Ajabu na kweli: Padri wa kanisa katoliki kaoa mke na anavuta sigara kali!

Ajabu na kweli: Padri wa kanisa katoliki kaoa mke na anavuta sigara kali!

Halafu ameenda kwa Padri?? Padri huyo bado analitumikia kanisa? Na kama analitumikia kanisa anaishi kwake kivipi amepanga au? Hebu fafanua hili kwanza la sivyo ni umbea ulokosa ladha..
 
Kijana alikuwa mpita njia tu lakini anaishi jirani na maskani ya padre....so anafahamu kila kitu kinachoendelea ndio maana hakusita kuniambia ukweli hadharani.
Huyo padri anaishi peke yake kivipi? Au ni kigango hiko so padri ni mmoja tuu? Au ni amepanga uraiani...maskani ya padri ni mazingira ya kanisa..hebu tuelezee vzr
 
What to say is :

Mathayo 13:30
Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto; kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ ”
 
Ukute wewe ni mbaba unafamilia inakutegemea, inajua umeenda kazini kumbe upo jf unaandika mashudu, et umeishiwa nguvu uliposikia mwanaume mwenzio ameoa, WHAT THE FVCK YOU TALK
Kama hujui jambo ni bora ukae kimya kuliko kuonesha udhaifu wako hadharani. Unafahamu sheria za kanisa katoliki au unakuja hapa kumwaga mipovu yako ya bia za maokoto bila kufikiri? Kama mm hili jambo limenishtua wewe kinakuuma nini? Wewe hapa JF ni kazini kwako? Usinipangie maisha mkuu.
 
Na wewe ulikuwa unapita kwa padri ukakuta mwanamke ukashangaa? Au ndiyo walewale? Umekuta mambo yamebadilika ukazimia?
Na wewe hebu niache na hizo hekaya zako za mapapai. Kama nyie huko kwenu mmezoea mambo ya mapapai sio kila mahali mapapai yanafanya kazi. Tulia sindako zikuingie bibi mkubwa!
 
Halafu ameenda kwa Padri?? Padri huyo bado analitumikia kanisa? Na kama analitumikia kanisa anaishi kwake kivipi amepanga au? Hebu fafanua hili kwanza la sivyo ni umbea ulokosa ladha..
Yupo kwenye maskani yake. Kama huelewi rudi shule ukasome Kiswahili lugha yako ya taifa.
 
Jiandae na mashambulizi kutoka kwa wanafunzi na waumini wao.... ila ukweli mchungu, mapadre wanaishi maisha ya kidunia mnoooo.
Tokea asbh mada za kuwashambulia mapdri imeshamiri na wee ukaenda mbali ukasema padri amekuonga pesa Kiasi fln


Pia uko Happ kukazia kuwa.mapdri wanaishi maisha ya kidunia inaonekana unajuwa kitu fln juu ya watu hawa
 
Kamripoti basi usiendelee kulegea hapo chini ulipochuchumaa na kushika kichwa...
Wewe kinachokuuma nini mke wa padre? Acha kumpotosha padri wa watu......mwache aende akatumikie watu wa Mungu. Tamaa za mwili zitakuua. Wanaume wote waliotapakaa hapa mtaani ukawaacha ukaenda kumrubuni padre aache kazi ya Mungu aaanze kukushughulikia wewe tu? Mungu anakuona.
 
...padri akivuta sigara anapondwa... Au maandiko yanasema padri asivute wengine wavute?
 
Huyo padri anaishi peke yake kivipi? Au ni kigango hiko so padri ni mmoja tuu? Au ni amepanga uraiani...maskani ya padri ni mazingira ya kanisa..hebu tuelezee vzr
Haishi peke yake....anaishi na mke wake. Ngoja nikuwekee highlight kabisa maana watu wengine mu wagumu wa kuelewa.
 
Ukistaajabu ya Musa hujaona ya Firauni. Hivi majuzi nilikuwa mitaa fulani nikapita karibu na maskani ya padre mmoja wa kanisa katoliki. Kwa mbali nikamuona mwanamke wa makamo anafanya usafi na kulisha mifugo. Haujapita muda mrefu nikakutana na kijana na kumuuliza kama padre yupo akanijibu padre katoka ila mke wake yupo. Nikamuuliza je, mke wake ni yule niliyemuona anafanya usafi pale nyumbani? Akajibu: NDIYO! Nilihisi kushikwa ganzi na kushindwa kusimama wima. Nikajifanya sijisikii vizuri nikawa nimechuchumaa chini nimeinamisha kichwa. Yule kijana kaniuliza: Vipi unaumwa? Nikamjibu najisikia vibaya.

Kwa mshtuko wangu nilihisi kabisa yule kijana ameunganisha hali yangu na tukio la mke wa padre kwa kuwa alikuwa akiniangalia kwa hofu iliyochanganyikana na wasiwasi. Kijana alionesha hofu ya kutoa siri za watu. Nikaanza kujilaumu kimoyomoyo kwanini nilishindwa kujikaza hadi kijana wa watu akahisi labda nitaenda kuvujisha hizi taarifa kwa viongozi wa kanisa. Nami wala sina nia hiyo na sijamwambia mtu yeyote hadi leo ninapoandika kuhusu jambo hili hapa JF.

Siku za nyuma kidogo (takribani miaka 3 iliyopita) niliwahi kumshuhudia padre mwingine wa kanisa katoliki akivuta sigara kali. Nikashangaa sana. Wavutaji wa sigra kali wanafahamu aina hii ya sigara. Hii sio sigara ya kawaida ndio maana ikapewa hili jina la kipekee. Tangu siku hiyo nikagundua kwamba kumbe upadre wakati mwingine ni kazi tu kama kazi nyingine wala haina koneksheni na utakatifu au matendo mema. Kuna mapadre genuine ambao kweli wamejitoa kumtumikia Mungu kwa hali na mali na wengine ni wachumiatumbo tu.

MAONI YANGU
Ifike wakati sasa kanisa litambue umuhimu wa matamanio ya mwili kwa wanadamu na kusitisha mpango wake wa muda mrefu wa kuwazuia mapadri kuoa na kutumia vilevi vingine kama watu wa kawaida ilmradi hawavunji amri 10 za Mungu. Kitendo cha kulazimisha mapadri wasioe na kushiriki matendo mengine mema ya dunia sio jambo zuri.

ANGALIZO
Hii sio mada ya kidini bali ni habari mchanganyiko inayohusu maisha ya binadamu bila kujali imani, dini, rangi, jinsia, kabila au ukanda. Mods msiingie mkenge kuhamisha hii mada kwenda jukwaa la dini tafadhali.

Nawasilisha.
8.USISEME UONGO
 
Wewe kinachokuuma nini mke wa padre? Acha kumpotosha padri wa watu......mwache aende akatumikie watu wa Mungu. Tamaa za mwili zitakuua. Wanaume wote waliotapakaa hapa mtaani ukawaacha ukaenda kumrubuni padre aache kazi ya Mungu aaanze kukushughulikia wewe tu? Mungu anakuona.
Wewe nawe una wenge...
 
Kuingia Upadre ni hiari hivyo hawalazimishi tena wanakuwa watu wazima, hata Yuda Iskariote mpaka leo anaitwa mtume
 
Back
Top Bottom