Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Sasa itabidi atume CV zake kwa Mbowe au Martin, si munaona sifa nyinyi kutukana mitandaoni? Kisa Mama
Mzanzibari munapayuka tu, sasa aende akatafute jembe akalime
 
Ni Mafuru pekeake ndio alitumbuliwa wakati huo?

Tuoneshe barua ya kutumbuliwa kwake na sababu za kutumbuliwa kwake.
We jamaa vipi?Yaani mtu anatoka studio tu kusema hayo aliyosema halafu anakutana ofisi na barua ya kutumbuliwa!
Soma between lines,tofauti na hapo utakuwa unakaza tu mshipa bila sababu zozote!
 
Sasa itabidi atume CV zake kwa Mbowe au Martin, si munaona sifa nyinyi kutukana mitandaoni? Kisa Mama
Mzanzibari munapayuka tu, sasa aende akatafute jembe akalime
Wewe ni mpuuz unayeona hakuna maisha nje ya ajira ya serikali!
Yaani mtu kulalamika tozo kila mahali ndio kutukana,kweli wewe ni bogus!
 
Tunaishi zamani wakati dunia inaishi nyakati nyingi zijazo, dunia inaishi kuleeee mbele, sisi tunaishi kuleee nyuma.
 
Sasa mkiona watu wamenyamaza au kusapoti kila kitu muwaelewe. Huyu ana bahati kufukuzwa kazi. Yaani kufukuzwa kazi ashukuru Mungu.
Trust mi mchongo mzima umefanikishwa na chawa tu, maza hajui lolote hapo na lengo ilikua kumuondoa jamaa kwenye system tu. Seems hakuwa na compatibility na walamba asali. Yani hapo wamepata solid reasons za kumuharibia tu.
 
Kuna ma group hata niwekwe iwe lazima natoka.
Nimebaki na group la Connection tu..hakuna cha michezo wala Bibi yake nani.
 
Hashindi si kwa sababu hana haki, ila ni kwa sababu hatuna organ yenye nguvu kumzidi raisi. Si bunge wala mahakama ambalo linaweza kupingana na matakwa ya raisi. A cursed state
Na hapo atakapo kata rufaa ya tume hio asiporidhika swala lake linapelekwa kwa Raisi maana mtumishi wa umma kesi yake na muajiri wake haiendi mahakamani
 
Na hapo atakapo kata rufaa ya tume hio asiporidhika swala lake linapelekwa kwa Raisi maana mtumishi wa umma kesi yake na muajiri wake haiendi mahakamani
Anaenda kula za kichwa 😀
 
Mashirika ya Umma yamejaa makada watiifu wa chama Cha mboga mboga hamna wanalo jua zaidi ya uchawa
Hata kama kulikuwa na kumdhalilisha Rais, mwajiri hana mamlaka ya kumfukuza mfanyakazi kwa kosa hilo kwa kuwa halihusiani na kazi ya mwajiriwa. Sana sana Serikali inaweza kumshitaki mtuhumiwa chini ya vipengee vingine vya sheria na akaadhibiwa kwa kutozwa faini au kufungwa lakini si kwa kufukuzwa kazi kwa kuwa kosa halihusiani na utendaji wa kazi.
 
Back
Top Bottom