Nafarijika sana na nyuzi kama hizi!, angalia tarehe ya bandiko langu hili
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...
Kilichofanya nikafarijika ni kukuta JF bado tuna few people ambao ni bonafide genuine. Watu wengi humu JF ni fake sana, hivyo watu genuine wakweli halisi toka ndani ya nafsi zetu, tunahesabika!, wewe Mkuu
Senior security ni one of them, big up for this!.
Kitendo cha kusema "Mimi simpendi Makonda, hata nyuzi zangu zinaonyesha hilo kwa uwazi kabisa lakini akigombea Urais nitamuunga mkono" hii maana yake na wewe umebaini kuwa licha ya mapungufu yake yote ya kibinaadamu, ubishoo, siasa za sanaa za maigizo, lakini unakiri Makonda ana kitu ndani yake hivyo akiishika hii nchi, itanyooka!.
Watu wa kweli wa type hii ndio wale watu watetezi wa kweli wa wanyonge, kwa hoja kuwa mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!.
Kama speed hii Makonda aliyoanza nayo, sio nguvu ya soda, na ataendelea na mchakamchaka huu hadi 2025, namshauri Rais Samia, awape wapinzani kila wanachotaka, katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, a level playing field na bado wataambulia patupu!.
Kwasababu Makonda ni yule yule Magufuli!, Paulo huyu wa sasa ni reincarnation ya Magufuli, hivyo CCM itakomba kila kata, kila jimbo, kila kitu! Kwasababu
Kwanza Makonda ameifufua CCM kuendelea kupendwa na kukubalika
Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!
Pili
Nikimwangalia Makonda, mambo anayoyafanya namuona kama Magufuli na tatu nauliza tena na tena
Bado kuna ubishi kuwa hiki ni chuma? Je, chuma hiki ni chuma kingine ila ni kama kile au chuma hiki ni kile kile kimerejea kivingine?
P