Adha kubwa tuipatayo abiria tunaosafiri na mabasi ya mikoani

Adha kubwa tuipatayo abiria tunaosafiri na mabasi ya mikoani

Hii mada mnaifanya breaking tatizo hamfanyii uhariri kutoka facebook mlikoitoa, member jf mnaniangusha asee..!!
 
kama ni lazima kula safarini. andaeni maandazi tu hapo nyumbani. unapiga na soda yako, safari inakuwa poa kabisa
 
Tengeneza chakula chako nyumbani, kifunge vizuri, utakula popote, muda wowote.

Mimi huwa nafunga ugalo wa LOYE
Mkuu kuna mhusika mmoja kwenye sinema fulani ya Ki-niger akiitwa Usopia, unamfahamu?
Sinema inaitwa (Usopia in London)

Kila nikiona michango yako humu nalinganisha na akili za huyu bwana.
 
Kupunguza Gharama ya chakula sidhani kama Inawezekana kwa siku za karibuni, Unanunua chakula unapewa risiti ya EFD, hii maana yake ni kwamba Kadri gharama inavyozidi kuwa kubwa ndo jinsi serikali inazidi kuongeza mapato na eneo husika kubaki na pesa kwa ajili ya operation ya eneo husika

Cha kufanya tuwakache tu, pika chako nyumbani beba ukifika sehemu ya kula nenda ukale chakula chako sehemu yao, kama hawataki kula tu kwenye gari, kwa magari yanayokataza kula ndani ya gari abiria shuka tu ukale
Hakuna namna aisee
 
Vyakula bei sana nyama zenyewe zinabanikwa alafu hazijaiva na ni makambakamba tu.
 
Solution ni kuandaa chakula chako tu, Mimi husafiri Mara nyingi Ila ukipita pa msosi vyakula huwa vibaya, nyama haziivi vizuri na zimekaa mda mrefu. So Mimi hukaanga zangu kuku wangu staki shida
 
Je, ni kwa kiasi gani hili ni tatizo kubwa?

"Serikali yetu hebu tusaidie wanyonge na hii tabia inazidi shamiri sana kwa wale ndg zetu wanao safiri mikoa ya mbali.
1. Dar to Mwanza, Dar to Mbeya,Dar to Kigoma, Dar to Arusha.
Kuna tabia na utaratibu wa mabasi walio jiwekea bila kuhofia abiria wao na sio rafiki kabisa wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu bila kujali abiria wao mifukoni mwao kuko vp chakula cha kawaida sana unakuta elfu 7 hadi elfu 8 na kuendelea wakati hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei hiyo halafu nu kidogo sana hivi wanadhani kila mtu anapesa ya kumudu hiyo pesa?

Jana nilikuwa natoka Arusha kuja Dar tulipo fika sehemu ya chakula nilitamani kulia niliongozana na Mama mmoja mwenye watoto watatu alivyoambiwa chakula cha bei ya mwisho ni elfu 7 alikuwa mnyonge sana na alikuwa na elfu 5 tu ikambidi anunue soda na biskuti roho iliniuma sana.
Sasa ombi langu kwa serikali itoe sheria na mwongozo kwa mabasi yote yawe yana simama kwenye mji ulio na huduma kwa wote sio kutupeleka maeneo ambayo wana maslahi nayo inaumiza sana.

NB. Kwa tetesi nilizo sikia dereva akipeleka basi sehemu ya hotel hupata huduma ya chakula bure yeye na watumishi wote wa gari na posho wanapewa kwa week au mwezi, sasa iweje maslahi yao yatutese abiria?
*Tupaze sauti kwa viongozi Wabunge na viongozi wote wa juu kuwa hii ni 2021
C and P from Whatsapp Groups
Shida ni eneo la kutosha kupaki mabasi, huduma ya vyoo, maintenance na maeneo mazuri kwa chakula. Kikubwa kuwe na ushindani kwenye hayo maeneo ya kula, yaani mwenye motel kazi yake iwe ni kuwaacha vendors wauze kwa bei zao za ushindani kisha wanamlipa kwa kutumia eneo Lake. Hapo adabu, class, quality, customer care nk zitakuwepo maana mteja atakuwa huru kuchagua na wauza vyakula watakuwa na discipline
 
vyakula vya hovyo mpaka huwa najisikia kinyaa,ndugu zangu tafuteni hela muwe mnasafiri na magari yenu unakula popote unapotaka.
 
Iadara za Serikali zinazohusika na ukaguzi nazo nahisi huwa zinahongwa yani bei za vyakula haviendani kabisa na ubora.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] yaani kila nikiwaza rock hill moyo wangu unajawa na furaha balaa[emoji23] nyama jamani nyamaaaa. Nyamaaa. Halaf ukiwahi napema zinakuaga tamu balaa. Watu wakishajaa waii.
Rock hill ni sehemu poa sana pa kula nashangaa mtu analalamika 7000 kwa chakula nzuri na sehem nzuri Kama ile..mm sipandagi gari ambayo najua haitasimama rock hill
 
Rock hill ni sehemu poa sana pa kula nashangaa mtu analalamika 7000 kwa chakula nzuri na sehem nzuri Kama ile..mm sipandagi gari ambayo najua haitasimama rock hill
Nilipandaga wakaenda kutulishia Highway. Jaman nilimind[emoji23] nilikasirika manusura kupasuka. Ila nafanyaje sasa na distance ndo hiyo. Nilichukiaaaa. Yaan rock hill kila variety unapata. Mpk bustani ya bure na hakuna wa kukuhoji kwanini umekuja na chakula chako. Unatandika zako mkeka ama unakaa kwenye majanj na wanao mnakula mpk basi. Mimi safari ambayo hakuna kula siutaki. Na kama hotel.chafu sigusi kitu acha niwe teja wa biskuti
 
Nilipandaga wakaenda kutulishia Highway. Jaman nilimind[emoji23] nilikasirika manusura kupasuka. Ila nafanyaje sasa na distance ndo hiyo. Nilichukiaaaa. Yaan rock hill kila variety unapata. Mpk bustani ya bure na hakuna wa kukuhoji kwanini umekuja na chakula chako. Unatandika zako mkeka ama unakaa kwenye majanj na wanao mnakula mpk basi. Mimi safari ambayo hakuna kula siutaki. Na kama hotel.chafu sigusi kitu acha niwe teja wa biskuti
Mm sehem kwenye safari ya arusha-dar ni rock hill na kilimanjaro tu ndio nakula Ila sana sana napendelea rock hill nile ile nyama choma nikiweka na bia zangu 4 inakua burdani nafurahia safari yangu,na uzuri wa pale naona hata usiku hawafungi coz Kuna siku nikisafiri na private usiku nakulaga pale...mtu akilalamika bei afungashe vyakula vyake home asafiri nayo.
 
Ni sawa, hebu check pale Liverpool palivyo na mazingira yale then unataka uuziwe chips kuku buku 4 sio? Bora mpambane waanze at least kuwa wanauza chips kivyake kwa mtu anaetaka, waaache ile kulazimisha mtu anunue mpaka na kuku.

Kwanza sio lazima mkule njiani eboo. Panda full luxury unapata zako soda,maji na biscuit vitakusaidia kupunguza ukame wa njaa. Kale huko unapoelekea.

Kuna hii biscuit ya eet som more ukipiga ile na soda unashiba ndiii, kwanza hata kuimaliza ni ngumu unless uwe food monga. Ukishindwa beba maandazi kwako
Dea wee acha hiv Dar - Songea unaweza kushindia biskut na soda? Safari masaa zaidi ya 17 kweli? Japo huwa wanatoa soda na maji.
Chakula ni muhimu, but mie huwa sili nikiwa safarini.
 
Mm sehem kwenye safari ya arusha-dar ni rock hill na kilimanjaro tu ndio nakula Ila sana sana napendelea rock hill nile ile nyama choma nikiweka na bia zangu 4 inakua burdani nafurahia safari yangu,na uzuri wa pale naona hata usiku hawafungi coz Kuna siku nikisafiri na private usiku nakulaga pale...mtu akilalamika bei afungashe vyakula vyake home asafiri nayo.
Hawawezi kufunga kwakua misiba ni mingi sana sana. Pia kuna madereva wa malori. Huwa wanatoaga oda. Yaan nakumbuka last time msiba wa babu mpk nikasema jamani si ijirudie tena[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji24][emoji24][emoji24]yaan watu wanakula na kunywaa[emoji119][emoji119] utasema sendoff. Mkifika mnasema sisi ni wateja fulan ama wa usafiri fulani. Tulikua na coaster 10. Me sikuona kama ni msiba kwakweli. Jamaa abarikiwe sana aisee. Na lile shamba lake la migomba big up sana. Kama Dar ex press wqsingezinguana maybe tusingepata kitu kizuri hivi.
Naona nimeanza uchawi mapema sana. Pale kuna madereva kama hawana hela hata wa magari wanaacha bill wanakujaga kuclear.
 
Mleta topic akumbuke ni kua hili ni soko huria, serikali haifanyi biashara ila ni “regulator” kwa kutumia sheria taratibu na kanuni! Sasa la kuwapangia wenye magari mle wapi au hotel ziuzeje mnadhani ni rahisi?

Pia zile hotel zina varieties kutokana na purchasing power yako kama huwezi nyama choma ya 10,000 , nunua ndizi za kukaanga za mia tano na soda au kula matunda ya buku.

Kama vipi beba mahindi ya kuchemsha, michembe na miwa kama wasukuma.

Mikoa ya kaskazini tumezoea haya mambo hata wa iringa na mbeya tangu enzi tumezoea pale Aljaazera!

Hata baadhi ya ndege walikua wana tabia ya kuuza viburudidho vingine ila sio abiria wote wana afford!

Kuna baadhi ya mambo ni jukumu la serikali ila mengine sasa tuwe tunatafuta ufumbuzi kama wateja/walaji, othetwise serikali za Kiafrica zitakua na mambo meeengi sana ya kufanya!

Huu ni mtazamo wangu tu!
 
Back
Top Bottom