750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

Ahsante kwa muongozo mkuu
 
Mkuu humu kuna mafogo hatari.

Uzuri wa humu muosha magari anamtukana boss wake, muuza vitunguu sokoni anavimba kuwa anafanya kazi UN Geneva.

Uamuzi ni wako uwe nani humu.

#fakeituntillyoumakeit#
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
My current job mkuu maana mwaka juzi nmekataa ajira yenyenkukaribia huo mshahara.
Mkuu hata yeye anafanya kazi halafu anafanya ninachofanya ndichonkilichotufanya tufahamiane na kuwa marafiki wakubwa mkuu.
Sawa sawa kaka.
 
Unasave vizuri tu, pamoja na vyakula kupanda bei
Familia ya watu 4
Mume, mke, watoto 2

Mchele 90k
Unga 60k
Maharage 20k
Nyama 20k
Umeme 30k
Gesi 50k
Mengineyo 200k
Kodi 150k
Jumla 620

Baki 130k
Hapo Kama anawatu wamemuwezesha kufika alipofika na wanauhitaji hawezi acha kuwategemeza pia.
 
Hii mechanism nashindwa kuelewa inakuwaje kuna ukame na mifugo ni mingi singida
 
Yani brother ungejua kama wengine tunatamani hata nusu ya unachopata ili tu survive, being jobless sucks, inflicts and hurts, na hasa ukiwa na majukumu, yaani mbona hata 300k nyingi sana
 
Ungeniuliza mahala pengine sio humu jeifu ningekujibu 750k unaishi vizuri tu na pisi kali ungekata
Ila kwa kua umeuliza jukwaani hapa nitajibu
750k ni matumizi ya mafuta tu ya gari yangu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii comments imejibu kila kitu
 
Wakuu nilikuwa nauliza tu kama 750k ni takehome inayoweza kumfanya mtu aishi kidogo standard life.

Maana isikute nadharau kumbe naweza kufanya kitu.
Jibu ni Ndio na unaweza Kuishi vizuri Hata kwa Take home ya laki6 tu

Twende kwenye mahesabu ya msingi sasa, tumia rule of 50/30/20
50 ni yale matumizi ya LAZIMA kama kodi,chakula,maji,umeme,Ada (375,000/=)

30 Hii ielekeze kwenye mahitaji yako sasa,labda kununua furniture ama hitaji lolote ambalo kwako ni la muhimu kwako kwa kipindi husika(225,000/=)

20 hii ni saving na kulipa madeni ya hapa na pale(150,000/=)

NOTE;750,000/= Is not a life Sentence kwamba hautapata hela zingine zaidi Nope, Hela zingine kama za semina,vikao vya nje ya kituo na overtime unaweza zitumbukiza kwenye matumizi ya lazima na ukaongeza Saving yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…