Aghairi kufunga ndoa iliyogharimu Tsh. 950m baada ya Mchumba wake kukataa kusaini PreNup

Aghairi kufunga ndoa iliyogharimu Tsh. 950m baada ya Mchumba wake kukataa kusaini PreNup

Ile kesi ya mchezaji wa zamani wa Arsenal ,Ebue kwa jina la utani tulikiwa tukimuita mpoki,imewafunza mastaa wengi,manaake Ebue baada ya ndoa yake na mkewe mwingereta kuvunjika alichopata ni nguo alizovaa TU,alotia huruma sana mwamba yule.
 
Kabisa, unajua ule mgawanyo wa mali, uliwekwa sababu mke ndiyo mfanya kila kitu kwa mume. Huduma zote za nyumbani. Ila sasa imeshakuwa nongwa, wanaona mwanamke anafaidi. Bora kila mtu abaki na chake tu.
Kwakizazi hiki ukimpata huyo binti anayefanya hivyo, shukuru Mungu[emoji23][emoji23][emoji23]. Ukipata mtoto wa kiume akifika kipindi chakuoa muulize mabinti wangapi wanaziweza hizo kazi na hao waliosoma waulize wangapi wanataka kuzifanya hizo kazi[emoji23][emoji23][emoji23], ukiwa mwanamke huyajui maswaibu ya mwanaume bora tu utulize sista. Binti, kazi yake ni starehe shopping na kununua chakula cha nyumbani hataki kupika[emoji23][emoji23][emoji23]. Wacha sisi tukae kimya nyie mjione watakatifu na wakamilifu kwenye majukumu yenu[emoji23][emoji23].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa, unajua ule mgawanyo wa mali, uliwekwa sababu mke ndiyo mfanya kila kitu kwa mume. Huduma zote za nyumbani. Ila sasa imeshakuwa nongwa, wanaona mwanamke anafaidi. Bora kila mtu abaki na chake tu.
Kwamba ukinipikia wali maharage, na kufua boxer zangu, basi unaqualify kubeba nusu ya mali zangu?

Kama kweli hii ingekua ni hoja ya msingi, basi wafanyakazi wa ndani a.k.a beki tatu, wangekua matajiri wa kutupwa. Maana wanafanya yote hayo kwa ufanisi mkubwa!
 
Wakenya ndo walipewa task ya Google translation ya kiswahil eh..kazi ipo
Wajinga Sana hao wametafsiri hovyo kabisa na maana halisi ya maneno ni potofu kabisa. Hawa jamaa ni viherehere kwa wazungu lakini wameharibu. App yoyote yenye menyu ya kiswahili kuanzia ATM, na app zote za google sijawahi kichagua lugha ya kiswahili, itakupeleka porini
 
Mcheza kikapu maarufu toka NBA, Stephen Jackson amemuacha solemba aliekuwa mchumba wake baada ya kukutaa kisaini makubaliano ya PreNup

Kwa Msaada wa Google Translator:

Umaarufu na utajiri humsaidia sana mtu aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili yake.

Lakini pia huwa na mabadiliko ya kila mtu anayehusika.

Muulize tu Stephen Jackson, ambaye aliona upendo wa maisha yake ukifichua rangi zake halisi kabla hawajakaribia kufunga pingu za maisha na mchumba wake.

Jackson alisimulia hadithi ya kichaa ya wakati alimuacha mchumba wake baada ya kukataa kutia saini makubaliano ya kabla ya ndoa (PreNup).

Jackson anafahamu vyema hadhi yake katika jamii.

Ni mchezaji wa NBA ambaye amejikusanyia kiasi kizuri cha umaarufu na utajiri.

Kusaini prenup halikuwa jambo la kibinafsi au la kujisifu. Alitaka tu kulinda mambo ambayo amefanyia kazi kwa bidii , kulinda mali na utajirialiochuma kipindi yupo NBA.

"Ninajali watu wengi.

Siruhusu mwanamke mmoja kudhibiti kazi ngumu ambayo nimefanya maishani mwangu.

Hakuna m@l@y@ hizi aliyekuwa kwenye mazoezi nami kipindi chote nipo Gym.

Kwa hivyo nilijiambia yeyote ambaye nimeolewa naye, wanasaini prenup , hataki hakuna ndoa."
Alisema Jackson


"Ninampa. Ninapompa, asishangae kwa sababu mimi na yeye tulikaa chini na kukubaliana juu ya prenup.

Tulikubali. Nisikilizeni nyote.


Tulikubaliana juu ya prenup" Aliongeza Jackson

Jackson alichukua neno lake na kuendelea na mipango ya harusi.

Bingwa huyo wa mara moja wa NBA alisema alitumia karibu dolar za kimarekani 400,000 ( karibia TSh. 950m za kitanzania ) kwenye siku hiyo kuu.

Jackson aligundua kuwa mwanamke huyo hakuwa ametia saini makubaliano ya kabla ya ndoa walipokuwa wakipanga.

Hakufanya fujo kutoka kwake, akionyesha upendo wake kwa mwanamke

Lakini basi, mambo yalibadilika haraka siku ya arusi yenyewe. Jackson aligundua kwamba mwanamke huyo kwa njia fulani alichukizwa na mchungaji.

Hakujali ni nani atakayeongoza.

Alichotaka ni kuolewa na mpenzi wa maisha yake, lakini ndoa imevunika baada ya mpenzi huyo kutia kuweka saini kwenye PreNup

Jackson alimalizia kwa kusema "I was born at night but not last night"

Akimaanisha "mimi siyo mjinga"

Ref: https://www.basketballnetwork.net/off-the-court/when-stephen-jackson-left-his-fiancé-after-she-didnt-want-to-sign-the-prenup

Kuna la kujifunza hapo

HUYU JAMAA NI SHUJAA ZAIDI YA ASHRAF HAKIM

View attachment 2589869
Huyu hamkutii hakimi! Hakimi kashinda baada ya tukio kutokea, huyu kashinda kabla ya tatizo kutokea!

Hakimi ni mwenyekiti wa kudumu wa chama cha wanaume duniani!
 
Pre nup ndo nini

Ni mkataba wanaitaka ingia kwenye ndoa wanasaini kuonesha mali ambazo kila mmoja anamiliki kabla hawajaongia ndoani. Sasa jamaa na mchumba wake walikubaliana kusaini but binti akawa hajasaini. Iwapo huu mkataba usiposainiwa wanapoingia ndoani, ikitokea talaka, mgao wa mali utahusisha mali wanazomiliki ndoa itakapofika kilele
 
Wazo zuri. Shida inakuja kwa baadhi ya wanawake wanaoingia ndoani kwa malengo ya muda mfupi. Yaan mtu anaingia ndoani kajipanga kuwa baada ya miaka 2, 3 tunaachana tunagawana hao ndio walioharibu game.

Zaman watu walikua wakiachana na wanagawana haikua shida. Ila siku hizi imekua ka mchezo ka maksudi kabisa.

Kuna jamaa alioa mwanamke yy ni mfanya biashara na binti alikua mtu wa home, alimtoa kwao. Wakati wanaoana jamaa alikua amepanga ila alikua na kiwanja na ka spacial kake.

Baada ya kuoana wakashauriana waanze kujenga. Kweli wakaanza. Mwamba akawa ni mtu wa kutafuta mpunga anampa mwanamke akafanye jambo kwenye ujenzi wao.

Bwana we, kumbe binti ni akili nyingi kuliko mchizi. Binti alikua kila anaponunua kifaa cha ujenzi (tofari, mchanga, mawe, sment nk) risiti alikua anaandika jina lake. Mwamba hakuona kama ni shida hio kwa kua mwanamke si ndio alienda kununua.

Baada ya nyumba kukamilika wakahamia. Wakakaa miezi kama 9, 10 hivi binti akalianzisha waachane. Purukushani hadi mahakamani. Kufika mahakamani ikaonekana ile nyumba ni mali halali ya mwanamke na mwanaume hakuchangia kitu. Sababu ni ushahidi wa zile risiti za vifaa vya ujenzi ambazo zote zina jina la mwanamke

Mahakama ikaamua, ile nyumba iuzwe na pesa ya nyumba apwe mwanamke, na mwanaume apewe pesa ya kiwanja chake. Kisha mali zingine walizo nazo wagawane sawa. Mwamba alilia kilio cha mbwa koko aliyeshikwa na chatu.

Mazingira kama haya yanaonesha kuwa kwa miaka ya sasa, 80% ya wanawake huolewa kwa malengo ya mali. Ndio maana wanaume wamesanuka siku hizi.
Ningekuwa mimi ni huyo mwanaume huyo mke ange uwawa kifo cha kikatili sana..

Hawa ndio wale wanawake unasikia ame uwawa na watu wasiojulikana.

Chanzo ndio migogoro kama hii.
 
Back
Top Bottom