Aghairi kufunga ndoa iliyogharimu Tsh. 950m baada ya Mchumba wake kukataa kusaini PreNup

Kabisa, unajua ule mgawanyo wa mali, uliwekwa sababu mke ndiyo mfanya kila kitu kwa mume. Huduma zote za nyumbani. Ila sasa imeshakuwa nongwa, wanaona mwanamke anafaidi. Bora kila mtu abaki na chake tu.
Wazo zuri. Shida inakuja kwa baadhi ya wanawake wanaoingia ndoani kwa malengo ya muda mfupi. Yaan mtu anaingia ndoani kajipanga kuwa baada ya miaka 2, 3 tunaachana tunagawana hao ndio walioharibu game.

Zaman watu walikua wakiachana na wanagawana haikua shida. Ila siku hizi imekua ka mchezo ka maksudi kabisa.

Kuna jamaa alioa mwanamke yy ni mfanya biashara na binti alikua mtu wa home, alimtoa kwao. Wakati wanaoana jamaa alikua amepanga ila alikua na kiwanja na ka spacial kake.

Baada ya kuoana wakashauriana waanze kujenga. Kweli wakaanza. Mwamba akawa ni mtu wa kutafuta mpunga anampa mwanamke akafanye jambo kwenye ujenzi wao.

Bwana we, kumbe binti ni akili nyingi kuliko mchizi. Binti alikua kila anaponunua kifaa cha ujenzi (tofari, mchanga, mawe, sment nk) risiti alikua anaandika jina lake. Mwamba hakuona kama ni shida hio kwa kua mwanamke si ndio alienda kununua.

Baada ya nyumba kukamilika wakahamia. Wakakaa miezi kama 9, 10 hivi binti akalianzisha waachane. Purukushani hadi mahakamani. Kufika mahakamani ikaonekana ile nyumba ni mali halali ya mwanamke na mwanaume hakuchangia kitu. Sababu ni ushahidi wa zile risiti za vifaa vya ujenzi ambazo zote zina jina la mwanamke

Mahakama ikaamua, ile nyumba iuzwe na pesa ya nyumba apwe mwanamke, na mwanaume apewe pesa ya kiwanja chake. Kisha mali zingine walizo nazo wagawane sawa. Mwamba alilia kilio cha mbwa koko aliyeshikwa na chatu.

Mazingira kama haya yanaonesha kuwa kwa miaka ya sasa, 80% ya wanawake huolewa kwa malengo ya mali. Ndio maana wanaume wamesanuka siku hizi.
 
Huo utakuwa mkataba mzuri ili kuzuia uhuni wa wanawake wapenda pesa na kuiba mali za wapambanaji. Maana nasikia wapo wanawake wa kizungu ambao kazi Yao ni kupola mali za wanaume Kwa kufata Sheria inayowalinda. Sasa wamekwisha [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni shujaa lakini hajamfikia Ashraf.

Wanawake wengi wanaingia jwenye ndoa ili wadhulumu mali.

KUna wanaoua waume zao na kurithi mali, kuna wanaorubuni mali ziandikwe majina yao kisha baadae wake hao wanaruka kuwa mali ni zao binafsi kuna wanaosomeshwa na wanaume kwa ahadi ya kuolewa nao huku wakijua hawawezi kamwe kukubali kuolewa na hao waliowasomesha; wakishindwa haya yote ndipo mahakama hutumika kama lqst resort ya kumnyang'anya mume mali.
 
Kwa hivyo nilijiambia yeyote ambaye nimeolewa naye, wanasaini prenup , hataki hakuna ndoa." Alisema Jackson

ameolewa naye ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…