Adha kubwa tuipatayo abiria tunaosafiri na mabasi ya mikoani

Hii mada mnaifanya breaking tatizo hamfanyii uhariri kutoka facebook mlikoitoa, member jf mnaniangusha asee..!!
 
kama ni lazima kula safarini. andaeni maandazi tu hapo nyumbani. unapiga na soda yako, safari inakuwa poa kabisa
 
Tengeneza chakula chako nyumbani, kifunge vizuri, utakula popote, muda wowote.

Mimi huwa nafunga ugalo wa LOYE
Mkuu kuna mhusika mmoja kwenye sinema fulani ya Ki-niger akiitwa Usopia, unamfahamu?
Sinema inaitwa (Usopia in London)

Kila nikiona michango yako humu nalinganisha na akili za huyu bwana.
 
Kupunguza Gharama ya chakula sidhani kama Inawezekana kwa siku za karibuni, Unanunua chakula unapewa risiti ya EFD, hii maana yake ni kwamba Kadri gharama inavyozidi kuwa kubwa ndo jinsi serikali inazidi kuongeza mapato na eneo husika kubaki na pesa kwa ajili ya operation ya eneo husika

Cha kufanya tuwakache tu, pika chako nyumbani beba ukifika sehemu ya kula nenda ukale chakula chako sehemu yao, kama hawataki kula tu kwenye gari, kwa magari yanayokataza kula ndani ya gari abiria shuka tu ukale
Hakuna namna aisee
 
Vyakula bei sana nyama zenyewe zinabanikwa alafu hazijaiva na ni makambakamba tu.
 
Solution ni kuandaa chakula chako tu, Mimi husafiri Mara nyingi Ila ukipita pa msosi vyakula huwa vibaya, nyama haziivi vizuri na zimekaa mda mrefu. So Mimi hukaanga zangu kuku wangu staki shida
 
Shida ni eneo la kutosha kupaki mabasi, huduma ya vyoo, maintenance na maeneo mazuri kwa chakula. Kikubwa kuwe na ushindani kwenye hayo maeneo ya kula, yaani mwenye motel kazi yake iwe ni kuwaacha vendors wauze kwa bei zao za ushindani kisha wanamlipa kwa kutumia eneo Lake. Hapo adabu, class, quality, customer care nk zitakuwepo maana mteja atakuwa huru kuchagua na wauza vyakula watakuwa na discipline
 
Ndo mana abiria wengine wanapanda na misosi yao kutoka majumbani mwao
 
vyakula vya hovyo mpaka huwa najisikia kinyaa,ndugu zangu tafuteni hela muwe mnasafiri na magari yenu unakula popote unapotaka.
 
Iadara za Serikali zinazohusika na ukaguzi nazo nahisi huwa zinahongwa yani bei za vyakula haviendani kabisa na ubora.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] yaani kila nikiwaza rock hill moyo wangu unajawa na furaha balaa[emoji23] nyama jamani nyamaaaa. Nyamaaa. Halaf ukiwahi napema zinakuaga tamu balaa. Watu wakishajaa waii.
Rock hill ni sehemu poa sana pa kula nashangaa mtu analalamika 7000 kwa chakula nzuri na sehem nzuri Kama ile..mm sipandagi gari ambayo najua haitasimama rock hill
 
Rock hill ni sehemu poa sana pa kula nashangaa mtu analalamika 7000 kwa chakula nzuri na sehem nzuri Kama ile..mm sipandagi gari ambayo najua haitasimama rock hill
Nilipandaga wakaenda kutulishia Highway. Jaman nilimind[emoji23] nilikasirika manusura kupasuka. Ila nafanyaje sasa na distance ndo hiyo. Nilichukiaaaa. Yaan rock hill kila variety unapata. Mpk bustani ya bure na hakuna wa kukuhoji kwanini umekuja na chakula chako. Unatandika zako mkeka ama unakaa kwenye majanj na wanao mnakula mpk basi. Mimi safari ambayo hakuna kula siutaki. Na kama hotel.chafu sigusi kitu acha niwe teja wa biskuti
 
Mm sehem kwenye safari ya arusha-dar ni rock hill na kilimanjaro tu ndio nakula Ila sana sana napendelea rock hill nile ile nyama choma nikiweka na bia zangu 4 inakua burdani nafurahia safari yangu,na uzuri wa pale naona hata usiku hawafungi coz Kuna siku nikisafiri na private usiku nakulaga pale...mtu akilalamika bei afungashe vyakula vyake home asafiri nayo.
 
Dea wee acha hiv Dar - Songea unaweza kushindia biskut na soda? Safari masaa zaidi ya 17 kweli? Japo huwa wanatoa soda na maji.
Chakula ni muhimu, but mie huwa sili nikiwa safarini.
 
Hawawezi kufunga kwakua misiba ni mingi sana sana. Pia kuna madereva wa malori. Huwa wanatoaga oda. Yaan nakumbuka last time msiba wa babu mpk nikasema jamani si ijirudie tena[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji24][emoji24][emoji24]yaan watu wanakula na kunywaa[emoji119][emoji119] utasema sendoff. Mkifika mnasema sisi ni wateja fulan ama wa usafiri fulani. Tulikua na coaster 10. Me sikuona kama ni msiba kwakweli. Jamaa abarikiwe sana aisee. Na lile shamba lake la migomba big up sana. Kama Dar ex press wqsingezinguana maybe tusingepata kitu kizuri hivi.
Naona nimeanza uchawi mapema sana. Pale kuna madereva kama hawana hela hata wa magari wanaacha bill wanakujaga kuclear.
 
Mleta topic akumbuke ni kua hili ni soko huria, serikali haifanyi biashara ila ni “regulator” kwa kutumia sheria taratibu na kanuni! Sasa la kuwapangia wenye magari mle wapi au hotel ziuzeje mnadhani ni rahisi?

Pia zile hotel zina varieties kutokana na purchasing power yako kama huwezi nyama choma ya 10,000 , nunua ndizi za kukaanga za mia tano na soda au kula matunda ya buku.

Kama vipi beba mahindi ya kuchemsha, michembe na miwa kama wasukuma.

Mikoa ya kaskazini tumezoea haya mambo hata wa iringa na mbeya tangu enzi tumezoea pale Aljaazera!

Hata baadhi ya ndege walikua wana tabia ya kuuza viburudidho vingine ila sio abiria wote wana afford!

Kuna baadhi ya mambo ni jukumu la serikali ila mengine sasa tuwe tunatafuta ufumbuzi kama wateja/walaji, othetwise serikali za Kiafrica zitakua na mambo meeengi sana ya kufanya!

Huu ni mtazamo wangu tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…