kwenye Tume ya Kipenka?
Bageni: Mtukufu Jaji, sikuwa specific katika tarehe ila rekodi isomeke siku ambayo alikuwa ‘summoned’ kwenye tume.
Jaji:Kwa nini alikwambia uandike nyingine wakati ulikwishaandika taarifa ya kwako?
Bageni:Aliniambai ifanyiwe marekebisho kidogo ili mambo yawe sawa.
Jaji:Mshtakiwa wa kwanza alisema hapa kuwa polisi hutii amri halali tu je hiyo ilikuwa ni amri halali?
Bageni:Ni halali sababu yeye ni mkubwa wangu
NB: Kuna sehemu kama hapo penye rangi nyekundu ndio palikuwa panatayarisha kabisa jeneza la Bageni.