Uchaguzi 2020 ACT-Wazalendo wajieleza kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kwanini Maalim Seif (ACT) alimuombea kura Tundu Lissu (CHADEMA)

Uchaguzi 2020 ACT-Wazalendo wajieleza kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kwanini Maalim Seif (ACT) alimuombea kura Tundu Lissu (CHADEMA)

Mwenye kumbukumbu ya barua ya onyo kwa ccm kutoka Tume ya uchaguzi, au ofisi ya msajili ningependa nione tafadhari wanajanvi. Au mwenye clip au voice, ya Tume ya uchaguzi or ofisi ya msajili tafadhari. (Ndani ya miaka 10 iliyopita)
 
Chama cha ACT Wazarendo leo kimetoa majibu kufuatia barua ya msajiri wa vyama vya siasa nchini kukituhumu kuvunja sheria ya vyama vya siasa kifungu 11a,ambapo mgombea urais wa Zanzibarkupitia chama hicho mhe,Sharif Hammad alimuombea kura mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshiwa Tundu Atipas Lisu.

Ikumbukwe kuwa kufuatia mafanikio ya vyama vya siasa mwaka 2015,Sheria ya vyama vya siasa ilifanyiwa marekebisho ili kuzuia muunganiko wa ghafra wa vyama vya siasa na kuweka mashariti magumu ili kuzuia ukawa nyingine. Baada ya kusoma barua ya ACT nimeona kuna tundu kwenye sheria linaweza kutumiwa na vyama vya upinzani kufikia adhima yao.
 

Attachments

  • ACT Letter 1.jpg
    ACT Letter 1.jpg
    147 KB · Views: 1
  • ACT Letter.jpg
    ACT Letter.jpg
    122.8 KB · Views: 1
Ile kauli alitoa Sefu kama Sefu kuwa anaimani Raisi wa Jamhuri atakuwa Lissu, hayo ni maoni binafsi kama maoni ya Mrema na Cheyo kuwa Magufuli atashinda Urais wa Tanzania.

Hata hivyo ACT hawajaungana na Chadema ila wanaimani Chadema itashinda Uchaguzi Mkuu kama ambavyo Chadema wanaimani ACT watashinda Zanzibar 2020...

Hata hivyo ACT Wamenifurahisha na huu mstari, Mwandishi wa hii barua akili kubwa Sana.[emoji116]

"Hata hivyo ACT kinaamini Raisi Magufuli hatakuwa Rais baada ya uchaguzi wa October 28 2020."

Hapa ACT wameamua kumkera msajili wa vyama vya siasa.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
 
Ile kauli alitoa Sefu kama Sefu kuwa anaimani Raisi wa Jamhuri atakuwa Lissu, hayo ni maoni binafsi kama maoni ya Mrema na Cheyo kuwa Magufuli atashinda Urais wa Tanzania.

Hata hivyo ACT hawajaungana na Chadema ila wanaimani Chadema itashinda Uchaguzi Mkuu kama ambavyo Chadema wanaimani ACT watashinda Zanzibar 2020...

Ina maana nchi hii wenye haki kuungwa mkono ni CCM tu vyama vingine havina hiyo haki nini maana ya demokrasia Sasa.
Yaani huyu msajili hadi anatia aibu
 
Walichoandika sio utetezi ni kukubali kosa na kuongeza kosa lingine .Kura ndio huamua nani atashinda !! Sio imani!!! Eti tunaamini Lisu atashinda!! Sababu ya umati unaojaa mikutano yake ya kampeni!! Aisee !!!!!!

Jamani hizi ofisi za vyama havina watu makini

Yaani barua wanaandika kwa msajili ya kumnadi Lisu serious? Mgombea wao Membe waliyemchagua wenyewe kupitia vikao halali vya chama wamempeleka wapi kwa kikao kipi ? kama wamemuondoa ugombea na Ku mu replace na Lisu kikao gani cha vyama cha kikatiba kiliamua hayo?

Msajili hiyo barua ni ushahidi tosha hata clip ukiitupa jalalani haina shida hiyo barua ni official letter Ku confirm kuwa wao wana mnadi Lisu bila idhini ya kamati kuu ,mkutano mkuu wao wala taarifa ya kumuengua Membe kutoka Tume ya uchaguzi

Hiyo barua ni ushahidi tosha wa jinsi Act inavyoendeshwa kienyeji
Maelezo hayo yanatakiwa tu kufanyiwa uamuzi wamekiri na ni kama wanasema come what may!!

Uandishi huo wa barua ni uswahilini hasa
Mtapata taabu sana. Sasa hapo ndio umeandika nini?
 
Back
Top Bottom