ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

ACT Wazalendo wataka Zanzibar ipewe mamlaka kamili

Duniani kote vyama huungana na kuwa na itikadi moja na kuunda Serikali, Kama sio swala la Tumbo maana yake ACT inakubaliana na Sera za CCM ndio maana wakaungana, tafuati na hapo wadanganyeni wajinga
ACT Wazalendo , wanazungumzia matakwa ya wazanzibari. Hi kauli mbiu ya Mamlaka kamili ilisha watilisha wengi ndani kwa kuonekana wanahatarisha Muungano.
Lakini ujuwe kuwa Chama cha siasa kina Maono yake na Mtazamo wake wa jinsi ya kuendesha nchi na siasa.
Huu Muungano usiokuwa na DIRA ni wa CCM si wa Chadema wala ACT.
Hata Mfumo wa Uendeshaji nchi wa mikoa ni wa CCM , chadema wao ni Majimbo. na Serikali 3
CCM sera yao ya msingi ni serikali 2 kuelekea 1. LakiniCCM Zanzibar hawaitaki hiyo. hapo ndio utaona kuwa kuna KIJAMBO kimejificha chini ya MUUNGANO.
ndio maana wenye maono tofauti wanataka shirikisho ambalo linaweza likaziunganisha nchi nyingine nyingi tuu.
 
Dawa ni kuvunjwa ama serikali 3 kuendelea na muundo wa serikali 2 huku Zanzibar umeishaikamilishia kwa kuwapa mamlaka kamili (yaani yote) ni kuendelea unyonyaji kwa Tanganyika
Hivi suala la serkali moja kwanini wengi hawalipigii chapuo! Kwangu naona zanzibar iwe tu mikoa. Serkali moja. Bunge 1. Mahakama 1.
Haiwezekan tumeshafikia maono ya Africa Mashariki kuelekea sarafu 1.
Africa 1.
Alafu bado Tanzania tunajikata vipandepande
 
Wanatafuta uhuru wakati uhuru wanao ila hawajui kama wanao
Nimekuelewa. Ila sasa sjui nisemeje domo linawasha ila hofu imetawala. Izi hofu za kijinga sana watanzania wengi tunatawaliwa na hofu, em ngoja nikae kimya tu.
 
Ukweli ni kwamba viongozi wa juu wa smz ndio wanao upigania muungano hata ikibidi kuua ndugu zao,ndio huomba msaada wa kijeshi pia ndio waliomtumia jecha kuvuruga uchaguzi,wanufaika wakuu wa huu muungano wa mchongo ni tabaka tawala la smz.
Ebu acha vituko , Karume aliposema koti la muungano linambana , unafikiri nani alikuwa na uwezo wa kumuua? Mastermind hapa ni Tanzania bara ndio maana walikuwa tayari kuua nchi yao ya Tanganyika kwa ajili ya muungano
 
Huo ndio ukweli,zenji ipewe mamlaka kamili iondoke zake ijitegemee inanyonywa sana na tanganyika kupitia koti la muungano.
CCM wameufanya huu Muungano kama ndoa ya kikatoliki (kikiristo )mke mmoja, hakuana kuachana.
sasa kweli mfumo umezeeka mno, na wao wenyewe hawezi kuuhimili.
Leo Raisi Mzanzibari Kashika Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Tanganyika Imo ndani,
Watanganyika hawaridhiki ,lakini wanagugumia kichichini.
Wengi wanaona kuwa mambo yanakwenda sivyo kabisa.
Kama Vile Wanaona Zanzibar Inapendelewa sanaa, Kule Zenji wanatawala wenyewe pekeyao,
Kisha huku bara wanachangia na wenzao, ilhali wao wako wengi kuliko zenji.
HII SHIDA KWELI
FUNGUKENI ILI MUELEZE MACHUNGU MUNAYOKABILIANA NAYO
MFUMO HUU SI MWEMA KATU
 
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Masoud Othman amesema Chama chake cha ACT Wazalendo kinataka Muungano utakaoitambua Zanzibar yenye Mamlaka kamili

Masoud amesema hayo kwenye mkutano wa Chama chake huko Nungwi

Chanzo: ITV habari
Hakuna kitu kama hicho. Hata Mungu ilimbidi amtume Malaika Gabrieli kwenda Nazareti kumpa habari njema Maria. Hata Yesu mwenyewe ilibidi azaliwe kwenye zizi la ng'ombe la Kisukuma kwa vile hoteli zilikuwa zimejaa shauri ya sensa.

Dunia ipo nyani na kuku, kuna inzi na mbwa, kila mmoja ana madaraka kamili hapo alipo la sivyo ukijipanua sana humgusa mwenziye madaraka hupingua. Mwambieni OMO kuwa serkali ilokuwa 1963 na madaraka kamili ni ya Muhamed Shamte, na mamlaka kamili tangu Mombasa gadi Sofala vikiwamo visiwa vya Mafia na Kilwa Kivinje na Songo Songo kwenye mafuta. Cha kwanza alichofanya Shamte ni kusainiana na Jomo Kenyatta pwani yote ya Kenya akaiachia, yaani madaraka kamili yakakoma. Pwani ya Tanganyika aliiachia
1887 zama za Sultani Barghash mwenyewe kwa Gavana wa Tanganyika Major Georg Kurt Wissman. Hii yote maelezo ya maana ya maneno "mamlaka kamili", hakuna kitu kama hiyo, haiwezekani ikawa open-ended.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Wakuu ukifuatilia kwa makini sera za ACT Wazalendo, pamoja na misimamo ya viongozi wao juu ya mamlaka ya Zanzibar, utakubaliana na mimi kwamba hawa jamaa ni lile kundi la Uamsho lilijificha nyuma ya chama cha siasa kinachojiita ACT Wazalendo.

Ukienda katika mikutano yao haswa ile inayofanyika huko Zanzibar, kitu cha kwanza utasikia wanazungumzia habari za mamlaka kamili ya Zanzibar pekee bila kuzungumzia na mamlaka ya Tanganyika.

Je, hicho chama kimeundwa kwa ajili ya wazanzibar peke yao au kwa ajili ya watanzania wote?

Kama jibu ni kwa ajili ya watanzania kwanini chama kijikite katika kuipigania Zanzibar pekee na sio Tanzania yote au Tanganyika na yenyewe ipewe hadhi yake?

Je kwanini Zito na katibu mkuu wake na wao wasiipiganie Tanganyika yao kama wenzao waipiganiavyo Zanzibar yao?

Yani Zito na elimu yake yote amekubali kuwekwa mfukoni na kina sheikh Makame kwa sababu ya vijipesa vidogo wanavyompa?

Msajili hebu kiangalie vizuri hiki chama, huenda ni kundi lile la Uamsho lililokuja kwa njia nyingine kupitia huu upinzani uchwara wa Zito na genge lake.

Hatuwezi kuiweka nchi yetu hatarini kwa sababu ya njaa za wanasiasa uchwara wachache wa ACT Wazalendo.
 
Kwani lazima wapinzani wote wafanane mawazo?

Hamuwezi kufanya siasa bila kushambulia wengine?

Au upinzani ni Chadema peke yake?

Wengine lazima wapigwe vita?
 
Logic ndogo anae ukumbatia muungano ndio mnufaika mkubwa, sasa Tanzania bara na Zanzibar nani yuko tayari kuua watu kuulinda? jibu ni rahisi Tanzania bara, ndio maana hata Rais wa Zanzibar mnachagua kutoka Dodoma ili mfanye mtakavyo kuulinda muungano
Tanzania bara inanufaika nini na Muungano ?
 
Wao wanasema Mapato hayakui sababu ya muungano. Mfano wao wanataka benki za Zanzibar ziwe kama za visiwa vya Jersey, Curacao, Seychelles ambako Kuna sheria rafiki za Kodi Ili wanaotunza mabilioni wakayafiche huko!!

Sasa wanasema wanashindwa kuweka sheria hizo rafiki sababu masuala ya fedha na kodi ni ya muungano!!

Wanasema pia Mapato hayakui sababu muungano hauja factor in kuwa Zanzibar ni service-sector based economy. Kwa hiyo ilibidi flexibility kwenye sheria za Kodi, fedha, uwekezaji n.k Ili yaendane na nature ya Zanzibar ambayo Haina rasilimali kma za bara.

So kwa hoja hizo according to Jussa Ladhu ni kwamba kwa mamlaka huru wataweza fikia hizo targets kuliko kwa Sasa ambako ni kama wilaya tu hivi ya Tanganyika.

Kuhusu ukubwa wa nchi mbona Nauru au Gambia Ina kura Moja UN sawa sawa tu na ma-nchi makubwa kama India!! So ukubwa inaweza isiwe challenge kama muundo uko well defined.
Mfano wako wa Gambia hauendani na wa Zanzibar kwa sababu Gambia ni nchi kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Sasa Zanzibar haiwezi kuwa na mamlaka kamili kinchi kama zilivyo nchi zingine huru halafu kuwe na Muungano.

Labda kama wanataka turudi kwenye communities tu kama SADC au EAC lakini tukifikia hatua hiyo hatutakuwa na Muungano ni obvious
 
Back
Top Bottom