Afisa Elimu Jiji La Tanga, wazazi tunaomba ufafanuzi wa hii michango ya fedha

Huku mwisho sijakuelewa mkuu,,,maana Hiki wanachokifanya hawa walimu kilifanyika hata kabla Serikali haijatangaza Elimu Bure, wanafunzi walikuwa wanatoa hela ili wasome masomo ya Ziada,,,, na unakuta mwalimu haingii kipindi chake cha kawaida ambacho kinafanya alipe mshahara ila anawaambia wanafunzi walipe kiasi cha hela ili afundishe muda wa ziada,,, so huu ukilitimba uliafanyika kabla hata Serikali haijatangaza Elimu Bure,,, Sanasana ilikuwa Shule za mijini ndiyo zinafanya huu ukilitimba.
 
Unayaona hawa wanaokupinga hivi. Ndiyo hivihivi inavyotokea kwenye sekta ya afya, wanajua kila kitu kinaendeshwa kwakufuata policy za serikari wakati kazi ya serikari bila extra efforts au ukiamua kufuata policy totally hutafanikisha chochote na watakaoumia ni wao wenyewe wananchi. Wanavyoongopewa na wanasiasa wanayabeba matamko kama yalivyo wakati hali ni ya tofauti, mwanasiasa ni muongo ila watanzania nao wanapenda sana kuongopewa wakijua kila kitu serikari inaweza kuingia gharama kubwa kwasababu yao. Nchi ngumu hii
 
Tatizo lingine shule za msingi Zina uhaba mkubwa sana wa walimu
Shule nyingi Zina walimu kuanzia 4 Hadi 6.wakati shule Kuna darasa la awali Hadi la Saba.
Nashindwa kuelewa kwanini mtoa mada hakuelewa hichi kitu. Yaani hakufikiria underlying cause ni nini! Madarasa yapo kama 8 huku tena yamegawanywa tena kiherufi kwakila darasa na kila mwaka serijari lazima iweke target goals mtumishi lazima afikishe lakini mwananchi hujali yanaowahusu wao tu na kumlaumu mtumishi sio serikari. Sasa watu 4 watafundisha watoto wote hao.
 
Siku nikipata ajirabyenyewe hii,nifuata utaratibu wa serikali tu. Haya mambo mengine nitaonekana najipendekeza tu
Yaani watanzania hawaelewagi kabisa hili kuwa extra efforts ni mtu kajitoa. Policy za serikari zikifuatwa watatukana kila taasisi na idara ya serikari, ila hawajuagi kabisa.
 
Yaani watanzania kwaujumla wanapenda tu malalamiko yasiyokuwa na msingi. Kwaujumla hawajui jinsi ya kuchambua tatizo na kujua mzizi hasa ni nini. Kazi kulalamika, hapo ndipo ninapoona kweli utu uzima sikuizi sio dawa.
 
Kimsing hii KPI ina changamoto zake, walimu wamejaza mkataba Kwa kufaulisha Zaid ya 50% huku mazingira hayaruhusu. Najiulizaga Daktar akiua mgonjwa anafanywa nini? kwanini mwalim apewe mkataba wa kufaulisha, Kwan kufaulu ni issue ya mwalim peke yake?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ya sekta ya afya usoyoyajua bora usiyaongelee tu chief. Hamna mtumishi wa serikari anaishi maisha mazuri jua hilo. Nenda kawe daktari kwanza uue halafu ndio tujaribu kujua utafanywa nini[emoji23][emoji23][emoji23].
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…