2025 ili ukubalike kwa haraka, italazimu Tundu Lissu kulitaja jina la JPM kuomba kura kwa Wananchi

Kaanzisha SGR, mkitaka muuze chuma chakavu shauri yenu, yeye Hana deni

Ndege kibao na nyingine Hadi naogopa ikiwa zitatua ama watazigawana hukohuko, mkitaka uzeni shauri yenu yeye Hana deni!!

Kakarabati bandari zote na kununua meli, mkitaka muuze mgawane pesa, shauri yenu

Vituo vya Afya na hispitali kajenga, mkitaka viwe vituo vya popo, shauri yenu, yeye Hana deni

Kaanzisha ujenzi wa madaraka makubwa kama busisi ili kuharakisha maendeleo, mkitaka msyaendeleze, mtajijua wenyewe, yeye keshasepa na Yuko kwenye ulimwengu mwingine kabisaaa!!

Wamachinga kawafanya wajione kuwa nao Wana haki ya kufanya biashara, mkitaka watimueni, Hana deni

Bwawa la umeme Stiglasgoji, mkitaka liwe bwawa la kunyweshea mifugo Aina ya swala,Simba, mbweha, chui, tembo, na mamba kuogelea au mahali pa kwenda mtu kuogelea, Sawa, yeye Hana shida

Miradi ya maji karibu kooote nchini, mkitaka fumueni na muanze kuwauzia wananchi maji, kwake yeye ni Sawa!!
 
Nchi hii haiwezi kuongozwa na “mzungu” wa 🇧🇪
 
Aya mambo unaweza kuyachukulia mzaha lakini ndio itakavyokuwa.

Leo asubuhi nimeona kwenye status ya mtu kuna kabinti kadogo tu kanalia eti kwa sababu JPM amefariki kabla yeye ajamuona kwa hiyo ameshindwa kutimiza ndoto yake.
 
Mkuu nilitaka nikupe milikes mingi kama ya kule instalive nkaja gundua kuwa hapa ni JF.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Aya mambo unaweza kuyachukulia mzaha lakini ndio itakavyokuwa.

Leo asubuhi nimeona kwenye status ya mtu kuna kabinti kadogo tu kanalia eti kwa sababu JPM amefariki kabla yeye ajamuona kwa hiyo ameshindwa kutimiza ndoto yake.
Mkuu, Mimi Naamini ndivyo itakavyokuwa, utawala Bora wanaweza kuwa wanamrejea Hayati JKN, lakini uchapa kazi watamtaja tu Jembe JpM
 
Mkuu na ule mdaraja wa wami wakisema wasiumalizie ili ile minguzo ya mchina wawape wanajeshi wawe wanaluka viunzi na kufanyia mazoezi ni wao tu JPM wa watu yupo mawinguni kwa baba.
 
Mkuu na ule mdaraja wa wami wakisema wasiumalizie ili ile minguzo ya mchina wawape wanajeshi wawe wanaluka viunzi na kufanyia mazoezi ni wao tu JPM wa watu yupo mawinguni kwa baba.
Good
 
Member since 2021 March 18.
Pole mjane.

Kwa hiyo wewe uliyejiunga 2017 ndiyo unajiona Mkongwe? Na walio na zaidi ya 10yrs tusemeje? Angalia hoja yake na siyo kwenda kuchungulia profile yake kujua kajiunga lini? Umenifanya hadi nikuzoom wewe unaedharau waliojiunga hivi karibuni. Punguza utoto.
 
wapiga kura sindio hawa toka 2015 wanatembea na vyeti mtaani mpaka 2025, Baba zao na ndugu zao walootumbuliwa kisa vyeti feki, waliobomolewa nyumba kisa sio wa kanda mpendwa? Au unaongelea wapiga kura wapi??.
 
Kumbe Kusifu na Kuabudu kunaendelea hadi leo!
 
Akili zako ni chache saaana mkuu,

Unadhani watu wanamtaja Hayati Sokonne Kwa sababu ipi, ni kutaka kumwabudu siyo??

Kunywa kwanza maji ya nazi upunguze uasubuhi kichwani mkuu
Unamlinganishaje Sokoine na Huyo jamaa yenu mnayemwabudu na kumsifu kama MUNGU vile.
 
Irani yachama itaandika JpM(Rais Magufuli),kweli chadema watakua wendawazimu yote iandikwe kuhusu Huyo!!!!
 
Teh! Kwani kulitaja ni kosa la jinai?
 
Kwa hiyo wewe uliyejiunga 2017 ndiyo unajiona Mkongwe? Na walio na zaidi ya 10yrs tusemeje? Angalia hoja yake na siyo kwenda kuchungulia profile yake kujua kajiunga lini? Umenifanya hadi nikuzoom wewe unaedharau waliojiunga hivi karibuni. Punguza u.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…