Abby Chams: Sijawahi kula miguu ya kuku wala firigisi, wala sijawahi kusikia sehemu inaitwa Mburahati

Abby Chams: Sijawahi kula miguu ya kuku wala firigisi, wala sijawahi kusikia sehemu inaitwa Mburahati

Umasikini mbaya sana.

Kwa maisha ya watanzania yalivyo magumu,mtu akisika stori kama hizi za mtanzania mwenzao wanaona kama anaigiza.

Huyu Binti ukimsikia tu akiongea accent yake ya kiswahili si ile ya kibantu na anachapia sana maneno ya kiwahili,means either hajakulia bongo au ni wale mboga Saba kupitiliza.

Mtu kama huyu akisema hajawahi kusonga ugali mnamshambulia kwa matusi.

Akisema hapajui mburahati na hajawahi kupasikia mnamshambulia. Kuna Binti niliwahi kuwa nae kwa mahusiano anasema hapajui kabisa mbagala na akazaliwa Dar. Mbagala na umaarudu wote lakini Kuna watu hawapajui kabisa na Wala siyo celebrities,sembuse mburahati au kigogo.

Akisema hajawahi kula miguu ya kuku na firigisi mnaona ana pretend,sasa miguu ya kuku nayo ya kujisifia na kuanza kumshambulia mtu akisema hajawahi kula? Kwa nyama Gani iliyonayo mtu ukitafuna utadhani unatafuna peni ya speedo.

Huyu Binti anashambuliwa sana mitandaoni na wabongo ,ila yote hii ni kwa sababu ya kuona vitu kama tulivyo(umasikini) badala ya kuona vitu kama vilivyo.
Umenena vyema sana
 
Huyo bint ni level nyingine, Kuna siku aliulizwa hua ananunua nguo za bei gani sijui akajibu hua haangalii wala kuuliza bei, ikimpendeza tu anatoa kadi analipia 😀

Wakati wazee wa pangu pakavu mgahawani tu, kila kitu hii shingapi hii shingapi 😀
Kuna watu hapa bongo hawaamini kuwa Kuna wabongo wanaishi kama wapo ulaya,hapa hapa bongo.

Kuna mtoto mmoja wa kishua nilienda kufanya nae manunuzi ya nguo mikocheni,tukaingia maduka ya Woolworth na ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza. Milioni mbili alitoka na nguo hata kwenye begi la mgongoni hazijai. Bei za bidhaa za Woolworth ni balaa na mtu hawazi.

Watu kama hawa wakikuambia hawajawahi kufua nguo tangu wazaliwe unaona kama wanakuletea dharau.

Wakisema ugali ni chakula cha kimasikini unaona wanakufuru Mungu. Pata Hela alafu uone unakula ugali mara ngapi kwa mwezi,labda tu uwe unakula kama mazoea na utamaduni.

Wakati Mimi najichanga ninunue Toyota second hand,Kuna mtu kwao Kuna magari kama kwa lugumi na hakuna Toyota kwenye yard.

Alafu wandishi walivyo wanoko wanamuuliza maswali ya uchokonozi ili awajibu wapate content maana wanajua dogo atasimangwa na watz na contents zao zitaenda viral.

Juzi kwenye janga la kariakoo huyo Binti kajitoa sana kwa kuchangia hadi kwenye list ya waliotajwa na waziri mkuu yumo,hao macelebs wao wanaojifanya Wana Hela sana ndiyo kwanza wanatapeli kwa kuchangisha michango watz wenye njaa.
 
Akiwa katika kipindi cha Jirani kupitia Crown FM, mwanamuziki Abby Chams anasema hajawahi kula miguu ya kuku wala firigisi hazijui.

Mwijaku akamuuliza unapajua Mburahati? Akamjibu hajawahi kupasikia ndio mara yake ya kwanza kupasikia.

NB
Huyu msanii Abby Chams kipindi cha nyuma aliwahi kusema hajui kusonga ugali.

Hao ndio macelebrity wa Bongo
Mkuu inaezekana kabisa.
Mtu unaweza kuhisi maisha unayoishi wewe ndiyo wanayoishi wengine lakini kumbe hapana.
Nafahamu watoto kadhaa hawajawahi kupanda daladala, mara nyingi wanakuja kupanda daladala chuo na hapo kwa sababu wanataka ule ufree hawataki kuongozana na madereva wa home, wanataka kwenda wanakotaka
Pasipow kufuatiliwa.
 
Broo mbona hata mimi pia siijui buza ,mbagara saku.....kinyerezi.......kibangu.......mbezi kwa magufuri ...........so hiyo ni kawaida tu ........usishangae........sema angeulizwa kama aijui dildo au m.b.o.o.o.o.o.o harafu mngesubilia majibu
 
Akiwa katika kipindi cha Jirani kupitia Crown FM, mwanamuziki Abby Chams anasema hajawahi kula miguu ya kuku wala firigisi hazijui.

Mwijaku akamuuliza unapajua Mburahati? Akamjibu hajawahi kupasikia ndio mara yake ya kwanza kupasikia.

NB
Huyu msanii Abby Chams kipindi cha nyuma aliwahi kusema hajui kusonga ugali.

Hao ndio macelebrity wa Bongo
Anajua miguu na firigisi ndio mboga zao za bei rahisi huko ughaibuni alikokuwepo!
 
Tunaangalia kipaji hayo mengine ni udaku usio na maana kiufupi ana kipaji itoshe kusema hivyo mengine ni kuchimbana ovyo tu
Huu ni uwongo.

Aliyekuambia wabongo mnaangalia kipaji nani? Tangu lini? Wabongo mnamsapoti mtu/msanii mwenye scandals na hekaheka.

Mngekuwa mnaangalia kipaji mngemsuport Belle 9,ila mmempa kisogo kisa Hana hekaheka na scandals za kiwaki wenyewe mnaita kiki.

Huyu dogo si msanii bali ni mwanamuziki. Anaujua muziki kuliko hata zuchu. Anajua kupiga karibia Kila kifaa cha muziki Tena kwa ufasaha na kwa kujiamini,ila Kuna watu humu humu kwenye huu Uzi wanasema hawamjui. Why? Hana heka heka,ndiyo mmeanza kumchokonoa ili angalau aende na hizo kiki mjini. Ila yuko real hafeki kama hao mastar waliotoka kwangu pakavu.

Ukiangalia ile nyimbo ya wasanii wa kike "super woman" utaona jinsi alivyo poa kupiga ile nini sijui mnaita.

Nyimbo ya maomboleza ya Magufuli ya wasafi WCB kaimba kidogo ila kaua,coz ana kipaji. Nyimbo yake na Mario pia Kali sana pia. Tusapoti kipaji.
 
Nilikutana na rafiki yangu mmoja wa Oysterbay akiwa New York. Aliondoka Tanzania mara baada ya kumaliza sekondari kwenda kusoma chuo Marekani akabakia kufanya kazi huko.

Siku moja nikamuuliza kama kashawahi kufika Buguruni, alikuwa hajawahi kufika.

Alikuwa hana sababu ya kwenda Buguruni.

Alisema kwao Oysterbay, alisoma Oysterbay na Tambaza, hakuwa na ndugu wala rafiki Buguruni, sasa angeenda Buguruni kufanya?

Akarudi Tanzania likizo, ikabidi aende kutembea tu Buguruni.
 
Miguu ya kuku na vichwa vinauzwa kikatili sana. Utakuta miguu imesokomezwa kwenye midomo ya kuku hadi umetoka kisogoni
IMG_0675.jpeg
 
Kinachokushangaza hapo ni kipi?

Kiumri, huyu ni binti mdogo sana, na kasoma nje ya nchi. Maana yake maeneo mengi ya mji huo wa Dar hajayafaham. Hivyo, ni kweli kutokana na mazingira aliyokulia.

Kuhusu kutokula miguu ya kuku; hilo ni jambo la kawaida kwa watu wanaotoka familia zenye kipato. Kama sisi kijijini kwetu mgeni hawezi kupakuliwa miguu ya kuku au mgongo wa kuku, vipi mtoto aliyezaliwa familia inayojiweza?
Jaribu kuacha negative perceptions kwenye kila jambo
Iweje mumjadili mtu ambaye hajala miguu ya kuku tu wakati mimi ambaye sijawahi kula mkia wa kuku, makende ya kuku wala masikio ya kuku hamjawahi kunijadili.
 
Nilikutana na rafiki yangu mmoja wa Oysterbay akiwa New York. Aliondoka Tanzania mara baada ya kumaliza sekondari kwenda kusoma chuo Marekani akabakia kufanya kazi huko.

Siku moja nikamuuliza kama kashawahi kufika Buguruni, alikuwa hajawahi kufika.

Alikuwa hana sababu ya kwenda Buguruni.

Alisema kwao Oysterbay, alisoma Oysterbay na Tambaza, hakuwa na ndugu wala rafiki Buguruni, sasa angeenda Buguruni kufanya?

Akarudi Tanzania likizo, ikabidi aende kutembea tu Buguruni.
Vishua hao.
 
Kinachokushangaza hapo ni kipi?

Kiumri, huyu ni binti mdogo sana, na kasoma nje ya nchi. Maana yake maeneo mengi ya mji huo wa Dar hajayafaham. Hivyo, ni kweli kutokana na mazingira aliyokulia.

Kuhusu kutokula miguu ya kuku; hilo ni jambo la kawaida kwa watu wanaotoka familia zenye kipato. Kama sisi kijijini kwetu mgeni hawezi kupakuliwa miguu ya kuku au mgongo wa kuku, vipi mtoto aliyezaliwa familia inayojiweza?
Jaribu kuacha negative perceptions kwenye kila jambo
Pumba
 
Back
Top Bottom