Umasikini mbaya sana.
Kwa maisha ya watanzania yalivyo magumu,mtu akisika stori kama hizi za mtanzania mwenzao wanaona kama anaigiza.
Huyu Binti ukimsikia tu akiongea accent yake ya kiswahili si ile ya kibantu na anachapia sana maneno ya kiwahili,means either hajakulia bongo au ni wale mboga Saba kupitiliza.
Mtu kama huyu akisema hajawahi kusonga ugali mnamshambulia kwa matusi.
Akisema hapajui mburahati na hajawahi kupasikia mnamshambulia. Kuna Binti niliwahi kuwa nae kwa mahusiano anasema hapajui kabisa mbagala na akazaliwa Dar. Mbagala na umaarudu wote lakini Kuna watu hawapajui kabisa na Wala siyo celebrities,sembuse mburahati au kigogo.
Akisema hajawahi kula miguu ya kuku na firigisi mnaona ana pretend,sasa miguu ya kuku nayo ya kujisifia na kuanza kumshambulia mtu akisema hajawahi kula? Kwa nyama Gani iliyonayo mtu ukitafuna utadhani unatafuna peni ya speedo.
Huyu Binti anashambuliwa sana mitandaoni na wabongo ,ila yote hii ni kwa sababu ya kuona vitu kama tulivyo(umasikini) badala ya kuona vitu kama vilivyo.