CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
==
Katika hotuba yake bora ya kihistoria ya kufunga mwaka wa 2024 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzània Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameitangazia Tanzània na Dunia kuwa mwaka 2025 utakuwa ni mwaka ambao Serikali yake itajikita zaidi katika kuvuta na kutumia mitaji ya sekta binafsi katika kukuza Uchumi Jumuifu wa Taifa la Tanzània.
Mhe Rais Dkt Samia katika hotuba yake hiyo ameitaja miradi kadhaa ya mifano iliyoko chini ya PPPC ambayo imefikia hatua mbalimbali za Utekelezaji wake kama Mafanikio ya wazi ya Serikali anayoiongoza kwa Mafanikio ya awamu ya 6.
Rais anasema mpaka Sasa tuna jumla ya miradi 74 inayoendelea katika hatua tofauti tofauti chini ya PPP na PPPC.
Mtakumbuka PPP Tanzània pamoja na uwepo wake kwenye Sheria kwa zaidi ya miaka 15 lakini haikuwahi kuwa na miradi yoyote "serious" isipokuwa leo chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambae ndie anayesimamia sera zote za maendeleo kwenye nchi hii hakuna ubaya tukimpongeza kwa kumchagua tena Oct 2025.
Tanzània ni Kweli Tunaweza kubishana katika mambo mbalimbali lakini kamwe hatuwezi kubishana kuhusu utendaji kazi uliotukuka wa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan.
====