Muhimu: orodha hii ni kwa makabila ya asili ya hapa kwetu, wageni kama waarabu, wahindi, wachina, n.k hawahusiki.
Wachaga -
Biashara, Elimu na siasa
Kubebana na kusaidiana ni silaha kubwa sana katika maendeleo Yao, umoja ni nguvu
Kibiashara kabila hili wapo katika nafasi nzuri, wamekuwa pioneers Wakubwa katika kuanzisha na kuziendeleza biashara kibao hapa Tanzania.
Kielimu wamejitosheleza, mkoa wanaotokea ndio unaongoza Kwa kuwa na shule nyingi, hali hii inatoa fursa kwao kuwa na elimu za kuwapa sifa za kupata ajira na vyeo.
Kisiasa Nako wapo active mno sijaona wa kuwakaraibia, vyama vikuu vya upinzani vilivhowahi kuleta upinzani mkali kuanzia Tlp, Nccr na Chadema vimeanzia huko kwao, Pia katika chama kikuu cha ccm influence Yao si haba.
Kila mwisho wa mwaka wanarudi kwao Kilimanjaro, Hata mchaga akiwa Marekani, Ulaya, n.k ikifika mwisho wa mwaka anarudi, kukutana huku husaidia kuchangiana mitaji, ndugu kujuliana hali pamoja na majirani, kupanga mikakati, kutambulisha watoto Kwa ndugu, n.k
Muhimu zaidi wachaga hawasahau walikotoka, licha ya kuwa na maendeleo miji ya ugenini lakini pia wanaendeleza vijiji walivyotokea hasa katika kujenga makazi, kuboresha huduma za kijamii na miundombinu. Hata ukitokea msiba au mtu karudi kusalimia kwao hapati shida.
Wakinga -
Biashara
Kama ilivyo Kwa wachaga, nao hawa Kubebana na kusaidiana ni silaha kubwa sana katika maendeleo yao, Idadi Yao ni ndogo hawavuki milioni lakini wanabebana sana pengine kuzidi hata wachaga.
hawa shabaha yao ya mafanukio wameilenga zaidi kwenye biashara, kwenye elimu bado wanajikongoja lakini main focus wameweka kwenye biashara na kiukweli biashara zimebadili maisha yao, wengi wanamjua vunja bei kwasababu ni mtu wa anaependa umaarufu lakini huyu bado yupo level za kawaida Kwa wenzake, wapo wakinga vijana tu kama yeye wana mkwanja mrefu zaidi lakini nidhamu yao ya pesa inafanya iwe ngumu kuwatambua, mkinga unakuta ana chain ya hotel na maduka lakini anaishi maisha ya kawaida kama tajiri mzungu ama mhindi
mwamko wa biashara kwa wakinga wengi ulianza miaka ya 2000 lakini ndani ya muda mfupi huu maendeleo yao yametuacha vinywa wazi, mfano mdogo tu ni kwamba soko kuu la kimataifa la Kariakoo wao ndio wanaongoza kwa uwakilishi, zamani palijaa wachaga na wapemba lakini kwa sasa wakinga wamepindua meza, wanauza vitu kwa faida ndogo na bei ndogo inakuwa ngumu sana kushindana nao. Nje ya Dar sehemu walizokamata kwa sana ni mikoa ya nyanda za juu kusini Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma..
Wapemba -
Biashara
Hawa nao kubebana na kusaidiana ni silaha kubwa sana katika maendeleo Yao, umoja ni nguvu
Kwenye swala la elimu huko Pemba wapo chini sana ni mkoa unashika namba ya mwisho miaka nenda rudi lakini kwenye biashara wapo mbali sana, mafanikio waliyonayo ni kuzidi hata ya wasomi wengi wanaopokea mishahara ya milioni, Huko kigamboni wamejazana tele.
Wasukuma -
Elimu na kilimo
Hawa ndio wanaongoza kwa kuwa na watu wengi hii nchi wapo takribani milioni 12, idadi yao ya kuwa wengi ilibidi iwabebe lakini tatizo lao kubwa ni kwamba wana ushirikiano mdogo na ndio maana hata wingi wao unakuwa kwenye namba tu, niwe mkweli tu hawa wasukuma wangekuwa wanabebana wangekuwa hawana hata mpinzani wa kuwakaribia hata robo, wangekuwa ni tishio sidhani hata kama mchaga angewafikia hata nusu, ila ndio hivyo tena umoja hata wa watu wachache una nguvu kubwa kuliko watu wengi waliotengana.
any way kwa wasukuma nao kwa vile idadi ni kubwa nao wapo kwenye elimu, kwenye biashara za migodi namo wapo sana sana kama wachimbaji wanaojitegemea.
Wahaya -
Elimu
Hapa ndipo makao makuu ya wasomi, kiukweli katika swala la akili za darasani hawa jamaa wapo juu, mkoani kwao mazingira ya elimu yapo chini lakini bado wanatisha, ilifikia kipindi serikali ilioneza alama za ufaulu kwa mkoa wa Kagera maana watu walikuwa wanafaulu kama wanacheza game.
Tatizo linapokuja kwa mhaya ni kwamba anategemea sana ajira kwa kutumia uwezo wa darasani ila kwa sasa zama zimebadilika, elimu siku hizi imesambaa mno, ufaulu umeongezeka, shule zipo kila kona ya nchi, elimu imerahisishwa, kuna mamia ya vyuo, n.k karibu kila kabila siku hizi kuna wahitimu wa vyuo katika fani mbali mbali wenye sifa za kuajiriwa, sio kama zamani tena! na sikuhizi wizara ya utumishi ndio inasimamia zoezi la ajira sio kama zamani kwamba bosi wa shirika au taasisi unamkuta ni mhaya au mchaga anajaza wenzake, Mambo yamebadilika!! Kwa mchaga ana mlango wa pili wa biashara lakini hapa kwa mhaya kujipambania inakuwa ngumu.
Pia Tabia ya majigambo Ina wagharimu sana maana hii tabia huenda sambamba na ubinafsi wa kujikusanyia vingi Ili kutambia wengine.⁵