750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

Gharama kivipi tena uku umesema mifugo bei rahisi na ugali wa mtama upo na viazi shida ipo wapi kuku bei rahisi ni mwendo wa kubadili mboga tu
Nimeishi huko huwez fananisha na sehemu zingne sawa mifugo ni bei rahisi lakini upatikanaji wa vyakula vingne ni shida kuna ukame mwingi sana kule sio utani,maji ni shida kuna baadhi ya sehemu watu wanakunywa maji machafu hakufai kule
 
Somo taken
Vizuri, tujenge utamadani wa kuweka akiba na tuwafundishe Watoto wetu tabia ya kuweka Akiba Wakiwa wangali Wadogo.

Tukijenga utamaduni huu kwenye familia zetu, Kuna uwezekano tukaondokana na mabalaa ya njaa pamoja na Umasikini hivyo Kuzalisha watu wenye vipato vya wastani na Matajiri (Akina Mo Dewji wamekuta Wazazi wao wameweka Akiba ya Mali na mitaji).
 
Kweli siku hizi mwanza maisha yanakuwa expensive sana, kuanzia nyumba za kupanga bei kubwa kama za Dar tuu ingawa wenye nyumba wanajenga nyumba nzuri sana, misosi bei kubwa.

Maji ya kunywa yanayouzwa 600 Dar kwa mwanza ni 1000. Cha urahisi kule ni usafiri tuu
Vyakula vipo bei sana...samaki bei yake ipo juu ndio usiseme mtu kama haupo mwanza unaweza dhani kila siku tunakula samaki huku
 
Back
Top Bottom