Sana mkuu we achia hisia Kali sana maisha yamebalika maisha ya zamani yalikuwa happy sana .
Kuna nyumba ya jirani kwa "Mzee Gidion" nilipofika nilikumbuka zamani enzi zile Tv wanazo watu wachache sehemu nyingine mara mnafukuzwa , mara mnaambiwa msikae kwenye kochi , mara muambiwe miguu ilikuwa ladha fulani sana , vipindi vya Tv 🔥 🔥 siku ya 'Ze comedy' mieleka mtaa mzima wote wanacheki show mkikutana Vijiweni manafanya review, kuigiza na kufurahi.
Nyumba ya huyo Mzee Gidion ilikuwa kama home naingia nikiwa mchafu na majasho yangu mpirani najitupa kwenye kochi sometimes unashika mpaka rimoti bila manyanyaso nilikuwa nilicheki hapo"Jumong" ITV enzi hizo
Nilipofika nikamsalimia mkewe tukapiga stori Kisha nikaenda sebuleni nikammkuta Mzee tukawa tunapiga stori kwa furaha akaingia mkewe alipotaja jina langu ndio akanifahamu kumbe hakunijua lakini alinichangamkia na kupiga stori .
Baada ya kunijua hakuaamini maana niliondoka nikiwa young shule ya msingi sasa nimemaliza vidato na chuo uso una ndevu pia . Mzee akamwambia mkewe "ujue huyu kijana ana akili sana mpaka kutukumbuka" akanikaribisha tena kwa upendo mkubwa akaleta chakula kusema nimeshiba hakukubali akaninawisha maji kwa mikono yake na kuniambia hapa ni nyumbani ni kala na akaniletea maji ya kunywa.
Ilikuwa furaha nikamshukiru kwa wema wake kipindi cha nyuma ilikuwa hata mwanae akituleta ukorofi Mzee anasimamia haki upande wetu na alikuwa humble bila manyanyaso na kujikuta.
Wiki mbili baadae nikapewa taarifa amefariki kwa ajali , nilisikitika sana ila nikashukuri at least moments zetu za mwisho nilimpa maua yake na kumshukuru live na alikuwa happy sana kuonana