Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine

Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine

Naona Christopher Michael Coke( a.k.a The Dudus) ameweka kambi TZ tena atakuwa airport akisimamia miradi yake bila bugudha!
 
c.c.m anzeni kutafuta njia nyingine ya kupata hela ya kampeni, hii ya madawa naona inabuma.
 
Aise kwa ustadi huu wa kuficha basi nimevulia kofia punda wa Tanzania!!! Yaani tungekuwa tunatumia akili hizo kuvumbua kazi za ujasiriamali na kubuni biashara halali au kusomea uhandisi basi nchi ingekuwa mbali sana kimaendeleo!!!! Matokeo yake tunaogopa makujumu magumu tunataka vya rahisi na matokeo yake ni kama yale ya akina Monyo jana Airport anatoa macho kama panya aliyekamatwa na mtego. Kwanza ukimwangalia tu na zile rasta na jinsi alivyokuwa anaonekana utajua kuwa ni victim wa madawa (punda na mtumiaji).
 
wakome kwani Mabosi wao si Tupo nao hapa hapa HAWATAJWI.

Ila mkuu inashangaza hivi kweli ina maana wakikamatwa hawataji majina ya wahusika wakuu? Kama kweli hawataji basi watakuwa wamefungwa ufahamu na mapepo. Hata siku moja sijawahi kusikia hawa punda wametaja mabosi wao. Halafu eti tunajidai tunapiga vita madawa huku makada wakuu wa madawa hawatajwi!!! Haya tusubiri ya Makyembe.
 
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.

Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.

Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.

6366947_orig.jpg


8940017_orig.jpg


8668822_orig.jpg
Yaani spare inaoka Tz kwenda Hon kong, wakati ndio traffic center, hata mimi ningelihisi kuna kitu.
 
Kuonyesha aliyetuma ana akili ndogo, kafikiria kua akituma hii kitu ikiwa ndani ya hiyo metal gear basi hatoshtukiwa, ati ataonekana tu anapeleka hii bidhaa labda kufanyia kitu flani, sawa haitokuwa detected kwenye machine kwa sababu ya hiyo metal cover, ila sasa tuje kwenye ukweli, unajua HK wanavyowasuspect watanzania, hata kama ni wewe compare Hong Kong na Bongo, unadhani Hong Kong hakuna metal gear kama hizo ambazo unaweza ukapata tena kwa bei nafuu zaidi na quality kubwa zaidi? ni mjinga ndiye atakayenunua bongo afu aisaifirishe ikafanye kazi Hong Kong maana kuna gharama za ndege kuisaifirisha pia.. Hahahaha! muuza madawa naye stupid hivi, bongo bna
 
wayaangalie kwa ukaribu makampuni ya kusafirisha mizigo ni eneo lao kuu la kusafirishia
 
Mazoea hujenga tabia, sasa kama watu walichakachua mafuta hadi kwenye gari ya "mkulu wa kaya" wewe unadhani watashindwa kuchakachua hivyo vimitambo vya hapo uwanja wa ndege na kupitisha dozi kamlili, mimi nachosubili kwa sasa aje kukamatwa mtu mkubwa mmoja au mtoto mmoja wa kigogo nadhani atakuwa "sample space" nzuri ya kufanyia case study.
 
Hizo mbona ni gear mbili tofauti? Au ni za matukio tofauti? Isije ikawa mambo mengine mipakazo tu. Na je, hao wanaokamatwa ni watanzania kweli?
Mwakyembe chunguza hili sakata vizuri tafadhali.
Soma vizuri post,gear ya kwanza ilishikwa na kuwa examined august 2 na ya pili imeshikwa jana august 15.
Hakuna kusingiziwa hapo na ndio maana wakubwa wako kimya otherwise ungewasikia wanakanusha.Wameshikwa pabaya na dawa pekee waionayo nikukausha kimyaaaaaaaaaaa...
 
Tukiamua kuacha kuwapa platform matajiri wanaofumuka kama uyoga bila shughuli za kueleweka tutakuwa tuna nia ya kweli ya kumaliza tatizo.
 
Hii ni hatari sana, hii nchi imeoza kwenye swala la usalama. Nachofahamu pale airport kuna usalama wa taifa...
 
Hiyo ni biashara ya JK mwenyewe ndio maana yuko kimya!!!!!!!
 
Kuonyesha aliyetuma ana akili ndogo, kafikiria kua akituma hii kitu ikiwa ndani ya hiyo metal gear basi hatoshtukiwa, ati ataonekana tu anapeleka hii bidhaa labda kufanyia kitu flani, sawa haitokuwa detected kwenye machine kwa sababu ya hiyo metal cover, ila sasa tuje kwenye ukweli, unajua HK wanavyowasuspect watanzania, hata kama ni wewe compare Hong Kong na Bongo, unadhani Hong Kong hakuna metal gear kama hizo ambazo unaweza ukapata tena kwa bei nafuu zaidi na quality kubwa zaidi? ni mjinga ndiye atakayenunua bongo afu aisaifirishe ikafanye kazi Hong Kong maana kuna gharama za ndege kuisaifirisha pia.. Hahahaha! muuza madawa naye stupid hivi, bongo bna

Pengine sio mara ya kwaza kutumia hii mbinu ...
 
Hivi hawa punda hawakomi kujitoa kafara,,,wangekuwa wanajitoa kafara kudai mikataba halari ya madini,,,ufisadi,,epa,,richmond,,haki za raia wa tanzania,,tanzania tungekuwa mbali sana,,,lakini wanataka watajirike wenyewe tu
 
Back
Top Bottom