Pre GE2025 Ahmed Kombo aliyesema akitoka Yesu na Mtume Muhammad anayefuata ni Rais Samia awaomba Radhi Wakristo na Waislam!

Pre GE2025 Ahmed Kombo aliyesema akitoka Yesu na Mtume Muhammad anayefuata ni Rais Samia awaomba Radhi Wakristo na Waislam!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Inasikitisha sana, unaona mabinti wengi hata baada ya kumaliza masomo na kukosa ajira, wameamua kujiajiri hata mama ntilie na kuuza vitu mbalimbali mitandaoni. Ila vijana wa kiume wapo mitandaoni wanajikombakomba kwa viongozi na kusifia watawala ili wapate vyeo na wengine wanaenda mbali na kuomba pesa kwa viongozi.

Tunahitaji mpango wa haraka wa kuokoa kizazi cha watoto wa kiume, kuna tatizo kubwa.

Sio hali ya kawaida kuona mwanaume anamsifia sifia na kujikombakomba kwa mtu hadharani na anaona ni hali ya kawaida.
Mkuu ni kweli ulisemalo, tatizo hili ni kubwa!!! Bahati mbaya machawa vinara yapo kwenye media!!! Yaani ni balaa!!!
 
Mkuu kwani kuchapia maanake nini, sio ndio kusema kule kule!!! Kwa kuchapia mtu hamsemi??? 🤣 🤣 🤣
Kuchapia ni kukosea kutamka, kutamka neno ambalo silo ulilokusudia. Kama yule mbunge aliyetamka "kuunga mkonyo hoja" tulicheka ila tulielewa alitaka kusema kuunga mkono hoja na si mkonyo.
 
Kuchapia ni kukosea kutamka, kutamka neno ambalo silo ulilokusudia. Kama yule mbunge aliyetamka "kuunga mkonyo hoja" tulicheka ila tulielewa alitaka kusema kuunga mkono hoja na si mkonyo.
🙏 Nimekusoma Mkuu!!
 
Hoja ni kwamba Je alichapia "ulimi hauna mfupa" au alikusudia kutamka kuwa Magufuli ni mungu?
Mkuu mazingira ya wakati ule, huyo Profesa alikuwa chawa wa kihindi vibaya kwa Magufuli.

Kisaikolojia haikuwa bahati mbaya, ndivyo alivyokuwa anampercieve Magufuli!!!

That guy is a learned Old man aliye badili hekima na utu wake kisa cheo!! Hukumbuki shukran yake kwa kutolea Jalalani!!
 
Mwanaharakati Ahmed Kombo amewaomba radhi Wakristo na Waislam kwa kauli aliyoitoa kuwa akitoka Yesu na Mtume Muhammad (SAW) anayefuata ni Rais Samia.

Kombo amesema yeye ni Muislamu na anatambua kuwa Yesu Kristo na Mtume Muhammad (SAW) ni Manabii hivyo anaomba radhi.

===

Pia soma uzi huu ambapo Ahmed alitamka maneno hayo;

- Huu uchawa umezidi: Kiongozi wa dini adai baada ya Mtume Mohammad na Yesu anafuata Rais SamiaK

Mwanaharakati Ahmed Kombo amewaomba radhi Wakristo na Waislam kwa kauli aliyoitoa kuwa akitoka Yesu na Mtume Muhammad (SAW) anayefuata ni Rais Samia.

Kombo amesema yeye ni Muislamu na anatambua kuwa Yesu Kristo na Mtume Muhammad (SAW) ni Manabii hivyo anaomba radhi.

===

Pia soma uzi huu ambapo Ahmed alitamka maneno hayo;

- Huu uchawa umezidi: Kiongozi wa dini adai baada ya Mtume Mohammad na Yesu anafuata Rais Samia
Mungu wake alikwisha lipokea neno lake, akamuombe radhi yeye, sisi hatuhusiki.
 
Inasikitisha sana, unaona mabinti wengi hata baada ya kumaliza masomo na kukosa ajira, wameamua kujiajiri hata mama ntilie na kuuza vitu mbalimbali mitandaoni. Ila vijana wa kiume wapo mitandaoni wanajikombakomba kwa viongozi na kusifia watawala ili wapate vyeo na wengine wanaenda mbali na kuomba pesa kwa viongozi.

Tunahitaji mpango wa haraka wa kuokoa kizazi cha watoto wa kiume, kuna tatizo kubwa.

Sio hali ya kawaida kuona mwanaume anamsifia sifia na kujikombakomba kwa mtu hadharani na anaona ni hali ya kawaida.
Kama Lucas mwashambwa hadi ameota kibiongo kwa kujipinda mgongo kuandika magazeti ya kusifia watawala ili naye akumbukwe.
 
Kwani kawakosea wakristo na waislam? Zile zilikuwa ni kejeli kwa Samia hivyo ndiye anayepaswa kuombwa msamaha.
Kawapa Kristo na Muhammad (s.a.w) priority halaf kafuata SSH. hiyo ni kwa mujib wa dini anayoanzisha. Lakini ukiona kimya ujue imekubalika na mhusika maana ni mojawapo ya aina ya mapambio tuliyozoea kusikia toka machawa wa Tz. Kna wkt JPM walimlinganisha na Mungu na hawakuona ni kufuru. Kuomba kwake radhi hakutuhusu, shauri yake na miungu wake
 
Back
Top Bottom