Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

We kichwa basi. Wenzio wote wanalalamika hapa na Physics. Chemistry ilikuaga rahisi. Nimeenda report shule kama wewe nilikua naenjoy tu mtaani. Kufika shule sina lolote kichwani. Chemistry nikawa nafeli siku moja madam akaniita mbele ya darasa. Eti muoneni huyu kapata kucha rangi halafu kichwani hamna kitu. Mwanangu PCM itakushinda. Nikasema hanijui huyu. Kuanzia pale nikawa naongoza mimi somo lake class na akaanza kunipenda. Nakumbuka kwenye mock niliongoza Chemistry shuleni kwetu akanipa zawadi ya Khanga. R.I.P Madam Mwimi.
 

Mzigua inaonekana chemistry ulipiga banda necta
 
Sasa nisome nielewe ili iweje. Nikisubiri kuelewa muda wenyewe hautoshi matopic mengiii bado usistaduu unanisubiri akaa
Hahaha Masista duh nyie ndio mlipotea njia mkazama kiumen physics
 
PCH ni combination gani?
 
Basi itakuwa una sura mbaya mno maana wengi wanawake waliosoma combination za kiume sura zao huwa ngumu mno
 
Phyz ilikuwa ngumu sana lakini nilikomaa naye na ikanitoa kimasomaso NECTA.

Miongoni mwa somo lililokuwa linanipanikisha kwenye pepa ilikuwa ni Phyz.

Sikuwahi kumaliza pepa hata moja la physics, siku moja nilienda kupiga mtihani(series) kwa mtiga ilikuwa pepa one.

Mechanics ilikuwa imesimama aisee, kila swali nikigusa haliendi na lina concepts mpya. Muda wa masaa 3 nauona kama lisaa limoja.

Baada ya Mechanics kugoma nikahamia swali la Environmental Physics nikajipoza kidogo kabla navuta pumz nasikia muda umeisha, nikapanic sana. Nilirudi shule nimenuna sana.

Sikukata tamaa nikakaza buti zaidi, wiki inayofuata nikarna tena kupiga series nyingine ambayo ilikuwa pepa two.

Kufika kituoni nikakuta matokeo ya wiki iliyopita yamebandikwa, nikajikuta nipo top ten japo niliambulia 40%, kuona hivyo nikajisemea kumbe mambo yanawezekana hapa. Nikaingia kupiga pepa na kwenye pepa hiyo nikawa na above 50% nikaingia top ten pia.

Kuanzia muda huo nikawa sikosi series kila wiki huku nikikomaa kusahihisha makosa yaliyojitokeza kwenye series zilizopita, ikafika muda nikaimprove na pepa moja nikawa wa kwanza. Hadi hapo nikacha kwenda kupiga series tena.

Physics ni somo nililotumia muda mwingi na pesa nyingi kulisoma kuliko masomo mengine.
 
ukiachana na babuu aliepata umaarufu pale aza boy, mwengine nilikuaga mimi wakiniita bizzle mtata, PCM sikuwahi kuwa TO ila hamna kilichonishinda kwenye PCM. baadhi waliniitaga mchawi, maana nilikuaga sisomi, napenda kulala na kuogelea beach. basi
 

Mie chemistry ilinichefua kwanza sikuwa nikiizingatia toka o level, pili madam niliyemkuta mie alikuwa na mimba sijui mimba yake ilinichukia, kifupi mimi na yeye tulikuwa hatuivi kabisa, yaani chochote ntakachofanya darasani ni ugomvi, akiongea kitu cha kuchekesha ukicheka mtiti wakati karibia darasa zima limecheka, ukikaa kimya eti umenuna nini, akiwa anaeleza kitu ukimkodolea macho analalamika kwanini namtizama kama kinyago, siku ukisema leo simtizami ugomvi eti.

Anataja jina langu analalamika simsikilizi namdharau, kama nishasoma huko nje ni heri nitoke darasani niwapishe wenzangu kuna siku akaniambia ni heri abaki na wajinga wachachr kuliko werwvu wengi

Kuna siku alikuwa anafundisha nahisi ni organic ile na nilikuwa na hamu kichizi ya kuijua kindaki ndaki,class watu huku nyuma wakacheka, bhanabwe alipogeuka tu kageuka kageuka na mimi, simama juu unacheka nini, kutaka kumuelewesha ukawa ugomvi, ikabidi niwe mpole akaongea wee akaniamnia najitia mwerevu sana ila mwisho wa uerevu wa binadamu ndio mwandamu ndio mwanzo wa ujinga wa mungu sijui, akazira na kufundisha.

Kuja kipindi nilifikiria sijui nimtombe tu kiukweli maisha yalikuwa magumu sana kwa madam yule ilifikia hatua vipindi vyake nikawa siingii sababu najijua mwenyewe sichelew kumkata mtu makofi, nikaona niepushe shari tu
 
Huwezi amini physics topic nyingi nilijifunza mwenyewe na hii ndio huwa tabia yangu toka mdogo kuchukua kitu na kujifunza mwenyewe.. ila chemistry kila nisomavyo naona chenga na huyo mwalimu darasani chenga pia.[emoji57] [emoji57] [emoji57]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…