Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hee hawakomi? Kweli wamerogwa si bure
wakome kwani Mabosi wao si Tupo nao hapa hapa HAWATAJWI.
JK kimyaaa kama hasikii vile!
Yaani spare inaoka Tz kwenda Hon kong, wakati ndio traffic center, hata mimi ningelihisi kuna kitu.Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.
Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.
Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.
![]()
![]()
![]()
Soma vizuri post,gear ya kwanza ilishikwa na kuwa examined august 2 na ya pili imeshikwa jana august 15.Hizo mbona ni gear mbili tofauti? Au ni za matukio tofauti? Isije ikawa mambo mengine mipakazo tu. Na je, hao wanaokamatwa ni watanzania kweli?
Mwakyembe chunguza hili sakata vizuri tafadhali.
Kuonyesha aliyetuma ana akili ndogo, kafikiria kua akituma hii kitu ikiwa ndani ya hiyo metal gear basi hatoshtukiwa, ati ataonekana tu anapeleka hii bidhaa labda kufanyia kitu flani, sawa haitokuwa detected kwenye machine kwa sababu ya hiyo metal cover, ila sasa tuje kwenye ukweli, unajua HK wanavyowasuspect watanzania, hata kama ni wewe compare Hong Kong na Bongo, unadhani Hong Kong hakuna metal gear kama hizo ambazo unaweza ukapata tena kwa bei nafuu zaidi na quality kubwa zaidi? ni mjinga ndiye atakayenunua bongo afu aisaifirishe ikafanye kazi Hong Kong maana kuna gharama za ndege kuisaifirisha pia.. Hahahaha! muuza madawa naye stupid hivi, bongo bna
Tanzania tunastahili tuzo katika hii biashara!