Wazo zuri. Shida inakuja kwa baadhi ya wanawake wanaoingia ndoani kwa malengo ya muda mfupi. Yaan mtu anaingia ndoani kajipanga kuwa baada ya miaka 2, 3 tunaachana tunagawana hao ndio walioharibu game.
Zaman watu walikua wakiachana na wanagawana haikua shida. Ila siku hizi imekua ka mchezo ka maksudi kabisa.
Kuna jamaa alioa mwanamke yy ni mfanya biashara na binti alikua mtu wa home, alimtoa kwao. Wakati wanaoana jamaa alikua amepanga ila alikua na kiwanja na ka spacial kake.
Baada ya kuoana wakashauriana waanze kujenga. Kweli wakaanza. Mwamba akawa ni mtu wa kutafuta mpunga anampa mwanamke akafanye jambo kwenye ujenzi wao.
Bwana we, kumbe binti ni akili nyingi kuliko mchizi. Binti alikua kila anaponunua kifaa cha ujenzi (tofari, mchanga, mawe, sment nk) risiti alikua anaandika jina lake. Mwamba hakuona kama ni shida hio kwa kua mwanamke si ndio alienda kununua.
Baada ya nyumba kukamilika wakahamia. Wakakaa miezi kama 9, 10 hivi binti akalianzisha waachane. Purukushani hadi mahakamani. Kufika mahakamani ikaonekana ile nyumba ni mali halali ya mwanamke na mwanaume hakuchangia kitu. Sababu ni ushahidi wa zile risiti za vifaa vya ujenzi ambazo zote zina jina la mwanamke
Mahakama ikaamua, ile nyumba iuzwe na pesa ya nyumba apwe mwanamke, na mwanaume apewe pesa ya kiwanja chake. Kisha mali zingine walizo nazo wagawane sawa. Mwamba alilia kilio cha mbwa koko aliyeshikwa na chatu.
Mazingira kama haya yanaonesha kuwa kwa miaka ya sasa, 80% ya wanawake huolewa kwa malengo ya mali. Ndio maana wanaume wamesanuka siku hizi.