'Adriz the Goat ' nimerejea rasmi JF baada ya safari yangu meditation

'Adriz the Goat ' nimerejea rasmi JF baada ya safari yangu meditation

Umejiandaaje na El Ninyo?

IMG-20260913-WA0064(1).jpg
 
Kwenye jambo Serikali ya JPM ilifanya la maana ni Ujenzi wa hizo barabara kwa kiwango Cha Lami

Nimepita juzi kidogo nipotee, bahati nilipata assistance ya Google

Jamaa ako loose Nut ametekwa na mzigo wa Vale Nafaka

Kila siku yupo busy kuupost 🤪
 
Kwenye jambo Serikali ya JPM ilifanya la maana ni Ujenzi wa hizo barabara kwa kiwango Cha Lami

Nimepita juzi kidogo nipotee, bahati nilipata assistance ya Google

Jamaa ako loose Nut ametekwa na mzigo wa Vale Nafaka

Kila siku yupo busy kuupost 🤪
Me Vale mashaka nimemjulia kwa thread za loose nut 😃😃

Juzi ndo nikakuta amepostiwa BBC
 
Me Vale mashaka nimemjulia kwa thread za loose nut 😃😃

Juzi ndo nikakuta amepostiwa BBC
Ningekuwa sijazeeka sana, ningemwoa awe mke wangu wa 4 ili kumkomesha loose Nut

Yeye kila siku anampost wakati hata kumwalika Dinner hajawahi 🤪

Saivi Vale amekuwa matawi, bila mpunga wa 1 to 2m huwezi kumng'oa
 
Moja kwa moja ..

Mwezi wa saba mwaka huu nilichukua umamuzi wa kuondoka Jf kwa muda , malengo ya kuondoka ni mwendelezo wa utamaduni wangu wa mara kwa mara ikifika kipindi fulani nakuwa nje kabisa na mitandao ya kijamii kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kurudi tena .

Vitu ambavyo nakuwa navifanya kipindi hiko ;

1. Kukithirisha usomaji wa vitabu (soft copy & hardcopy . Usomaji wa vitabu imekuwa starehe yangu kubwa na kiliwazo tokea primary mpaka sasa na huwa napenda kusoma vitabu vya Historia , Afya , Dini , Teknolojia , Lugha na Saikolojia .

2. Kusafiri na Matembezi mbalimbali kama vile ;

a) Sehemu mbalimbali za asili na zenye mazingira mazuri ya kuvutia , mfano mzuri hapo chini 👇
View attachment 3682959


b) Sehemu nilizokulia utotoni , nilizosoma na kutembelea majirani na marafiki wa utotoni .

Napenda sana kukumbuka nilipotoka , na nasikia furaha na napata hisia nzuri nikiJiConnect na kumbukumbu nzuri za utotoni na zamani .

Nilitembelea shule yangu ya msingi ya utotoni 👇
View attachment 3682956

Nikatembelea Msikitini wa kwanza kuswali nikiwa hata sijaanza shule.

Nikakumbuka chanzo cha kuswali rafiki yangu aliniambia saa 7 mchana kutakuwa na tamthilia ya "jumba la dhahabu" enzi hizo inatamba sana . Mimi nikaenda kumuuliza Mama kama saa 7 tayari muda huo yupo na wageni yeye akasema "Mwanangu kumbe unaakili unataka kwenda kuswali ? mimi kuona soo nikasema ndio ilipofika saa 7 akamuambia Kaka yangu anipeleke msikitini na anifundishe kuswali basi tokea hapo swala na Mimi mpaka Leo Alhamdulillah.

View attachment 3682892


View attachment 3682894

Nikatembelea sehemu ambazo nilikuwa tunacheza mpira na ligi mbalimbali Kiwalani , nikakumbuka matukio mengi sanaView attachment 3682898

Nikasikitika kukuta huu uwanja (chini👇)maarufu wa " Kigorofani" ambao ulikuwa maarufu kwa ligi za kuku na Mchele , timu za mitaa mbalimbali tukishindana na ugomvi nje nje sasa umegeuka shamba wakati muda wote ulikuwa vumbi watu wakicheza boli.
View attachment 3682901

Nikahitimisha kusalimia majirani na marafiki wengi . Nilikaribishwa kiFalme sana ilikuwa furaha sana kuja kuwaona baada ya miaka mingi . Nikapiga stori na kubadilishana mawazo na machizi wangu wa utotoni .

Matembezi yalikuwa marefu pia nilitembelea sehemu nyingine kama vile Upanga , Kisutu sababu nina Historia napo na nikafika mpka Kijijini kusalimia ndugu.

3. Mazoezi mbalimbali na meditation ; nikarudisha utaratibu wangu wa kufanya mazoezi mbalimbali na kuMeditate kitu ambacho nakipenda sana sababu Kuna faida kubwa kiAfya na kiakili unakuwa unaitoa kama unaitoa nje 'negative energy ' na najikuta stable and flexible ki miwili na kiakiliView attachment 3682914

Vipindi ambavyo napunguza distraction nakuwa bize na Meditation.

1. Ninapokaribia kutimiza umri mpya , mfano kesho October 4 ndio siku yangu ya kuzaliwa kabla ya kufikia ndio maana kabla ya kufikia miezi ya karibuni nilitoka Jf na sehemu nyingine kwa muda ili nifocus zaidi na kujitathimi safari yangu ya maisha , yale niliyofanya nyuma , malengo yangu yaliyopita na kuweka malengo mapya .

Mimi mwaka wangu mpya unaanza tarehe ninayo zaliwa kabla ya kufika nakuwa tayari nishafanya tathimini na kuweka mipango na malengo mapya pamoja na maboresho mbalimbali.

2. Ninapoingia phase mpya ya maisha mfano , kutoka primary kwenda secondary, secondary to advance, advance to University nk , hata nikitaka 'kuoa' nitatulizana sana .

Hii kumbukumbu kipindi cha nyuma baada ya kumaliza form six , nilikataa kujiunga jeshi nikaenda Library shuleni nikachukua vitabu mbalimbali vya afya , technology, history na majarida ya New York times, Times week nk . Nikaenda pia maktaba ya dini nikachukua vitabu mbalimbali .

Mwisho nikachukua simu yangu nikaenda kariakoo nikaiuza ili nibaki free nikisoma ,kuandika mafunzo na facts mbalimbali pamoja .

Hili (pichani) lilikiwa ghetto langu hapo sehemu ya kusomea , nilikuwa nasoma zaidi ya mwanafunzi mwenye hofu na Necta kumbe ilikuwa kwa ajili ya maarifa mbalimbali tu .

NB : hapo nilipoficha nimeficha notebook 📓 📒 zangu ambazo ni maarufu sana naogopa nilizosoma nao wakiona watanijua utambulisho wangu halisi.

View attachment 3682933

Sasa nimerudi rasmi , niliiMiss sana Jf pamoja na marafiki zangu jukwaani . Ningependa kuwastua .

1. Mighty brothers Kaka zangu wa nguvu jukwaani Selikavu Razorblade Kaka aliyetupotea Intelligent businessman

Ujumbe : Gunman nimerudi kutoka Joseon 😂

2. Dadaz wa nguvu ;

Dada yangu kipenzi Shadeeya , Mimi nasema Yanga bingwa

Bestie wangu wa nguvu Joanah , pole sana nilipigiwa simu na Kaka Mr Kiwembe alinieleza hali yako , nilistuka sana ,pole sana nilikuombea na nitazidi kukuombea

Mwanangu sana Seran ; pamoja sana

3. Ghayos Gang ; wanangu wa Maghayo Family Babu loose Nut , muhuni Maghayo The Mongolian Savage , Usutaz Busu la Kenge na pacha mpya Adryz pamoja na mkuu wa majeshi Gengis Khan wa Jf

Ujumbe : Hata mnikatae vipi Mimi ni Gayo family ghayos Gang ni chama langu

4. Moderators
Cookie Payge and others

Ujumbe : nawakubali sana kongole kwa kazi nzuri hapa Jf

Wengineo

secretarybird Ayatollah wa Jf from Tehran ya Ikwiriri

Kaka Red black , shukran kwa kujali

Kaka Ertugrul Bey gul bay

Lamomy ; Sniper nimerudi mjengoni nimerudi

Mufti kuku The Infinity

Kaka GENTAMYCINE Mazimpaka , nakutakia kheri huko ulipo
Dogo una mkwara mbuzi.

Mbusii wewee
 
Oya adriz halafu hayo maeneo nimeishi sana.

Pande za Malawi na Yombo relini nimechili sana miaka fulani.

Nimefanya sana mazoezi hapo shule uwanjani.
 
Dogo una mkwara mbuzi.

Mbusii wewee
Nafurahi kuwa na Influence kubwa jukwaani kiasi cha kupelekea member kibao kuniiga ukiwemo wewe kwa hakika hii ni kubwa sana inathibitisha UGoat wangu.

Hata Ronaldo na Messi kuwa watu kibao wanajifananisha na wao na kujiita majina yao . Adriz the Goat 🐐 huwezi kuwa goat mpaka wapatikane watu ambao wanakuona kama Idol wao kama ilivyo Mimi

Kesho In Shaa Allaah nakuja na bonge la Uzi la kuwashauri mnaoniiga jukwaani , kuwapa madini ile muwe intellectually gifted kama Mimi.

NiliAnticipate toka kitambo kutokana na umaarufu wangu na vipawa vyangu Kuna watu wataniiga ndio maana nikaVerify akaunti yangu sababu niliona ya mbele kijasusi .
 
Haters nawaambia nimerudi kutakuwa na 'harmony and Peace " hili ban lilinikuta nikiwa nimetoka tayari Mwanangu Selikavu alinipigia kuniambia ananiona nimekula ban

Nikambishia nikasema umeona vibaya sababu nilikuwa nimetoka Jf kwa masaa mengi mno nikiwa na dhamira ya kuicha mdogo mdogo Kisha kusepa , nikamwambia naenda kucheki hatimaye nikakuta ban la wiki Moja kwa kosa ambalo ni kichekesho sana . Nikaona anyway wamenirahishia kazi yangu maana nilikuwa naona ugumu .

Siku hiyo nilikuwa bize nachat Seran friendly nikasikia na yeye kala ban , pamoja na rafiki yangu mwingine secretarybird . Watu wote wa 3 tulikula ban siku Moja 😂

View attachment 3682970
I miss you adriz achana na haters!
 
Oya adriz halafu hayo maeneo nineishi sana.

Pande za Malawi na Yombo relini nimechili sana miaka fulani.

Nimefanya sana mazoezi hapo shule uwanjani.
Malawi street nimekaa hapo 2008 - 2009.
Kula sana bia Suncity Bar, Monie Bar, Kwa Jimmy Woodland Park, Ikizu Bar mwisho wa Lami kule kwa mbele.
Jamaa kanikumbusha mbali maeneo ya shule ya Yombo Vituka, Montfort English Medium School, Kwa Limboa, Kwa Bude sijui 😃
 
Malawi street nimekaa hapo 2008 - 2009.
Kula sana bia Suncity Bar, Monie Bar, Kwa Jimmy Woodland Park, Ikizu Bar mwisho wa Lami kule kwa mbele.
Jamaa kanikumbusha mbali maeneo ya shule ya Yombo Vituka, Montfort English Medium School, Kwa Limboa, Kwa Bude sijui 😃
Sio poa.

Hiyo barabara ya Montfort siku hizi imeekwa lami umetandikwa mkeka wa maana.

Way back hakuna lami unanyooka na hiyo road mpaka mbele kule sokoni relini.

Chini ardhi nyeusiii kwa sababu ya kuuza mkaa mda mrefu kila unapopita kweusi dadeki.

Jioni hapo relini sokoni tunaenda kula matunda nanasi za mia mbili na jero miksa machungwa na ndizi sijui kama bado wanauza.

Daah kitambo sana Lumo moja hiyoo.
 
Sio poa.

Hiyo barabara ya Montfort siku hizi imeekwa lami umetandikwa mkeka wa maana.

Way back hakuna lami unanyooka na hiyo road mpaka mbele kule sokoni relini.

Chini ardhi nyeusiii kwa sababu ya kuuza mkaa mda mrefu kila unapopita kweusi dadeki.

Jioni hapo relini sokoni tunaenda kula matunda nanasi za mia mbili na jero miksa machungwa na ndizi sijui kama bado wanauza.

Daah kitambo sana Lumo moja hiyoo.
Duh ! kumbe wewe wa kwetu kabisa .

Siku hizi Yombo nzima karibia kila sehemu lami . Soko la relini Lina historia kubwa zamani ilikuwa jioni vibe sana supu za mangozi na biashara mbalimbali.

Ijumaa msikiti ya Yombo kwa Limboa
 
Kwenye jambo Serikali ya JPM ilifanya la maana ni Ujenzi wa hizo barabara kwa kiwango Cha Lami

Nimepita juzi kidogo nipotee, bahati nilipata assistance ya Google

Jamaa ako loose Nut ametekwa na mzigo wa Vale Nafaka

Kila siku yupo busy kuupost 🤪
Miradi ya DMDP Yombo Kuna lami za viwango sana Kuna sehemu ukipita utashangaa🔥 🔥 🔥

loose Nut mkubwa hovyo , siku hizi amefuata ushauri wangu anasoma kasema anataka kuishi meaningful life amechoka Unyangwisi
 
Miradi ya DMDP Yombo Kuna lami za viwango sana Kuna sehemu ukipita utashangaa🔥 🔥 🔥
Kwa kweli imeboost sana mwonekano wa hiyo Kata
loose Nut mkubwa hovyo , siku hizi amefuata ushauri wangu anasoma kasema anataka kuishi meaningful life amechoka Unyangwisi
Itakuwa vizuri akiishi kwa mtindo huo

Nimempa ofa, nikiwa kama Mzee humu kwamba anitume na Wazee wenzangu tukampose Vale Nafaka kwa niaba yake

Yeye anaruka ruka tu, ngoja wajanja wamwahi 😅
 
Duh ! kumbe wewe wa kwetu kabisa .

Siku hizi Yombo nzima karibia kila sehemu lami . Soko la relini Lina historia kubwa zamani ilikuwa jioni vibe sana supu za mangozi na biashara mbalimbali.

Ijumaa msikiti ya Yombo kwa Limboa
Aah aah nmekaa sana pande hizo.

Pale relini sokoni kulikuwa na gari za mjini kati Kkoo zinapitia bombom na kijiwe samli kule viwandani.

Baadae njia ikawa mbaya kutokana na mvua gari zikawa hazipiti siku hizi kote wametandika mikeka ya maana.

Pia pale yombo relini kulikuwa na vipanya vya kwendea tandika unapitia darajani nyuma nyuma huku ilikuwa shoti kati moja matata sana ukipanda ukiibuka chap upo tandika.

Siku hizi yombo,lumo na kiwalani yake zimetandikwa mikeka ya kwenda.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom