750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

Mbona hiyo ni kubwa sana. Mimi nalipwa 70,000/- kwa mwezi na nina familia, maisha yanaenda.
 
Aiseee maisha kweli yanataka tafakari, yaani mimi 400,000 wiki imekwisha.
Siyo siku wiki tu ata ukitaka kwa siku itaisha na ukitaka kwa mwezi itaisha tu wewe mwenyewe jinsi unavyo panga bajeti zako ukitaka lakini nne imalizike mwezi itawezekana
 
Ishi kulingana na kipato chako mkuu.

Ukipata elfu 50 kwa mwezi ishi kielfu 50 ,ukipata 750k pm ishi hivyo hivyo....Hela huwa haitoshagi hata ulipwe 10m per month maana matumizi nayo yataongezeka ,cha msingi ni kuishi kulingana na kipato unachoingiza.
Uko sahihi mtu asiforce kula kuku wakati uwezo wa dagaa.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu hawa-save hata mia na wanapokea kila mwezi.
Akipokea tu mshahara anaenda bar ya karibu anamwagilia moyo tu. Siku 4 tu mshahara kwisha, akili inarudi mahali pake maisha yanaendelea.
Hiyo ndio monthly routine.
Kuna mtu anasoma ujumbe huu anatabasamu tu anatamani ku-like anajisemea maisha ndio hayahaya.
Kwa shida gani ufe halafu huku nyuma watu wanagombania mali zako!
 
Kwa nyanda za juu upo sahihi mkuu ila kwa Singida hapana aisee maisha ya Singida ni shida kuna Tatizo kubwa la maji na chakula na ukame ni mkubwa sana kule ,nimeishi Singida miaka mingi sana ,mambo ya kula ugali wa mtama,mihogo na viaz vitamu kila siku yaliboa sana,kitu ambacho ahueni Singida ni mifugo kama mbuzi na kuku bei yake n ndogo sana lakini kwa maisha ya kawaida Singida ni gharama
Gharama kivipi tena uku umesema mifugo bei rahisi na ugali wa mtama upo na viazi shida ipo wapi kuku bei rahisi ni mwendo wa kubadili mboga tu
 
Hpo inategemea na mkoa na mazingira ya kazi
Kweli,kwa morogoro,mwanza,mbeya,iringa,katavi,kahama na hata dar hiyo pesa inakusongesha vizuri kabisa,ila ukipita kwenye kimji kama cha arusha usishuke kwenye basi,usile hata mshikaki,utakuwa umeilaani hela yako,itaisha ndani ya siku nne,arusha,moshi,bagamoyo,kinondoni() hivi vi mji vina majini hela
 
Bora ukose hela ya Kula lakini usikose hela ya kuweka Akiba 🤗

Manake Kuna watu Wana kula hadi Akiba alafu wakikwama kwa kupata tatizo hata la shilingi 30,000 lazima wapige simu kukopa. Hii ni mbaya Sana kwa kweli
😂😂😂😂 aloooo
Yan kwamba tunakula hadi akiba
 
Back
Top Bottom