Zumaridi aviponza Vyombo vya Habari. TCRA yatoa onyo na kuvitaka kusimamia misingi ya utoaji habari

Ukiiangalia hii barua, inazua maswali ya uelewa wa wasomi wetu. Imani ni nini? Ni kuwa na mategemeo katika mambo usiyoyajua, usiyoyaona. Je Imani kama Imani sio mambo ya kufikirika?
Ikitokea sheikh au kasisi anarekodiwa akitoa mawaidha mubashara na akaongea kama haya tcra inayojaribu kuyapiga vita, chombo cha habari kifanye nini?
Katiba inatoa haki kwa MTz kuhabarishwa, kutoa maoni yake pia. Hili katazo lao linasimamia upande gani?
 
TCRA wamekurupuka. Cha kwanza wanajua kuwa hakuna elimu yoyote ya kidini inayotambuka serikalini. Msingi kwa nini serikali haitambui hizo taaluma ni kwa sababu ni za kufikirika.

Cha pili, ni TCRA haohao na serikali ndio wamelakubali maudhui ya kidini ya enezwe kwa njia ya redio na tv. Kwann walikubali elimu wasioitambua ifudishwe hadharani na kinyume chake wanakataza maelezo ya mtalaam ZUMARIDI? Au wanatumika kwa maslahi ya dini fulani?

Cha tatu, hakuna dini mpya imeingia kilaini katika jamii. Dini zote zimeenea kwa njia ya kupigana kupitia kupata kuungwa mkono na viongozi wa kisiasa. ZUMARIDI anatakiwa apambane ungwaji mkono
 
Watu wanapenda kuchukulia vitu very serious wakati vingine unapaswa kuchukulia kama comedy tu ucheke uongeze siku zako za kuishi
Kama ni kwasababu ya zumaridi hapo TCRA mmefeli pakubwa,
Hakuna mwenye akili timamu atakua bothered na story za zumaridi mana unajua tu anatafuta popularity and after sometimes atapotea ataibuka zumaridi mwingine kwa staili yake!
And that is life,
 
TCRA naona hawana kazi za kufanya sasa mpaka kuhangaika na maswala ya Imani....na bahati nzuri yule mama wa kifalme kasema yoote aliyoyaona ilikuwa ni ndoto iliyomtokea usiku....sasa TCRA wanahangaika na ndoto ya Zumaridi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Zumaridi hajavunja sheria yoyote ya nchi.

Kila mtu ana haki ya kutoa maoni, kuabudu, n.k. as long as havunji sheria za nchi wala haki za binadamu mwenzie.

Serikali ijikite kufanya mambo ya msingi, siyo kuamria watu waamini ama wasiamini nini.
 
Zumarudi hatukani wala kukashfu dini nyingine so Hana Kosa hapo anaongea Hisia zake na mambo Aliyoyaonaa Huko ndotoni mbona Wengi kibao huwa wanasema jui ya waliyoyaonaa ndotoni[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Zumaridi ndo anaonekana tu peke yakee kweli??? Wawakataze woteee....
 
Kama Chizi Mwamposa anapewa "airtime" kwa nini Chizi Zumaridi asipewe airtime"? Wote hao machizi tu. Pia machizi wa dini nyingine za kikristu na kiislaamu hupewa airitime, kwa nini chizi Zumaridi anyimwe?
Hivi wewe una akili timamu ?!

Zumaridi ni wa kumfananisha na mwamposa na wengineo hao unaowataja na unaowafahamu?! 🤔
 
Hivi kwa anavyovizungumza yule na mafundisho jinsi yalivyo ukijumlisha na matendo yake anayoyafanyaga unamuona yuko timamu kiakili?!
 
Mwambie Millard Ayo na timu yake aache kukurupuka kuhangaika kutafuta content ambazo hazina maana kwenye kwasababu ya kutafuta hela za laana... pesa za aibu zinafedhehesha...
Kamejipunguzia heshima sana kale kabwana mdogo kwa kumuita huyo CHIZI amhoji. Bora niwe namsoma Sam misago na Clouds media sio huyu asiyetaka kuoa... 😅
 
Swali la msingi kabisa,
Tukikubaliana na TCRA katika hili huko mbele ni maumivu makubwa kwa uhuru wa habari.
Nape anafikiri kazi yake ni kuminya uhuru wa habari. Naamini watu wa TCRA ni waelewa, hawawezi kuwa walikuja na kitu kama hiki. Lazima ni shinikizo la mtu fulani mwenye uelewa mdogo.
 
Wako sahihi kabisa. Ni makosa makubwa kutoa mambo ya dini ambayo YAKO secret ( forbidden Knowledge) kuyaweka public. Haifai kabisa. Ni kuwakoroga watu vichwa.
 
zumaridi ana dini yake ambayo wanaongea kisukima Hadi mbinguni,kwa hilo siyo tatizo.Tatizo ni pale dini ya zumaridi mfalme inachanganya na maudhui ya Imani za watu wengine mfano mtume Petro hapo anazungua Imani ya Kikristo na anapotosha,hapo kavuka mipaka.Angeamua akatengeneza wahusika wake kama ngosha,jiwe nk isingekuwa tatizo.Afanye uzumaridi ila Ukristo,uislam ,nk aachane nao.
.
 
Tena wahubiri wengine hua wanadai kua wana uwezo wa kumfufua mtu aliyekwisha kufa.
Kuna yule mwingine aliwaleta hasi kanisani kabisa, kuwa Hawa walikuwa misukule, Kwa jina la yesu wamepona. Sasa taabu Iko wapi Kwa zumaridi. Tuache Double standard.

Dini zote zinazungumzia mambo ya kufikirika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…