Pre GE2025 Abdulrahman Kinana: Chaguzi za 2019 na 2020 zilileta hofu, Mwaka 2024 na 2025 zitakuwa za Huru na Haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Aache uongo....
 
Yaani mimi kupiga kura tena kwa Tanzania hii sijui ...

Watu wengi wamekata tamaa kusimama kwenye foleni muda mrefu huku mnasikia viongozi wakubwa wakisema... 'Mpige kura msipige CCM ndiye mshindi'

Kinana bado sijaamini kauli yake
Jamaa lengo lao tukate tamaa, mimi big no nitapiga ili wajue kuwa sikuwachagua hata kidogo
 
Your browser is not able to display this video.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekusudia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuwa huru na haki.

Kinana amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa ACT- Wazalendo unaofanyika leo Machi 5, 2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.

Pia Soma:
- Rais Samia: Uchaguzi utakuwa huru na wa haki
 
Lakini si tutaiba kama kawaida, maana nilishapata hofu tusije tukapoteza majimbo
 
Kuna kamsemo ka kitoto kua mwanasiasa akikusalimia "habari ya asubuhi" basi toka nje kuhakiki kama kweli kumekucha.
Hawa jamaa ni waongo sijapata ona.

Hao mawaziri lukuki wapo tayari kupoteza nafasi zao, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya nk aisee sio rahisi kwa nchi hii.
 
Aache maneno matupu mbona amegomea Tume Huru na Katiba Mpya?
Si ndio hapo Sasa, yaani anategemea watu waamini kauli za mdomoni huku hawataki tume huru ya uchaguzi? Yaani bado anataka watu washiriki uchaguzi kisha watoe nafasi mbili tatu za hadaa kuonyesha kuwa Kuna uchaguzi huru. Wawape ACT maana hao ndio hiyo wanaamini kwenye mbeleko ya ccm.
 
Viongozi wavuta bange,ifikie hatua Bangi iharalishwe tu.
Watu wazima ovyo.
Ccm ndo adui wa maendeleo wa Nchi hii.
Akili ndogo kutaka kuongoza akili kubwa.
Kina Kasheku kwenda Dubai kusoma mkataba wa Bandari🐍.

Mpaka mda huu ilitakiwa mshtakiwe,Kwa vile wananchi wengi wa vijijini ni Majinga majinga ndo afueni yenu.
 
Sheria za Uchaguzi ndio za kubadili , hatuwezi kuingizwa kingi kwa kauli za Kinana , Mwenye Tuhuma za kuiba kura 2015 , Akiongoza ofisi ya Masaki .

Nani amesahau ?
kuzira na kususa hakutasaidia wala kubadili chochote....

ukiona hakuna haja kushiriki uchaguzu kaa kando na uwe mtulivu, acha watakaoshiriki wafanye hivyo kwa haki, uhuru na namani...

we watizame tu kwa tv...
 
CCM WAKIKUAMBIA KUMEKUCHA USIAMIMI TOKA KWANZA UKACHUNGULIE
MARIDHIANO HAWATAKI
KATIBA MPYA HAWATAKI
TUME HURU WAMEBADILISHA JINA TU TUME NI ILE ILE YA CCM
 
'If voting changed anything, they'd ban it' - msemo huu nimeukopa
 
THIS IS NONSENSE!

Haya maelezo yalipaswa kutolewa na tume , tena tume HURU ya Uchaguzi, na waombe radhi kwa Watanzania kutokana na ukandamizwaji mkubwa wa HAKI na wizi wa kura wa kupindukia ambao haujawahi kutokea tangu mfumo wa vyama vingi kuasisiwa nchini,


Rais Samia ambaye ni mwanaCCM Pamoja na Kinana yeye kama Makamu Mwenyekiti wa chama kimojawapo cha SIASA Hana mamlaka ya kutupa au kututoa hofu maana yeye hayo mamlaka Hana Kwani naye kinandharia alipaswa kuwa muhanga wa huo ukandamizwaji, unless sasa tukubaliane kuwa CCM wao ndio wanaamua Uchaguzi uwe HURU au vinginevyo .


Hawa watu sijui wanatuonaje Watanzania, wanafikiri Sisi ni mazombi??
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM yangu anakiri tulibaka uchaguzi 2019/2020.

Jasiri haachi asili
 
Mheshimiwa askari Kinana mimi sina shida na kauli yako huo ni wajibu wala haitaki shukurani.Sisi tunataka iwepo sheria ya kuwepo uchaguzi ulio huru na haki bila mkono wa mtu kutumia cheo au wadhifa kufanya kinyume.Pia tumeshuhudia mtu wa kawaida sana anaapishwa kulinda na kutetea katiba lakini anaenda kinyume,ndio maana tunataka kuondoa Mungu watu anzia kwenye chama chako ndio mvunjaji mkuu wa katiba kwa kiwango kikubwa.Lakini kama mna mapungufu ya upeo jaribu AI kama msaada.
 
Kinana huwezi kuzungumzia ukosefu wa umeme kwenye viwanda, wewe ni uchaguzi tu? .kwa hiyo uchaguzi wa 2015 ulikuwa wa huru na haki mno?
Lowasa hakuibiwa kura?
Ukiambiwa CCM wanaiba kura unakomaza fuvu kisa buku 7, aliyeongea ukweli huu ni KM wa CCM, bisha tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…