Inasikitisha sana, unaona mabinti wengi hata baada ya kumaliza masomo na kukosa ajira, wameamua kujiajiri hata mama ntilie na kuuza vitu mbalimbali mitandaoni. Ila vijana wa kiume wapo mitandaoni wanajikombakomba kwa viongozi na kusifia watawala ili wapate vyeo na wengine wanaenda mbali na kuomba pesa kwa viongozi.
Tunahitaji mpango wa haraka wa kuokoa kizazi cha watoto wa kiume, kuna tatizo kubwa.
Sio hali ya kawaida kuona mwanaume anamsifia sifia na kujikombakomba kwa mtu hadharani na anaona ni hali ya kawaida.