Zumaridi asichukuliwe kimasihara, imani ni kitu kikubwa sana inahuisha na imani inaua Watanzania tuamke

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Zumaridi anawafundisha watoto kwamba yeye ni mungu, yeye ndie msaada na ndie anayewakinga na mauti, anasema yeye ni mtawala wa dunia mzima na anayetawala vitu vyote vya duniani na mbinguni tena wake kuna uzima wa milele.

Your browser is not able to display this video.



Halafu anawaambia watoto leo atawapikia tena wali😎😎😎

Inatisha, inasikistisha..... huyu heri angebakigi kulekule jela
 
Hao Watoto ni yatima hawana Wazazi?

By the way hizo ni project za Ccm kuspin akili za watu kila linapotokea jambo kubwa la kitaifa kuwahamisha watu kwenye mjadala.
 
Kwani hao watoto hawana wazazi ?
Hao wazazi Mungu wao ni Nani ?

Kama na wao wana muabudu huyo Zumaridi wanapaswa kulaumiwa ?

Sitetei nasema tu Kama Changamoto
 
Mungu gani huyu anakula ugali, anajiremba na mwenye lafudhi ya kanda ya ziwa? Iko hivi, serikali isimbughudhi imuache tuone mwisho wake ila asiue watu kama yule wa shakahola kenya. Huenda akawa ni mungu mtu
Imani Ina nguvu ya kuleta madhara isipodhibitiwa
 
Imani Ina nguvu ya kuleta madhara isipodhibitiwa

Huu ndio ukweli
Sasahivi tutaona hili jambo halituhusu ila matokeo yake yataigusa jamii yote hayatachagua kwamba huyu alinyamaza, au alishangilia au alikemea

Yesu atusaidie sana
 
Wako wengi sana akina zumaridi. Kuna wengine wanagawa hela kwenye madhabahu zao, wanajiita mitume, manabii na makuhani. Walio kinyume na majina haya nao wameibuka wakijiita shetani, lusifa na ibilisi wakidai nao wana mwanga na uwezo wa kutatua shida za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…