Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Makundi ya kijamii yepi aliyotolea maoni. Au ni hapa JF.
 
Ndio vizuri akakosoe vizuri huko Nje
 
Utakuta wala amri haikutoka juu.
Utakuta ni watu tu wasiojiamini na wanachofanya na kutegemea kupata mileage kisiasa kwa maamuzi kama haya au watu wanaodhani bado tuko kwenye enzi zileee za kuabudu watu....
Hata hizo enzi unadhani kila maamuzi ilikuwa ni amri kutoka juu? Kuabudiana kunaendelea tu.
 
Wengine tunacomment hapa huku tukitetemeka wasije wakatu pyuu pyuu.
 
Ukifukuzwa kazi unapata mafao /pension ya muda uliohudumu kazini ?
 
Akimpata wakili mzuri asiyeogopa vitisho anashinda kesi mapema
Anashinda mapema kivipi wakati ameelekezwa kukata rufaa tume ya utumishi wa umma ambako nako licha ya rufaa kusikilizwa baada ya miaka 3 toka kuwasilishwa, watasema rufaa yake haina mashiko na kisha watamwelekeza akate rufaa kwa Rais wa JMT, huko maamuzi yake ushajua yatakuaje. Usisahau kuwa Rais anaweza kutoa maamuzi ya rufaa hiyo hata baada ya miaka 4...umapema unatoka wapi happ mkuu?
 
Hata ukiwekeza kwa kujenga kiwanda, shule, hoteli, hospitali, ama kuanzisha kampuni. Ukiikosoa ccm utaijua kwann Ina rangi ya kijani.
Afadhali huko, lakini kuisema serikali ukiwa serikalini ni suicide mission
 
Shida Ni kutoa maoni . Serikali ukitoa maoni tofauti nayo Ni matusi.
Ndio ukweli..... tafuta shughuli nyingine kama nia yako ni kuwa huru. Hata ingekuwa ni private company, wasingeruhusu mfanyakazi wao auseme vibaya uongozi wa kampuni.... nenda kwa Bhakhresa kamseme vibaya yule mzee uone kama utaachwa
 
Na pia alisema "... Kwa kuwa yeye ndio msajili wa Hazina(TR) hakuna mtumishi wa umma anayelipwa milioni 40(40M).."
Na wakati jiwe alishawahi tuambia kuwa kuna watumishi walikuwa wanalipwa milioni 40 na zaidi.
Alikanusha taarifa ya Rais.
Kesho yake wakala kichwa na kuteuliwa Dr. Mashindano kutoka idara ya uchumi Udsm kuwa TR mpya.

Nilikuwa nachomekea tu...!!
 
Sijabahatika kuona alichokiandika hicho inachosemekana ametukana lakini naye si ilimpasa kujiongeza...sasa mpo kwenye Mtumbwi alafu unagombana na anayeuendesha....kweli.

Ye haoni wengi wanaokosoa ni mpaka wnapokuwa Upinzani, yaaani tayari wanakuwa na mlo mbadala.

Kuna na yule wa kule Zenji naye alisema alichosema waka dili naye...nasikia ameshaokoka.
 
Ukishakuwa kwenye nafasi ya utendaji, huna privilege ya kukosoa au kupinga.
Wanasiasa wakishasema, wewe unatakiwa kuitikia; 'Na iwe hivyo'...
Otherwise vua koti la utumishi wa umma uje kupambana kwenye majukwaa ya kisiasa.
 
🀣🀣 Sasa huyo jamaa alikuwa anasema JPM hakuwahi kutenda hivyo! Tena jamaa aliongea kistaarabu kabisa!
 
CCM OYEEEE !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…