Afisa Elimu Jiji La Tanga, wazazi tunaomba ufafanuzi wa hii michango ya fedha

Afisa Elimu Jiji La Tanga, wazazi tunaomba ufafanuzi wa hii michango ya fedha

Katika saikolojia kuna kitu kinaitwa attention span hicho ndo kinatofautisha kizazi cha sasa na zamani kwani kizazi cha zamani walikuwa wanatumia muda mchache kujifunza na kuelewa kwani attention span yao ilikuwa kubwa ila watoto wasasa wanajifunza kwa wakati mwingi na nguvu kubwa sababu attention span yao ni ndogo.
Wazazi lazima wajue kama ndiyo policy ya serikali, siyo kila mwalimu anafanya analofikiria bila mwongozo.
 
Hiyo ni zimamoto 🔥 kisa kikiwa background mbovu ya wanafunzi,hapo wapo wasiojua kusoma,kuandika hata hesabu za kujumlisha,so walimu Wana kibarua kigumu,inabidi wapige bampa tu bampa
Mi shule zote nilisoma siku 5 tu

Hao wanakaririshwa kujibu mitihani
 
Kuna mwalimu anaitwa yusuph pangoma yule anayetrend
Swali langu ni je na zamani mlikuwa mnasoma kama anavofundisha yule mwalimu
Ifikie wakati tutambue zama zimebadilika na mbinu nazo zimebadilika na na kizazi nacho kimebadilika hivyoo serikali nayo ibadilishe mfumo wa elimu
 
Ndiyo policy ya Elimu? haya ya kujitungia walimu is not acceptable! kama hawawezi kufudisha Monday to friday, basi waache.
Suala siyo policy,walimu mikoa mingi wamepewa ultimatum ya matokea ya la7, hivyo wanayofanya ni katika kurescue situation.
 
Tanga watoto wengi vichwa ngumu aka uelewa hafifu so walimu wanahitaj nguvu ya ziada ili shule ipate matokeo mazuri
Kwa utaratibu upi? wa kujitungia au ndiyo policy ya Elimu? Siyo mwalimu anaamua kuwatoza watoto hela bila kuwa na utaratibu hela inakwenda wapi na kwa ruhusa ya nani? Watoto wasome mpaka Ijumaa, jmosi wawaache watoto wapumzike na may be kuwasaidia wazazi. Elimu haiwi hivyo kuwashindiulia watot kuzidi uwezo wao.
 
Wazazi lazima wajue kama ndiyo policy ya serikali, siyo kila mwalimu anafanya analofikiria bila mwongozo.
Walimu wanafanya kwa maelekezo ya wakuu wao na sio kwamba wakuu hawaoni ila ndo wanaona ni njia sahihi ya kusaidia kizazi chetu cha mabroiler
 
Narudia hayo yanafanyika kwa kua background ya hao watoto ni duni,na walimu wamepewa kiwango Cha ufaulu so wanachofanya ni kurescue the situation,at least ziro zipungue,hawana namna.nadhani concern yako ni pesa wanayotoza,wanahitaj motisha pia😅so wangefanya bure isingekuwa issue eti?
Yaani kila mwalimu anaamua la kwake? Hapana! Watoto wanafika nyumbani saa moja eti wanafundishwa. Fundisha yale yanayowezekana muda uliopangwa!
 
Watoto wa saiv wanatakiwa kufundishwa kwa vitendo kuliko kukaririshwa na tatizo waalimu sio wabunifu. Na mitaala imebakia kukaririsha masuala ya vita vya maji maji badala ya kwenda na wakati wa technology. Yanayofundishwa veta yangepelekwa shule ya msingi ingependeza sana
 
Kuna baadhi ya wazazi wanaoelewa maana ya elimu bora wanaona kugharamika wao ili watoto wao wapate elimu bora japo elimu yetu ndio hivyoo ina changamoto nyingi
 
Ndio maana mnaambiwa mchangie chakula ili mtoto ale shuleni Nyie mnakaza shingo.. muache mtoto ashinde shule aepukane na makundi hatarishi. Elimu ghalama..

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
Naamini na wewe umesoma, je mtoto anaweza kufundishwa masaa 10 mfululizo akawa anaelewa?

Je o-level kuna content ndefu kiasi gani kumfanya mwanafunzi aende shule saa 12 na kurudi saa 12?

Makundi hatarishi ni mazingira unayomlea mwanao,
 
Kweli nimesoma hii thread adi roho inauma wacha shule za private zitubuluze tu
Sasa hv kuna private wanafundisha kwa mtaala wa cambridge na watoto hao ni wa kitanzania(wazazi wanaoelewa maana ya elimu bora haoni tabu kumgharamia mtoto wake ili apate elimu bora)
 
Naamini na wewe umesoma, je mtoto anaweza kufundishwa masaa 10 mfululizo akawa anaelewa?

Je o-level kuna content ndefu kiasi gani kumfanya mwanafunzi aende shule saa 12 na kurudi saa 12?

Makundi hatarishi ni mazingira unayomlea mwanao,
 
Wazazi sijui mnataka nini? Watoto wakifeli mnalalamika waalimu wakiwasaidia watoto kujiandaa na mitihani mnalalamika. Hizo shule za private mnaona wanavyoandaa watoto na mitihani. Watoto hao wa private wanashindana na hao watoto wenu.

Wazazi msipende vya bure wajibika kwa elimu ya mtoto wako kughalamia shilingi elfu tatu kwa wiki kwa ajili ya elimu ya mtotk wako unaona ni gharama?
Unataka mwalimu afanye kazi ya ziada lakini usimlipe. Wasikilizeni wana siasa wenyewe watoto wao wako private wanawalipia wewe wanakudanganya.
Wewe acha hizo mambo! Nadhani kila mtu hapa amesoma, hamna cha kusaidia wala cha rafiki yake na kusaidia, mtoto anatakiwa kupumzika siyo kila mara anasoma, we angalia ule muda rasmi tu wa wanafunzi kuwa shuleni yaani saa mbili hadi saa tisa na nusu, unakuta wanafunzi wengi wamepiga usingizi, sasa uje uwasomeshe mpaka saa 12 jioni kuna wa kuelewa hapo!! Acheni utani
 
Back
Top Bottom