Zumaridi aviponza Vyombo vya Habari. TCRA yatoa onyo na kuvitaka kusimamia misingi ya utoaji habari

Zumaridi aviponza Vyombo vya Habari. TCRA yatoa onyo na kuvitaka kusimamia misingi ya utoaji habari

Kwani mkutano wa mwamposa unapokuwa live nani hapo TCRA amehakikisha kinacho zungumzwa pale ndio ukweli? Kuna mtu TCRA amewahi kwenda mbinguni na akatuhakikishia kinacho semwa mikutanoni live ndio ukweli wenyewe?
Usiwalaumu sana maana wana uwezo mdogo wakufikiri ijapokuwa wamepewa mamlaka makubwa kuyaongoza, huwa napatwa na wasiwasi inakuaje akili ndogo inapewa mamlaka makubwa na je mteuwaji wa hizo akili ndogo yeye akili yake niyaaina gani?

Maswaali fikirishi sanaa
 
bado inaukakasi,
Zumaridi Tv bado watayarusha hayo ya ndani ya nyumba ya ibada kwenye Online Zumaridi Tv.

Hawa wengine wanaofufua watu, wanaogawa mafuta, maji ya baraka nk huku wakiwa live tena wamelipia hizi coverage kwenye media kubwa kabisa zinazoheshimika.
 
Zumaridi yuko sahihi. Sisi wafuasi wake tunataka kusikia aliyoyaona mbinguni.

Kila mtu ana nadharia yake ya mbinguni jinsi kulivyo, wamuache mfalme wetu Zumaridi.

Na wiki ijayo ataenda mbinguni na atatuambia ameona nini.

Next week itakua ya watu wafupi akiwemo mkuu wa tisiaraei, mbinguni hawafiki.
 
Mbna manabii wengi tu na mitume huwa wanashuhudia makanisan kuwa wameoteshwa walinda sjui wapi , kwa zumaridi imekuwa nongwa , TCRA badara ya kushughulika na utapeli wa vifurushi wazee wa tuma kwa namba hii , unakuja kukomaa na mtu kama Zumaridi duuh
 
Hapo sijui TCRA wameandika nini. Haisomeki vizuri kwenye Itel yangu. Lakini naona kama uhuru wa dini unaingiliwa.
Check out this Good Man.
Nimesikia sasa hivi kwenye taarifa ya habari. Habari za dini zinafuata nini mtandaoni? Habari za dini zinatakiwa kuwa kwenye nyumba za ibada. Ina maana ule utumbo alioongea Zumaridi aliposema atamfufua Kanumba,akiongelea kwenye nyumba ya ibada sio kosa.
Taasisi muhimu inaongozwa na watu hawa Maadui wa Mwenyezi Mungu.
 
TCRA inaenda kinyume na kuwezesha umma kufikiri. Uwezo wa bongo la binadamu kujenga taswira ya kufikirika ni muhimu sana .

Mfano simulizi za mnara Babel ulikuwepo kule Babylonia Iraq ya leo ambao wakaazi wake walitaka kujenga mnara mkubwa wafike anga za juu kumuona Mungu, naye Mungu akaamua kukatiza mradi huo kwa ghafla bin vu kuwapa wajenzi na wafadhili wa mradi lugha nyingi ili wasiweze kuwasiliana kukamilisha mradi wakwame kufikia azma yao ya kufika anga za juu je lugha mojawapo haikuwa Kisukuma, Kindali, kiArmenia, kiHebrew, Kiarabu n.k ?

Dini yoyote iwe ya kutoka Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali, bara hindi, dini za Andes kule Marekani ya Kusini n.k inayoamini uwepo wa mamlaka kubwa kwa nafasi inayoitwa Mungu pia ni suala la kufikirika

TCRA isiwe chombo cha kidikteta kuzuia watu kuota, kuweka hadithi za kufikirika n.k inayowezesha jamii kujenga uwezo wa kuhoji, kujadiliana na kuvumbua vitu vipya kupitia njozi, kuota kwenda anga za mbali n.k
 
Back
Top Bottom