Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa kimeshafanya mazungumzo na vyama vingine vya upinzani kwa lengo la kuungana na kuikabili Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi ujao.
Kauli hiyo imetolewa Februari 9, 2025, na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, alipokuwa kwenye mkutano katika Jimbo la Kibiti, wakati akiendelea na ziara yake ya siku tatu katika majimbo matatu ya Mkoa wa Kichama wa Mwambao.
Soma: Ado Shaibu: ACT Wazalendo, CHADEMA na vyama vingine makini vya upinzani tuungane kuing'oa CCM madarakani
Ado Shaibu amesema tayari ACT Wazalendo kimezungumza na vyama vyenye nguvu vya upinzani, vikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR- Mageuzi
Amesema vyama hivyo vina historia ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ambao walidai ulikumbwa na dhuluma.