Hata Ndugai alifukuzwa baada ya kusema 2025 watu waamue kati ya huyu bibi tozo na asiyekuwa na haya matozo.
Hivi Ndugai nae mnamhurumia?
Nina sababu mbili zakutomuonea huruma huyo bwana na napenda kukushawishi uungane NAMI.
1: Mahali alipo semea hapakua sahihi .
Ndugai alikua sipika,
Kwakanuni walizo jitungia hahojiwi namamlaka yeyote kwa maneno alio yasema akiwa Bungeni.
Je ni wazimu gani walimupelekea kutohoji hiyo mikopo ndani ya mjengo ambako angepewa majibu ,pengine yasio lizisha nasisi wapiga kura tungepima nakuchekecha.
Pia bunge kama chombo lingepata nafasi ya kujadili na kushauli.
Ikumbukwe Bungeni yumo waziri wa fedha na mwana Sheria mkuu.
2:Ndugai kama kiongozi mkuu wa wa bunge , alikua na nafasi ya kuitisha kura ya kutokua na Imani na Rais.
pengine asingefanikiwa kufika kwenye kipengere Cha kupiga kura, kulingana najinsi chama chenyewe kilivyo jawa nawatu woga hata nje yahuyo anae pigiwa kura.
Bila kujali angeondolewa kati kahatua ipi kabla ya kamilisha zoezi tajwa, angeheshimika kwangu nawapenda Democrasia Duniani .
Kitendo chakwenda kujifungia Kongwa nawale walio itwa wazee nikitendo Cha uoga na unafiki, hakistahili hata kuonewa huruma.