TCRA inaenda kinyume na kuwezesha umma kufikiri. Uwezo wa bongo la binadamu kujenga taswira ya kufikirika ni muhimu sana .
Mfano simulizi za mnara Babel ulikuwepo kule Babylonia Iraq ya leo ambao wakaazi wake walitaka kujenga mnara mkubwa wafike anga za juu kumuona Mungu, naye Mungu akaamua kukatiza mradi huo kwa ghafla bin vu kuwapa wajenzi na wafadhili wa mradi lugha nyingi ili wasiweze kuwasiliana kukamilisha mradi wakwame kufikia azma yao ya kufika anga za juu je lugha mojawapo haikuwa Kisukuma, Kindali, kiArmenia, kiHebrew, Kiarabu n.k ?
Dini yoyote iwe ya kutoka Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali, bara hindi, dini za Andes kule Marekani ya Kusini n.k inayoamini uwepo wa mamlaka kubwa kwa nafasi inayoitwa Mungu pia ni suala la kufikirika
TCRA isiwe chombo cha kidikteta kuzuia watu kuota, kuweka hadithi za kufikirika n.k inayowezesha jamii kujenga uwezo wa kuhoji, kujadiliana na kuvumbua vitu vipya kupitia njozi, kuota kwenda anga za mbali n.k