750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

Ukiingiza kwenye anasa ni pesa kidogo sana iyo,pesa ni matumizi yako tu hakuna pesa nyingi isioisha kwenye matumizi

Mimi nmewahi kutumia 17M ndani ya masaa 3 tu,Ingia Hardware uone
Uliitumia kwenye nini Mili 17 kwa masaa matatu Tanzania hii tajiri?
 
Kweli siku hizi mwanza maisha yanakuwa expensive sana, kuanzia nyumba za kupanga bei kubwa kama za Dar tuu ingawa wenye nyumba wanajenga nyumba nzuri sana, misosi bei kubwa.

Maji ya kunywa yanayouzwa 600 Dar kwa mwanza ni 1000. Cha urahisi kule ni usafiri tuu
Wahamiaji ni wengi sehemu ikiingiliwa na wageni maisha yana panda mahitaji yana kuwa juu mfano wa Nyumba za kukodi
 
Wahamiaji ni wengi sehemu ikiingiliwa na wageni maisha yana panda mahitaji yana kuwa juu mfano wa Nyumba za kukodi
Sema ninachokubali Mwanza wenye nyumba wanazipangisha wanajenga na kuwekeza haswa nyumba nzuri ya kisasa, hata mtu unapotoa hela yako unasema kweli naishi pazuri.

Wanajali sana nyumba za kupangisha tofauti na Dar unapanga gofu halafu bei imesimama bado matatizo kibao.
 
Mwenyewe nilimshangaa huyo SILULU
Unashangaa nini Singida maisha ni magumu ,mkalama na Iramba nakufahamu na nimewahi lima mahindi huko,maji wanachota kwenye visima na maji yao kwa kiasi kikubwa yana chumvi mpaka vitoto vikikua vinakuwa na meno mekundu,Ikungi na Manyoni hali ni ile ile ungeniambia kwa kilimo cha alizeti na vitunguu sawa ,tusidanganyane hali halisi ya Singida ni ngumu huwezi fananisha na mikoa ya Rukwa,Ruvuma,Mbeya,Morogoro au Manyara
 
Mwenyewe nilimshangaa huyo SILULU
Mimi mwenyewe nimeishi mjini na kijijini pia navifaham vijiji vingi mpaka ndani mtekente huko unaweza ukalima mahindi au maharage,yataota vizur tu lakini likija jua linawaka mahindi yanaanza kukauka hata kabla ya kukomaa ndiyo maana wanalima sana mihogo,viazi vitamu ,mtama, ulezi na uwele mazao yanayostahimili ukame,
 
Wakuu nilikuwa nauliza tu kama 750k ni takehome inayoweza kumfanya mtu aishi kidogo standard life.

Maana isikute nadharau kumbe naweza kufanya kitu.

Mmm uwe na mke mpanga bajeti na mchungu na maisha ndio utatoboa laa ni ngumu hawa wake zetu wanao taka kila siku elfu 20 na ndani kuna mchele unga maharage mafuta vitunguu roba ya sabuni unga sabuni mche ges mkaa maji nyama kwenye freg kuku samaki na bado kila siku anakwambia matumizi ya nyumbani elfu 20
 
Back
Top Bottom