Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Makundi ya kijamii yepi aliyotolea maoni. Au ni hapa JF.
 
Hii ni hatari sana. Ina maana kutoa maoni ni kosa? Inara ya 18 ya katiba JMT inasema vipi?

TAMKO LA TRC
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema inawezekana ni kweli kwa kuwa mhusika alikuwa na matatizo kadhaa na uongozi.

“Kwa sasa sijapata taarifa rasmi ya suala hilo, ninachojua mhusika alikuwa na changamoto kadhaa na uongozi na suala lake lilikuwa linashughulikiwa,” - Jamila
Ndio vizuri akakosoe vizuri huko Nje
 
Utakuta wala amri haikutoka juu.
Utakuta ni watu tu wasiojiamini na wanachofanya na kutegemea kupata mileage kisiasa kwa maamuzi kama haya au watu wanaodhani bado tuko kwenye enzi zileee za kuabudu watu....
Hata hizo enzi unadhani kila maamuzi ilikuwa ni amri kutoka juu? Kuabudiana kunaendelea tu.
 
Wengine tunacomment hapa huku tukitetemeka wasije wakatu pyuu pyuu.
 
Ukifukuzwa kazi unapata mafao /pension ya muda uliohudumu kazini ?
 
Akimpata wakili mzuri asiyeogopa vitisho anashinda kesi mapema
Anashinda mapema kivipi wakati ameelekezwa kukata rufaa tume ya utumishi wa umma ambako nako licha ya rufaa kusikilizwa baada ya miaka 3 toka kuwasilishwa, watasema rufaa yake haina mashiko na kisha watamwelekeza akate rufaa kwa Rais wa JMT, huko maamuzi yake ushajua yatakuaje. Usisahau kuwa Rais anaweza kutoa maamuzi ya rufaa hiyo hata baada ya miaka 4...umapema unatoka wapi happ mkuu?
 
Hata ukiwekeza kwa kujenga kiwanda, shule, hoteli, hospitali, ama kuanzisha kampuni. Ukiikosoa ccm utaijua kwann Ina rangi ya kijani.
Afadhali huko, lakini kuisema serikali ukiwa serikalini ni suicide mission
 
Shida Ni kutoa maoni . Serikali ukitoa maoni tofauti nayo Ni matusi.
Ndio ukweli..... tafuta shughuli nyingine kama nia yako ni kuwa huru. Hata ingekuwa ni private company, wasingeruhusu mfanyakazi wao auseme vibaya uongozi wa kampuni.... nenda kwa Bhakhresa kamseme vibaya yule mzee uone kama utaachwa
 
Wewe unaishia Dunia gani?Unakumbuka kilichomfukuzisha Mafuru pale hazina?Alialikwa clouds 360,akahojiwa kuhusu malalamiko ya wananchi kwamba vyuma vimekaza!Akatoa sababu za kiuchumi ikiwa ni pamoja na serikali kubana matumizi,serikali kufanya miradi mikubwa inayochukua pesa nyingi Kwa pamoja hivyo pesa nyingi kwenda huko na hivyo kupunguza mzunguko wa ndani!

Baada ya hapo,alikutana na barua ya kutumbuliwa ofisini!
Na pia alisema "... Kwa kuwa yeye ndio msajili wa Hazina(TR) hakuna mtumishi wa umma anayelipwa milioni 40(40M).."
Na wakati jiwe alishawahi tuambia kuwa kuna watumishi walikuwa wanalipwa milioni 40 na zaidi.
Alikanusha taarifa ya Rais.
Kesho yake wakala kichwa na kuteuliwa Dr. Mashindano kutoka idara ya uchumi Udsm kuwa TR mpya.

Nilikuwa nachomekea tu...!!
 
Sijabahatika kuona alichokiandika hicho inachosemekana ametukana lakini naye si ilimpasa kujiongeza...sasa mpo kwenye Mtumbwi alafu unagombana na anayeuendesha....kweli.

Ye haoni wengi wanaokosoa ni mpaka wnapokuwa Upinzani, yaaani tayari wanakuwa na mlo mbadala.

Kuna na yule wa kule Zenji naye alisema alichosema waka dili naye...nasikia ameshaokoka.
 
Hili ni tatizo la kiutamaduni ni big problem. utamaduni wetu ni wa kijinga katika suala ukosoaji tuko ziro eti mkubwa hakosei na hakosolewi, ni upumbavu tu. Ili nchi isonge mbele watoto wafundishwe kuwa kukosoa wakubwa ni sahihi na wakubwa kuomba msamaha wadogo wanapowakosea ndio modern civilization!

Jamaa kaonewa ana haki ya kukata rufaa maana kuna haki za binadamu "freedom of speech" zifuatwe tumesaini wenyewe UN!
Ukishakuwa kwenye nafasi ya utendaji, huna privilege ya kukosoa au kupinga.
Wanasiasa wakishasema, wewe unatakiwa kuitikia; 'Na iwe hivyo'...
Otherwise vua koti la utumishi wa umma uje kupambana kwenye majukwaa ya kisiasa.
 
Na pia alisema "... Kwa kuwa yeye ndio msajili wa Hazina(TR) hakuna mtumishi wa umma anayelipwa milioni 40(40M).."
Na wakati jiwe alishawahi tuambia kuwa kuna watumishi walikuwa wanalipwa milioni 40 na zaidi.
Alikanusha taarifa ya Rais.
Kesho yake wakala kichwa na kuteuliwa Dr. Mashindano kutoka idara ya uchumi Udsm kuwa TR mpya.

Nlikuwa nachomekea tu...!!
🤣🤣 Sasa huyo jamaa alikuwa anasema JPM hakuwahi kutenda hivyo! Tena jamaa aliongea kistaarabu kabisa!
 
Hii ni hatari sana. Ina maana kutoa maoni ni kosa? Inara ya 18 ya katiba JMT inasema vipi?

TAMKO LA TRC
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema inawezekana ni kweli kwa kuwa mhusika alikuwa na matatizo kadhaa na uongozi.

“Kwa sasa sijapata taarifa rasmi ya suala hilo, ninachojua mhusika alikuwa na changamoto kadhaa na uongozi na suala lake lilikuwa linashughulikiwa,” - Jamila
CCM OYEEEE !!
 
Back
Top Bottom