zamani hakukua na shinikizo la kufaulisha, hata likifeli darasa zima poa Tu. Sasa hiv tamisemi wamekuja na Key performing Indicators, shule zimepewa malengo zifikie, kila mwalim, kila shule, kila wilaya na kila mkoa wanatakiwa kuwa na mpango kazi kufikia malengo.
Heb tuwape ushirikiano walimu maana wanaosaidiwa ni watoto wetu, tusitafute vikwazo tu, Kwanza zamani tulikua tunachelewa Sana kuanza shule, wengi wetu tulianza na miaka 9 ama 10, Sasa hiv miaka hiyo ni la 4 au 5 hivyo hawajielew hata wamefata nini shule. Sisi zamani tulikua tunaulizana maeneo kwenye Atlas, miji mikuu, tuna madaftari tunaandika viongozi wa serikali, mawaziri, wakuu wa wilaya na mikoa, Tulikua na vitabu vya JIANDAE VEMA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI. Kwa kiasi kikubwa tulikua tunajiongoza wenyewe.
Hawa watoto wa sasa hawajakomaa kisawasawa hawana self determination kama tulivyokua Sisi, Siri moja kubwa wanatumia Sana seminary na shule binafsi na kumkeep mtoto busy Kwa kumpa mazoez ya kutosha.Idle brain is a source of evils ndo maana hata private mtoto akirud jioni anakuja homework akifunga shule anakuja na home package anapambana na maswali mpaka shule zinafunguliwa. Kama unataka mtoto acheze mpeleke shule yenye sports academy.