Pre GE2025 Abdulrahman Kinana: Chaguzi za 2019 na 2020 zilileta hofu, Mwaka 2024 na 2025 zitakuwa za Huru na Haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Aliyesababisha hofu yupo chini futi sita
Mifumo iliyopelekea uhayawani ule bado ipo hivyo hivyo. Kwanini kusiwe na tume huru badala ya hadithi za mdomoni? Ni kipi kinawafanya mlazimishe kubaki kwenye mifumo ile ile inayolinda ubatili? Kama mnagoma tume huru ya kisheria, mnapata uhalali gani wa kutaka muaminike kwa porojo za mdomoni?
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekusudia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuwa huru na haki.

Kinana amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa ACT- Wazalendo unaofanyika leo Machi 5, 2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.

Pia Soma:
- Rais Samia: Uchaguzi utakuwa huru na wa haki
This is rubbish! Unaogopa nini kuweka tume huru kama unataka haki?
Hawa msiwaamini , these are thugs! Ujinga mtupu, hilo analoliambia ni tawi la CCM
 
Hata Magufuli kwenye uchaguzi wa 2019/2020 aliahidi hivyo hivyo tena mbele ya mabalozi kwenye sherehe zao za mwaka mpya ndani ya Ikulu,kikichofuata ni uchafuzi baadala ya uchaguzi chini ya uratibu wa tisi!
 
kuzira na kususa hakutasaidia wala kubadili chochote....

ukiona hakuna haja kushiriki uchaguzu kaa kando na uwe mtulivu, acha watakaoshiriki wafanye hivyo kwa haki, uhuru na namani...

we watizame tu kwa tv...
Tunasema hivi, Tanzania hakuna uchaguzi bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Wanaofaidika na mfumo wa wizi hawataki tume huru ya uchaguzi, ili waendelee kuwa na maamuzi ya kiwango Cha ushindi wautakao wao, na kidogo wa kuwapa wapinzani Ili kupunguza kelele.

Halafu wanaohadaa umma kuwa kutakuwa na uchaguzi, wanasema ukichagua mpinzani serekali haitapeleka maendeleo!
 
View attachment 2925116

"Uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utakuwa wa huru na wa haki, wakati nazungumza hivi nina hakika wapo ambao wana mashaka na kauli hii, na hao wenye mashaka wanazo sababu, na sababu zao zinatokana na 2019 na 2020 huo ndio ukweli"

"Sheria tuliyokuwa nayo ya uchaguzi ambayo ilitupeleka kwenye uchaguzi wa 2015 iliwezesha wanachama kutoka upinzani 117 kuingia bungeni, sheria hiyo hiyo iliwezesha karibu asilimia 40 ya madiwani kuingia kwenye nafasi za halmashauri, tulipokuja 2020... msema kweli lazima tuseme kweli"

"Hofu ya watanzania hofu ya wenzangu vyama vya siasa, asasi za kiraia, baadhi ya viongozi wa dini, msingi wa hofu yao ni yale yaliyotokea 2019/2020. Niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan ameamua uchaguzi mwaka huu na mwakani mtaachwa wapiga uamuzi wao utoe tafsiri ya uchaguzi" - Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Chanzo: EATV
Kisheria au utashi wa watawala, je baada ya hapo miaka ijayo akija mtawala mpumbavu kama aliyepita itakuwaje?
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekusudia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuwa huru na haki.

Kinana amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa ACT- Wazalendo unaofanyika leo Machi 5, 2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.

Pia Soma:
- Rais Samia: Uchaguzi utakuwa huru na wa haki
HATA MAGUFULI ALIUELEZA ULIMWENGU KUWA ATAFANYA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI MATOKEO YAKE NI KUWAKAMATA WAPINZANI KUWAJAZA MAGEREZANI KWA KESI ZA MAUAJI KUWATEUA KINA HALIMA MDEE NA WENZAKE KUWAPA UBUNGE hivyo CCM HAIAMINIKI
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekusudia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuwa huru na haki.

Kinana amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa ACT- Wazalendo unaofanyika leo Machi 5, 2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.

Pia Soma:
- Rais Samia: Uchaguzi utakuwa huru na wa haki
Kwa hiyo uchaguzi kuwa huru na haki ni matakwa binafsi ya Rais au ni matakwa ya kidemokrasia na kisheria? Mpaka lini tutaendelea kuongozwa na hulka binafsi za kiongozi
 
Naskia harufu ya udnii,udni udini...
Hawa viongozi wakizeeka watubu basi wapumzike nyumbani wabaki kufanya ibada zaidi...
Sasa mtu mzeeee bado hutosheki unang'ang'ana na dhulma,WIZI na uongo hujiandalii hata pepo njema daah????
 
Tunasema hivi, Tanzania hakuna uchaguzi bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Wanaofaidika na mfumo wa wizi hawataki tume huru ya uchaguzi, ili waendelee kuwa na maamuzi ya kiwango Cha ushindi wautakao wao, na kidogo wa kuwapa wapinzani Ili kupunguza kelele.

Halafu wanaohadaa umma kuwa kutakuwa na uchaguzi, wanasema ukichagua mpinzani serekali haitapeleka maendeleo!
huna dira, huna wagombea mahiri wala makini, huna ishawishi, huna mipango, huna mikakati wala uelekeo, atakuchagua nan? uibiwe isichokua nacho kivip sasa...

Tz hayupo wa kuchagua mihemko na malalamiko...
 
Kabla ya 2005 ccm ndio ilikuwa na uhakika wa kushinda kihalali maana kile Bado kilikuwa kizazi chake. Kwa uhayawani unaoendelea kwenye chaguzi zetu, nakushauri 🌈 unyamaze yu.

Na sio kwamba ccm haiwezi tu kushinda kihalali, Bali haitakaa iweze tena. Imeisha hiyo. Sana sana tutaishia kushuhudia chaguzi zilizopuuzwa na wapiga kura.
 
Hata JIWE alitoaga ahadi hiyo hiyo ,tulichokuja kushuhudia 2019 & 2020 ilikuwa ni AIBU na FEDHEHA kubwa..

Leteni Katiba mpya iliyo bora tume huru + usawa,..vumbi litimke!
 
Kwani uchaguzi HURUMA
View attachment 2925116

"Uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utakuwa wa huru na wa haki, wakati nazungumza hivi nina hakika wapo ambao wana mashaka na kauli hii, na hao wenye mashaka wanazo sababu, na sababu zao zinatokana na 2019 na 2020 huo ndio ukweli"

"Sheria tuliyokuwa nayo ya uchaguzi ambayo ilitupeleka kwenye uchaguzi wa 2015 iliwezesha wanachama kutoka upinzani 117 kuingia bungeni, sheria hiyo hiyo iliwezesha karibu asilimia 40 ya madiwani kuingia kwenye nafasi za halmashauri, tulipokuja 2020... msema kweli lazima tuseme kweli"

"Hofu ya watanzania hofu ya wenzangu vyama vya siasa, asasi za kiraia, baadhi ya viongozi wa dini, msingi wa hofu yao ni yale yaliyotokea 2019/2020. Niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan ameamua uchaguzi mwaka huu na mwakani mtaachwa wapiga uamuzi wao utoe tafsiri ya uchaguzi" - Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Chanzo: EATV
Kwani uchaguzi HURU na WA haki ni lazima upinzani ushinde ??

Anyway hio ni fursa nzuri kwa upinzani kujijenga hakuna mtawala atakubali kukupa usawa kirahisi au kukufungilia magoli yote umfunge
Fursa yoyote inayopatikana ni vyema mkatumia effectively sio kusasa susa kijinga
MWISHO wa siku hata msiposhiriki watawala hawajali Nyie ndo mnaumia
Wazee wetu wangesusa susa wakoloni wasingeachia nafasi
 
Daaaa nawatazama TU viongozi wa Tanzania walivyo na uchu na madalaka

CCM embu kuweni wazalendo na taifa msifanye vitu kwa maslah binafsi
Saivi kila mtanzania anaelwa huwezi danganya hata mtoto wa miaka mitano
Teuweni mtu mwingine tofauti na Samia Ili msibolonge25
 
Back
Top Bottom