'Adriz the Goat ' nimerejea rasmi JF baada ya safari yangu meditation

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
17,595
Reaction score
39,893
Moja kwa moja ..

Mwezi wa saba mwaka huu nilichukua umamuzi wa kuondoka Jf kwa muda , malengo ya kuondoka ni mwendelezo wa utamaduni wangu wa mara kwa mara ikifika kipindi fulani nakuwa nje kabisa na mitandao ya kijamii kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kurudi tena .

Vitu ambavyo nakuwa navifanya kipindi hiko ;

1. Kukithirisha usomaji wa vitabu (soft copy & hardcopy . Usomaji wa vitabu imekuwa starehe yangu kubwa na kiliwazo tokea primary mpaka sasa na huwa napenda kusoma vitabu vya Historia , Afya , Dini , Teknolojia , Lugha na Saikolojia .

2. Kusafiri na Matembezi mbalimbali kama vile ;

a) Sehemu mbalimbali za asili na zenye mazingira mazuri ya kuvutia , mfano mzuri hapo chini πŸ‘‡



b) Sehemu nilizokulia utotoni , nilizosoma na kutembelea majirani na marafiki wa utotoni .

Napenda sana kukumbuka nilipotoka , na nasikia furaha na napata hisia nzuri nikiJiConnect na kumbukumbu nzuri za utotoni na zamani .

Nilitembelea shule yangu ya msingi ya utotoni πŸ‘‡


Nikatembelea Msikitini wa kwanza kuswali nikiwa hata sijaanza shule.

Nikakumbuka chanzo cha kuswali rafiki yangu aliniambia saa 7 mchana kutakuwa na tamthilia ya "jumba la dhahabu" enzi hizo inatamba sana . Mimi nikaenda kumuuliza Mama kama saa 7 tayari muda huo yupo na wageni yeye akasema "Mwanangu kumbe unaakili unataka kwenda kuswali ? mimi kuona soo nikasema ndio ilipofika saa 7 akamuambia Kaka yangu anipeleke msikitini na anifundishe kuswali basi tokea hapo swala na Mimi mpaka Leo Alhamdulillah.






Nikatembelea sehemu ambazo nilikuwa tunacheza mpira na ligi mbalimbali Kiwalani , nikakumbuka matukio mengi sana

Nikasikitika kukuta huu uwanja (chiniπŸ‘‡)maarufu wa " Kigorofani" ambao ulikuwa maarufu kwa ligi za kuku na Mchele , timu za mitaa mbalimbali tukishindana na ugomvi nje nje sasa umegeuka shamba wakati muda wote ulikuwa vumbi watu wakicheza boli.


Nikahitimisha kusalimia majirani na marafiki wengi . Nilikaribishwa kiFalme sana ilikuwa furaha sana kuja kuwaona baada ya miaka mingi . Nikapiga stori na kubadilishana mawazo na machizi wangu wa utotoni .

Matembezi yalikuwa marefu pia nilitembelea sehemu nyingine kama vile Upanga , Kisutu sababu nina Historia napo na nikafika mpka Kijijini kusalimia ndugu.

3. Mazoezi mbalimbali na meditation ; nikarudisha utaratibu wangu wa kufanya mazoezi mbalimbali na kuMeditate kitu ambacho nakipenda sana sababu Kuna faida kubwa kiAfya na kiakili unakuwa unaitoa kama unaitoa nje 'negative energy ' na najikuta stable and flexible ki miwili na kiakili

Vipindi ambavyo napunguza distraction nakuwa bize na Meditation.

1. Ninapokaribia kutimiza umri mpya , mfano kesho October 4 ndio siku yangu ya kuzaliwa kabla ya kufikia ndio maana kabla ya kufikia miezi ya karibuni nilitoka Jf na sehemu nyingine kwa muda ili nifocus zaidi na kujitathimi safari yangu ya maisha , yale niliyofanya nyuma , malengo yangu yaliyopita na kuweka malengo mapya .

Mimi mwaka wangu mpya unaanza tarehe ninayo zaliwa kabla ya kufika nakuwa tayari nishafanya tathimini na kuweka mipango na malengo mapya pamoja na maboresho mbalimbali.

2. Ninapoingia phase mpya ya maisha mfano , kutoka primary kwenda secondary, secondary to advance, advance to University nk , hata nikitaka 'kuoa' nitatulizana sana .

Hii kumbukumbu kipindi cha nyuma baada ya kumaliza form six , nilikataa kujiunga jeshi nikaenda Library shuleni nikachukua vitabu mbalimbali vya afya , technology, history na majarida ya New York times, Times week nk . Nikaenda pia maktaba ya dini nikachukua vitabu mbalimbali .

Mwisho nikachukua simu yangu nikaenda kariakoo nikaiuza ili nibaki free nikisoma ,kuandika mafunzo na facts mbalimbali pamoja .

Hili (pichani) lilikiwa ghetto langu hapo sehemu ya kusomea , nilikuwa nasoma zaidi ya mwanafunzi mwenye hofu na Necta kumbe ilikuwa kwa ajili ya maarifa mbalimbali tu .

NB : hapo nilipoficha nimeficha notebook πŸ““ πŸ“’ zangu ambazo ni maarufu sana naogopa nilizosoma nao wakiona watanijua utambulisho wangu halisi.



Sasa nimerudi rasmi , niliiMiss sana Jf pamoja na marafiki zangu jukwaani . Ningependa kuwastua .

1. Mighty brothers Kaka zangu wa nguvu jukwaani Selikavu Razorblade Kaka aliyetupotea Intelligent businessman

Ujumbe : Gunman nimerudi kutoka Joseon πŸ˜‚

2. Dadaz wa nguvu ;

Dada yangu kipenzi Shadeeya , Mimi nasema Yanga bingwa

Bestie wangu wa nguvu Joanah , pole sana nilipigiwa simu na Kaka Mr Kiwembe alinieleza hali yako , nilistuka sana ,pole sana nilikuombea na nitazidi kukuombea

Mwanangu sana Seran ; pamoja sana

3. Ghayos Gang ; wanangu wa Maghayo Family Babu loose Nut , muhuni Maghayo The Mongolian Savage , Usutaz Busu la Kenge na pacha mpya Adryz pamoja na mkuu wa majeshi Gengis Khan wa Jf

Ujumbe : Hata mnikatae vipi Mimi ni Gayo family ghayos Gang ni chama langu

4. Moderators
Cookie Payge and others

Ujumbe : nawakubali sana kongole kwa kazi nzuri hapa Jf

Wengineo

secretarybird Ayatollah wa Jf from Tehran ya Ikwiriri

Kaka Red black , shukran kwa kujali

Kaka Ertugrul Bey gul bay

Lamomy ; Sniper nimerudi mjengoni nimerudi

Mufti kuku The Infinity

Kaka GENTAMYCINE Mazimpaka , nakutakia kheri huko ulipo

#Nimerudi kama Gunman aliyerudi Joseon kutokea Japan
 
Hilo la kutembelea maeneo ya utotoni ulipokulia inakupa feelings fulani za nostalgia.. muda mwingine unajikuta machozi yanakutoka yaan
Sana mkuu we achia hisia Kali sana maisha yamebalika maisha ya zamani yalikuwa happy sana .

Kuna nyumba ya jirani kwa "Mzee Gidion" nilipofika nilikumbuka zamani enzi zile Tv wanazo watu wachache sehemu nyingine mara mnafukuzwa , mara mnaambiwa msikae kwenye kochi , mara muambiwe miguu ilikuwa ladha fulani sana , vipindi vya Tv πŸ”₯ πŸ”₯ siku ya 'Ze comedy' mieleka mtaa mzima wote wanacheki show mkikutana Vijiweni manafanya review, kuigiza na kufurahi.

Nyumba ya huyo Mzee Gidion ilikuwa kama home naingia nikiwa mchafu na majasho yangu mpirani najitupa kwenye kochi sometimes unashika mpaka rimoti bila manyanyaso nilikuwa nilicheki hapo"Jumong" ITV enzi hizo

Nilipofika nikamsalimia mkewe tukapiga stori Kisha nikaenda sebuleni nikammkuta Mzee tukawa tunapiga stori kwa furaha akaingia mkewe alipotaja jina langu ndio akanifahamu kumbe hakunijua lakini alinichangamkia na kupiga stori .

Baada ya kunijua hakuaamini maana niliondoka nikiwa young shule ya msingi sasa nimemaliza vidato na chuo uso una ndevu pia . Mzee akamwambia mkewe "ujue huyu kijana ana akili sana mpaka kutukumbuka" akanikaribisha tena kwa upendo mkubwa akaleta chakula kusema nimeshiba hakukubali akaninawisha maji kwa mikono yake na kuniambia hapa ni nyumbani ni kala na akaniletea maji ya kunywa.

Ilikuwa furaha nikamshukiru kwa wema wake kipindi cha nyuma ilikuwa hata mwanae akituleta ukorofi Mzee anasimamia haki upande wetu na alikuwa humble bila manyanyaso na kujikuta.

Wiki mbili baadae nikapewa taarifa amefariki kwa ajali , nilisikitika sana ila nikashukuri at least moments zetu za mwisho nilimpa maua yake na kumshukuru live na alikuwa happy sana kuonana
 
Haters nawaambia nimerudi kutakuwa na 'harmony and Peace " hili ban lilinikuta nikiwa nimetoka tayari Mwanangu Selikavu alinipigia kuniambia ananiona nimekula ban

Nikambishia nikasema umeona vibaya sababu nilikuwa nimetoka Jf kwa masaa mengi mno nikiwa na dhamira ya kuicha mdogo mdogo Kisha kusepa , nikamwambia naenda kucheki hatimaye nikakuta ban la wiki Moja kwa kosa ambalo ni kichekesho sana . Nikaona anyway wamenirahishia kazi yangu maana nilikuwa naona ugumu .

Siku hiyo nilikuwa bize nachat Seran friendly nikasikia na yeye kala ban , pamoja na rafiki yangu mwingine secretarybird . Watu wote wa 3 tulikula ban siku Moja πŸ˜‚

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…