Akili Mnemba ni teknolojia iliyosambaa ulimwenguni ikiwa imerahisisha kazi za binadamu kutokana na kwamba inaweza kufikiri kama binadamu. Lengo la AI ni kuweza kufanya mambo kama vile kutambua mifumo, kufanya maamuzi, na kuhukumu kama binadamu.
Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.
Akili mnemba ni muhimu katika shughuli za kila siku kwani husaidia kurahisisha utendaji kazi wenye ufanisi hata hivyo kama itatumika katika namna ovu...