Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Hii ni hatari sana. Ina maana kutoa maoni ni kosa? Ibara ya 18 ya katiba JMT inasema vipi?

20220822_120746.jpg

20220822_120749.jpg

20220822_120752.jpg


TAMKO LA TRC
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema: “Kwa sasa sijapata taarifa rasmi ya suala hilo, nalifanyia kazi kisha nitatoa taarifa rasmi,” - Jamila
 
Tanzania hatuna tofauti na nchi kama South Korea, Russia, Cuba na China ..... Bado tuko kule kule kwenye zama .... Naona itakuwa ngumu sana kutoka huko mpaka pale CCM itakapotoka madarakani.....!!
Kuifananisha nchi inayo nuka umasikini[ Tanzania ] na mataifa Kama China, Russia, South Korea unaya vunjia sana heshima hayo mataifa.
 
Kumkosoa muheshimiwa raisi kistaha siyo kosa!Ila nadhani meneja alitukana viongozi matusi mazito ya nguoni tena bila staha,Mama ameamua kumparura😬

Kwa jicho la mbali naona hata akikata rufaa hashindi.
Tuko gizani sana, nahisi siku ikitokea mtu akachana hotuba ya raisi anaweza akapigwa shaba on the spot. Refer to what Pelosi did to Donald Trump 😂😂😂
 
Kumkosoa muheshimiwa raisi kistaha siyo kosa!Ila nadhani meneja alitukana viongozi matusi mazito ya nguoni tena bila staha,Mama ameamua kumparura😬

Kwa jicho la mbali naona hata akikata rufaa hashindi.
Hashindi si kwa sababu hana haki, ila ni kwa sababu hatuna organ yenye nguvu kumzidi raisi. Si bunge wala mahakama ambalo linaweza kupingana na matakwa ya raisi. A cursed state
 
Hili ni tatizo la kiutamaduni ni big problem. utamaduni wetu ni wa kijinga katika suala ukosoaji tuko ziro eti mkubwa hakosei na hakosolewi, ni upumbavu tu. Ili nchi isonge mbele watoto wafundishwe kuwa kukosoa wakubwa ni sahihi na wakubwa kuomba msamaha wadogo wanapowakosea ndio modern civilization!

Jamaa kaonewa ana haki ya kukata rufaa maana kuna haki za binadamu "freedom of speech" zifuatwe tumesaini wenyewe UN!
 
Back
Top Bottom