Afisa Elimu Jiji La Tanga, wazazi tunaomba ufafanuzi wa hii michango ya fedha

Afisa Elimu Jiji La Tanga, wazazi tunaomba ufafanuzi wa hii michango ya fedha

1. Kila asubuhi watoto eti wanafanya mitihani. Mtoto anawajibika kuripoti shuleni saa 12 asubuhi na kuanza mtihani saa 12.30 asubuhi. Ada shiling 200 kila asubuhi.

2. Jumamosi mtihani. Toka saa 1 mpaka saa 7 mchana. Ada ya mtihani shilingi 1,200. Hii ndiyo utaratibu kutoka ofisini kwako? Au ni invention ya walimu kwamba kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake?

3. Mtoto anarudi saa 11 jioni. na break ya saa nne ni kama haipo maana wanapewa dakika 5 kwenda kujisaidia. Shule inafungwa saa ngapi?

4. Wazazi tujue shule inafungwa saa ngapi tuweze kuwafuatilia watoto vema kama wanafika nyumbani inavyotakiwa.

OMBI: Waacheni watoto Jumamosi wapumzike na kuwasaidia wazazi.
Wazazi ongeeni na walezi wenzenu (shule). Watoto wako mikononi mwenu!
 
unaongelea zamani ipi, Kwanza zamani ilikua likizo lazima twende tution maana walimu walikua hawamaliz topics, kama hujaenda tution unakuja kuomba rafiki akufundishe. Zamani hakukua na shinikizo walimu wafaulishe, hivyo ilikua ukikaa kusubir ufundishwe kila kitu imekula kwako. O level nimesoma mpwapwa sec na advance Musoma
Tangu nizaliwe sijawahi soma kitu inaitwa tuition. Enzi zetu (za Mwalimu) mambo yalikwenda Kwa mpangilio sana
 
Wewe ndio kichwa maji,unafikiri kazi ni kufundisha mda wote!
Njaa ya mwanao unamweleza nani mwenye jukumu la kumlisha?
Mlipie mwanao chakula na stationaries acha kujibebisha.
Wenzio wanasomesha Private na wanalipa pesa nyingi husikii walalamika.
We elfu tatu kwa wiki ushatukana walimu!
Nyie mlichobakia nacho kichwani ni kuchapa tu
 
Kwa uwingi wa watoto kwa darasa moja pale Olympio na level ya ufaulu wanayopata ni sahihi kabisa njia wanayotumia.Niliangalia matokeo darasa la saba Olympio darasa lina wahitimu zaidi ya 600.Ndiyo maana wazazi wengi wanapeleka watoto wao hapo maana ni nafuu na bado inashindana na shule nyingi za Private zenye ada kubwa.

Walau Wazazi tu appreciate juhudi za walimu kuwapatia elimu watoto wetu.
ok
 
zamani hakukua na shinikizo la kufaulisha, hata likifeli darasa zima poa Tu. Sasa hiv tamisemi wamekuja na Key performing Indicators, shule zimepewa malengo zifikie, kila mwalim, kila shule, kila wilaya na kila mkoa wanatakiwa kuwa na mpango kazi kufikia malengo.

Heb tuwape ushirikiano walimu maana wanaosaidiwa ni watoto wetu, tusitafute vikwazo tu, Kwanza zamani tulikua tunachelewa Sana kuanza shule, wengi wetu tulianza na miaka 9 ama 10, Sasa hiv miaka hiyo ni la 4 au 5 hivyo hawajielew hata wamefata nini shule. Sisi zamani tulikua tunaulizana maeneo kwenye Atlas, miji mikuu, tuna madaftari tunaandika viongozi wa serikali, mawaziri, wakuu wa wilaya na mikoa, Tulikua na vitabu vya JIANDAE VEMA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI. Kwa kiasi kikubwa tulikua tunajiongoza wenyewe.

Hawa watoto wa sasa hawajakomaa kisawasawa hawana self determination kama tulivyokua Sisi, Siri moja kubwa wanatumia Sana seminary na shule binafsi na kumkeep mtoto busy Kwa kumpa mazoez ya kutosha.Idle brain is a source of evils ndo maana hata private mtoto akirud jioni anakuja homework akifunga shule anakuja na home package anapambana na maswali mpaka shule zinafunguliwa. Kama unataka mtoto acheze mpeleke shule yenye sports academy.
ok
 
Kwa mwendo huu shule za private zitaendelea kuwa juu. Kuba shule inaitwa Kings secondari ipo Goba, saa kumi na moja napita kwenda job mwalimu yupo class na madogo wanapambana, ww umeambiwa mtoto akafanye pepa jumamosi unalalamika kama mwl anahusika na toto lako. Kama vp kataza bonto lako lisiende af jaribu ujinga

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Huko ni kukaririsha watoto.
Mbona sisi tumesoma
Saa 2-8?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilikua na mtoto st fransis mbeya, Mtoto akifunga shule anakuja na maswali mengi Sana, Yan akitoka chumbani ni kuja Kula na kurudi chumbani kufanya maswali mpaka wanafungua, mpaka namuonea huruma mtoto. Matokeo kutoka watoto wote one za Saba na nane chache, Nina mtoto mwingine lasaba mwaka huu wazaz tumetoa mil 1 Kwajil ya masomo ya ziada, ELIMU ni gharama, hakuna kizuri chabure
Kukaririshwa ndio mnaona sifa

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Huko ni kukaririsha watoto.
Mbona sisi tumesoma
Saa 2-8?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Lakini bado ulikariri midhari ulisoma hapa hapa Bongo. Inanikumbusha Wazazi wetu pia enzi tunasoma walikuwa wanapondea mfumo wa ufundishaji enzi zetu na wakisifia elimu ya enzi zao.Wazazi tuwape ushirikiano walimu ili watoto wetu wasome
 
unaongelea zamani ipi, Kwanza zamani ilikua likizo lazima twende tution maana walimu walikua hawamaliz topics, kama hujaenda tution unakuja kuomba rafiki akufundishe. Zamani hakukua na shinikizo walimu wafaulishe, hivyo ilikua ukikaa kusubir ufundishwe kila kitu imekula kwako. O level nimesoma mpwapwa sec na advance Musoma
zamani ulikuwa hujazaliwa. And why a lot of materials at this time? watoto wafundishwe mambo kidogo ambayo yanahitajika katika maisha yao.
 
1. Kila asubuhi watoto eti wanafanya mitihani. Mtoto anawajibika kuripoti shuleni saa 12 asubuhi na kuanza mtihani saa 12.30 asubuhi. Ada shiling 200 kila asubuhi.

2. Jumamosi mtihani. Toka saa 1 mpaka saa 7 mchana. Ada ya mtihani shilingi 1,200. Hii ndiyo utaratibu kutoka ofisini kwako? Au ni invention ya walimu kwamba kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake?

3. Mtoto anarudi saa 11 jioni. na break ya saa nne ni kama haipo maana wanapewa dakika 5 kwenda kujisaidia. Shule inafungwa saa ngapi?

4. Wazazi tujue shule inafungwa saa ngapi tuweze kuwafuatilia watoto vema kama wanafika nyumbani inavyotakiwa.

OMBI: Waacheni watoto Jumamosi wapumzike na kuwasaidia wazazi.
Mwanangu yuko grade 6 na anaenda hadi jumamosi...anarudi saa10..inanikwaza mno mno sasa sijajua grade 7 wataenda had j'pili...?argh
 
Mimi nilikua na mtoto st fransis mbeya, Mtoto akifunga shule anakuja na maswali mengi Sana, Yan akitoka chumbani ni kuja Kula na kurudi chumbani kufanya maswali mpaka wanafungua, mpaka namuonea huruma mtoto. Matokeo kutoka watoto wote one za Saba na nane chache, Nina mtoto mwingine lasaba mwaka huu wazaz tumetoa mil 1 Kwajil ya masomo ya ziada, ELIMU ni gharama, hakuna kizuri chabure
Halafu St.Francis wakifanya vizuri kitaifa,watu wanaanza kusema kuwa wanachukua watoto wenye vipaji maalumu tu .Hii juhudi inayowekwa na Walimu kwa hao watoto huwa hatuioni kabisa.
 
Mwanangu yuko grade 6 na anaenda hadi jumamosi...anarudi saa10..inanikwaza mno mno sasa sijajua grade 7 wataenda had j'pili...?argh
Wapi huko? Grade hazitumiki Tanzania... Watoto wanalundikiwa mambo mengi ambayo hayana faida maishani mwao. wanaongeza muda eti Eti wanamaliza syllabus. Kwanini upuuzi mwingi kwenye sylabus?
tatizo kubwa
 
yaani ada hulipi unaambiwa umchangie mwalimu 200 kwa siku ili mwanao afaulu mtu anaona tabu!!!? dah! asee kuzaliwa bongo sio siri ni laana.

hizi sababu ndo zilinipelekea nikaishia njiani kimasomo, unakuta mzazi hawezi kumudu gharama za kukusomesha kiasi cha kukufanya u-concentrate na masomo pekee. Hadi unakufuru kwamba alikuzaa ya nini au hakujua wajibu wake wa kukusomesha?
 
basi nitaliforward kwa waziri! Wawaache watoto wasome muda uliopangwa na serikali. kama kufeli wacha wafeli
Hivi unajua maana ya kufeli au unaangalia ile zero,kufeli maana yake mwanafunzi hakupata stadi alizokusudiwa kupata,kama alitakiwa kujua kusoma maana yake anatoka bila kujua kusoma,kama alitakiwa kujua kuandika anaondoka bila kujua kuandika, huko ndio kufeli, Je lengo la kwenda shule ni hilo? kwamba aende shule na aondoke kama alivyokuja? Sasa ukisema kama kufeli na wafeli maana yake kusiwepo na shule kwa sababu hatutaki watoto wajue kuhesabu,kuandika na kusoma,
 
Back
Top Bottom