Unajua kuna kitu watu hawaelewi.
Safari hii team nyingi sana zimekuja na wachezaji wanaocheza nchi za nje. Mataifa mengi yamefanya kama ilichokifanya Tz kuwaita wachezaji wao waliokulia nje ila hawajapata nafasi za kuitwa mataifa ya huko, tofauti ni kwamba wenzetu wamefanikiwa kwa kupata wachezaji wa aina hiyo wenye viwango kuliko sisi.
Leo nimefuatilia team ndogo ambazo zimeshacheza (Guinea zote, Msumbiji, Gambia) ,wachezaji wote ni wa nje na wengi wao hawajaanzia mpira kwenye mataifa yao.
Ni kama mashikisho mengi ya mpira kwa Africa yameshtuka na kuacha kutegemea kuzalisha wachezaji kutoka ligi zao za ndani.