Renegade
JF-Expert Member
- Mar 18, 2009
- 7,221
- 6,940
CCM ni Chama, Mgombea ni wa Chama, Chama kina stronghold nyingi,Chama ni wanachama, Mh. Rais Samia akisimama kama Mgombea wa Chama ni kazi ya chama kuhakikisha kuwa anashinda.Huu Uzi ningependa usomwe kwa umakini, na tuweke siasa za mihemuko pembeni.
Ni dhahiri CCM watamsimamisha SSH Kama Mgombea wao wa uraisi,lakini ukweli lazima usemwe sioni Samia akitoboa kwenye sanduku la kura, kwenye uchaguzi ulio huru na haki kwa sababu zifatazo.
- Samia hana strongholds hata moja ambayo ina wapiga kura wengi, asikudanganye mtu,ata marekani Kuna strongholds za Republican na Democrats, mgombea yeyote wa Republican anakuwa ashajihakikishia ushindi wa, Texas, Indiana, South Carolina, na Ohio. na Mgombea yeyote wa Democrats anakuwa ashajihakikishia ushindi kwenye majimbo ya California, Illinois, Deleware, Newyork, DC, n.k
Samia hana strong holds popote hapa Tanzania, Kanda ya ziwa hawezi toboa, Kasikazini hawezi toboa, Dar hatoboi, mikoa ya Iringa na Mbeya hatoboi,mikoa ya kusini haielewekagi.
- Maisha magumu Sana aisee, nipo kwenye ground, maisha magumu hatari,watu ata hawajui kuwa Covid-19 na Vita ya urusi imechangia vitu kupanda Bei, wenyewe wanachojua ni kuwa Samia ndo amepandisha vitu, na Samia ata hakemei, anapiga kimya na mwishowe anakuja sema vitu vitazidi kupanda bei. Mafuta ya kula Lita 7000, sabuni mche ni 3500, ngano Ni 2000,n.k
- Ajira hakuna, mmesikia wenyewe juzi kuhusu magereza,afya anaajiri watu elfu mbili, Elimu ambayo ilikuwa na ajira nyingi anaajiri walimu elfu, ajira hamna kabisa, mbaya zaidi wananchi wamekaririshwa kuwa ufisadi umerudi chini ya Samia,
Ili Samia ashinda uchaguzi 2025 hana budi kuteka, kutesa, nyanganya fomu za wapinzani, wawekee mapingamizi wapinzani, kuingiza kura vituoni n.k hapo atashinda.
Huo ndo ukweli whatever you like or not.
Kupanda kwa bei sio matokeo ya Rais Samia, Bei zilipanda wakati wa Nyerere na pia hali ilikuwa ngumu sana kiasi ambacho watu walivaa magunia, walifua kwa sabuni za majani ya mpapai, Wakati wa ruksa pia sio kila mtu alikuwa na hali bora, Wakati wa mkapa mambo hayakuwa Rahisi, Hata wakati wa Kikweye kuna watu walilala na njaa wakati wengine wanashiba. Wakati wa Mzee baba ndio usiseme kila mtu alkuwa anadai hali ngumu.
Kwa hiyo acha kumbagua Samia, Inlfation upanda na kushuka, ila hii ya sasa lazima itakuwa zaidi maana imegusa kwenye Mafuta, na Mafuta ndio nyenzo ya kila bidhaa na uzalishaji na usambazaji bidhaa.
Vita ya Ukraine kila mtu anataharuki, Mkubwa wetu Marekani hali ya mafuta mbaya, karibu dunia nzima.
Na Tanzania ni sehemu ya Dunia hatuwezi kujitenga na matatizo.