adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 17,595
- 39,893
Moja kwa moja ..
Mwezi wa saba mwaka huu nilichukua umamuzi wa kuondoka Jf kwa muda , malengo ya kuondoka ni mwendelezo wa utamaduni wangu wa mara kwa mara ikifika kipindi fulani nakuwa nje kabisa na mitandao ya kijamii kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kurudi tena .
Vitu ambavyo nakuwa navifanya kipindi hiko ;
1. Kukithirisha usomaji wa vitabu (soft copy & hardcopy . Usomaji wa vitabu imekuwa starehe yangu kubwa na kiliwazo tokea primary mpaka sasa na huwa napenda kusoma vitabu vya Historia , Afya , Dini , Teknolojia , Lugha na Saikolojia .
2. Kusafiri na Matembezi mbalimbali kama vile ;
a) Sehemu mbalimbali za asili na zenye mazingira mazuri ya kuvutia , mfano mzuri hapo chini 👇
b) Sehemu nilizokulia utotoni , nilizosoma na kutembelea majirani na marafiki wa utotoni .
Napenda sana kukumbuka nilipotoka , na nasikia furaha na napata hisia nzuri nikiJiConnect na kumbukumbu nzuri za utotoni na zamani .
Nilitembelea shule yangu ya msingi ya utotoni 👇
Nikatembelea Msikitini wa kwanza kuswali nikiwa hata sijaanza shule.
Nikakumbuka chanzo cha kuswali rafiki yangu aliniambia saa 7 mchana kutakuwa na tamthilia ya "jumba la dhahabu" enzi hizo inatamba sana . Mimi nikaenda kumuuliza Mama kama saa 7 tayari muda huo yupo na wageni yeye akasema "Mwanangu kumbe unaakili unataka kwenda kuswali ? mimi kuona soo nikasema ndio ilipofika saa 7 akamuambia Kaka yangu anipeleke msikitini na anifundishe kuswali basi tokea hapo swala na Mimi mpaka Leo Alhamdulillah.
Nikatembelea sehemu ambazo nilikuwa tunacheza mpira na ligi mbalimbali Kiwalani , nikakumbuka matukio mengi sana
Nikasikitika kukuta huu uwanja (chini👇)maarufu wa " Kigorofani" ambao ulikuwa maarufu kwa ligi za kuku na Mchele , timu za mitaa mbalimbali tukishindana na ugomvi nje nje sasa umegeuka shamba wakati muda wote ulikuwa vumbi watu wakicheza boli.
Nikahitimisha kusalimia majirani na marafiki wengi . Nilikaribishwa kiFalme sana ilikuwa furaha sana kuja kuwaona baada ya miaka mingi . Nikapiga stori na kubadilishana mawazo na machizi wangu wa utotoni .
Matembezi yalikuwa marefu pia nilitembelea sehemu nyingine kama vile Upanga , Kisutu sababu nina Historia napo na nikafika mpka Kijijini kusalimia ndugu.
3. Mazoezi mbalimbali na meditation ; nikarudisha utaratibu wangu wa kufanya mazoezi mbalimbali na kuMeditate kitu ambacho nakipenda sana sababu Kuna faida kubwa kiAfya na kiakili unakuwa unaitoa kama unaitoa nje 'negative energy ' na najikuta stable and flexible ki miwili na kiakili
Vipindi ambavyo napunguza distraction nakuwa bize na Meditation.
1. Ninapokaribia kutimiza umri mpya , mfano kesho October 4 ndio siku yangu ya kuzaliwa kabla ya kufikia ndio maana kabla ya kufikia miezi ya karibuni nilitoka Jf na sehemu nyingine kwa muda ili nifocus zaidi na kujitathimi safari yangu ya maisha , yale niliyofanya nyuma , malengo yangu yaliyopita na kuweka malengo mapya .
Mimi mwaka wangu mpya unaanza tarehe ninayo zaliwa kabla ya kufika nakuwa tayari nishafanya tathimini na kuweka mipango na malengo mapya pamoja na maboresho mbalimbali.
2. Ninapoingia phase mpya ya maisha mfano , kutoka primary kwenda secondary, secondary to advance, advance to University nk , hata nikitaka 'kuoa' nitatulizana sana .
Hii kumbukumbu kipindi cha nyuma baada ya kumaliza form six , nilikataa kujiunga jeshi nikaenda Library shuleni nikachukua vitabu mbalimbali vya afya , technology, history na majarida ya New York times, Times week nk . Nikaenda pia maktaba ya dini nikachukua vitabu mbalimbali .
Mwisho nikachukua simu yangu nikaenda kariakoo nikaiuza ili nibaki free nikisoma ,kuandika mafunzo na facts mbalimbali pamoja .
Hili (pichani) lilikiwa ghetto langu hapo sehemu ya kusomea , nilikuwa nasoma zaidi ya mwanafunzi mwenye hofu na Necta kumbe ilikuwa kwa ajili ya maarifa mbalimbali tu .
NB : hapo nilipoficha nimeficha notebook 📓 📒 zangu ambazo ni maarufu sana naogopa nilizosoma nao wakiona watanijua utambulisho wangu halisi.
Sasa nimerudi rasmi , niliiMiss sana Jf pamoja na marafiki zangu jukwaani . Ningependa kuwastua .
1. Mighty brothers Kaka zangu wa nguvu jukwaani Selikavu Razorblade Kaka aliyetupotea Intelligent businessman
Ujumbe : Gunman nimerudi kutoka Joseon 😂
2. Dadaz wa nguvu ;
Dada yangu kipenzi Shadeeya , Mimi nasema Yanga bingwa
Bestie wangu wa nguvu Joanah , pole sana nilipigiwa simu na Kaka Mr Kiwembe alinieleza hali yako , nilistuka sana ,pole sana nilikuombea na nitazidi kukuombea
Mwanangu sana Seran ; pamoja sana
3. Ghayos Gang ; wanangu wa Maghayo Family Babu loose Nut , muhuni Maghayo The Mongolian Savage , Usutaz Busu la Kenge na pacha mpya Adryz pamoja na mkuu wa majeshi Gengis Khan wa Jf
Ujumbe : Hata mnikatae vipi Mimi ni Gayo family ghayos Gang ni chama langu
4. Moderators
Cookie Payge and others
Ujumbe : nawakubali sana kongole kwa kazi nzuri hapa Jf
Wengineo
secretarybird Ayatollah wa Jf from Tehran ya Ikwiriri
Kaka Red black , shukran kwa kujali
Kaka Ertugrul Bey gul bay
Lamomy ; Sniper nimerudi mjengoni nimerudi
Mufti kuku The Infinity
Kaka GENTAMYCINE Mazimpaka , nakutakia kheri huko ulipo
#Nimerudi kama Gunman aliyerudi Joseon kutokea Japan