Ajali Korogwe: Madaktari walipigiwa simu saa nne usiku wakafika saa kumi na moja

Ajali Korogwe: Madaktari walipigiwa simu saa nne usiku wakafika saa kumi na moja

Inasikitisha sana watu kutotomiza wajibu wao halafu kuwabebesha wengine mzigo.
Suala la ajali kubwa za kutisha nchi hii limeshakuwa kama jambo la kawaida na waliopaswa kuwajibika zisitokee hawatekelezi wajibu wao ipasavyo badala yake wanatafutwa mbuzi wa kafara tu.
Nyie mnaacha mnauana huko barabarani, mnataka kuwatwika watu wa watu mizigo mkiwa mizoga.
 
Ujue simu inapigwa ya hospital ya mtu ya mkononi
 
Angekuwa Magufuli haya yasingetokea trust me uzembe umekuwa mkubwa sana ofisini siku hizi:

Nipo natazama ITV super brand mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na wananchi wa lijitokeza wakati wa ajari mbaya iliyouwa Watanzania 20 watatu wakifua hospitalini wanathibitisha kuwa madaktari walipigiwa simu na mkuu wa wilaya ya korogwe wakaitikia na kusema wao walishapata taarifa mapema kabla hawajapigiwa simu muda wa saa nne na nusu usiku ila cha ajabu wakatokea saa kumi na moja asubuhi.

Wananchi wenye hasira walikuwa wakitaka hatua kali zaidi maana huo ni uzembe na uuwaji kabisa kwa kuwa kama wagonjwa wangepata huduma wasingekufa wengi zazi hasa walipelekwa usiku hospitalini.

"Uzembe kazini ilikuwa ni kutumbua papo kwa hapo kipindi cha jemedari Magufuli"

USSR
Africa 90% ya vifo husababishwa na hao jamaa.Trust me.
 
Hii inamaanisha nini kwenye vifo vya watu 17?
Hapana hao idadi imeongezeka kutokana na kukosa huduma hadi usiku huu wako 20 ,kuna watoto wawili na mwanaume mmoja wamekufa leo

USSR
 
Sijui ni mimi ndio nimeielewa hii habari vibaya au kuna watu wana matatizo ya akili

Nahisi nimemsikia RC anadai Doctors waliitwa Hospital sio eneo la accident
Ndio uko sahihi hawasomi hawa wao ni kuandika tu tena hao madaktari wanaishi kota

USSR
 
Bro, wewe si wa kwanza kuishi nje. Sasa sijui wazungumzia nje ipi. Madaktari hawahusiki na tiba ya ajali nje ya hospitali. Huko kuna paramedics, ambao si madaktari. Mna paramedics hapa bongo?
Wewe unambiwa hospitalini wewe unasema nje ya hospitali nje wapi mbona huwa mnakwenda vichochoroni kutibu

USSR
 
Ww mbona unaongea ujinga, sasa kama huyo Dc sio mtaalam wa afya hiyo referral form kaandika kitu Gani? Acheni kuingiza siasa kwenye taaluma za watu hilo ni jukumu la zimamoto na vikosi vya ulinzi kazi ya ma Dr ni kuwasubiri hao wagonjwa hospitali wawatie huduma.
Wewe ni daktari?

USSR
 
Africa 90% ya vifo husababishwa na hao jamaa.Trust me.
Kabisa mara ukute yamelewa mara hayapo mapuuzi tu wako bias sana hao wapuuzi

USSR
 
Asilimia kubwa ya Watu humu hawajafuatilia kilichotokea kuhusu hao madaktari.

Madaktari hao hawakuitwa eneo la Ajari bali ni hospitalini. Na hawakufika kwa wakati na zaidi .

Na zaidi mmoja wao anaishi eneo hilo hilo la Hospitali.
 
Ni upuuzi tu !! Kwani masaa ya kazi hayajulikani? Hata uwapigie simu siyo lazima waje muda huo, kwani hawana shughuli nyingine waliyokuwa wanafanya? Eti asingekuwa Magufuli wasingefanya hivyo? UJINGA MTUPU.

Mbona yeye mwenyewe KAFA akiwa Rais? Kwa nini watu hawakumuogopa kuwa atakufa.
Unafahamu daktari akiwa zamu, anakuwa zamu siku nzima(24hrs).

Na hao madaktari walioitwa ni Viongozi yaani DMO na Incharge wa hospitali ya wilaya.
Yaani hospitalini kwako umeletewa majeruhi wa ajari kubwa hiyo.

Incharge wa hospitali usionekane eti masaa ya kazi.!!!!
 
Asilimia kubwa ya Watu humu hawajafuatilia kilichotokea kuhusu hao madaktari.

Madaktari hao hawakuitwa eneo la Ajari bali ni hospitalini. Na hawakufika kwa wakati na zaidi .

Na zaidi mmoja wao anaishi eneo hilo hilo la Hospitali.
Hiyo Hospitali ina madaktari wangapi?

Ina Emergency Operation Plan/mpango wa dharura?

Kwa nini hao waliitwa? Ndio ilikuwa zamu yao kwa matukio ya dharura siku hiyo au wao ndio wahusika wa kila tukio la dharura?

Kama kungekuwa na ajali nyingine dharura sehemu nyingine hilo tukio lingeshughulikiwaje?
 
Hiyo Hospitali ina madaktari wangapi?
Ina Emergency Operation Plan/mpango wa dharura?
Kwa nini hao waliitwa? Ndio ilikuwa zamu yao kwa matukio ya dharura siku hiyo au wao ndio wahusika wa kila tukio la dharura?
Kama kungekuwa na ajali nyingine dharura sehemu nyingine hilo tukio lingeshughulikiwaje?
Iko hivi Hospitalini, hasa hizi za huku chini, mara nyingi wakati wa Usiku huwa kuna Daktari mmoja au wawili
Inapotoea dharura madaktari huwa wanaitwa.

Tena dharura ikiwa kubwa, unaitwa hata kama hauko zamu.

Sasa ulitegemea nani awaite watumishi ambao hawako zamu, waje wasaidie kama sio Incharge na DMO.


Incharge wa hospitali bila hata kuitwa, unapopata taarifa kuwa kuna dharura hospitalini kwako, dharura ambayo ni tishio kwa resource zako( Staffs + Equipments). Lazima uwepo ili kuorganize vizuri. Good enough wew mwenyewe ni Daktari means utatumika.

Hii kitu sio kwa madaktari na hospitali hata ofisini kwako ukiwa wew ndio bosi na imetokea dharura kubwa. Ni muhimu uwepo.

Hii kitu ukiangalia kwa jiko la neutral, madaktari wamekosea
 
yaani kusema ukweli, kwa wale waliowahi kuishi nje kidogo, madaktari wa kibongo wanaboa sana. wana kiburi, wapenda rushwa na vinajifanya vitaalaamuuuu wakati kutibu haviwezi. kuna wakati huwa naviangalia naviacha tu. kwamba tusiwaseme ati wanatutibu wakati tunawaona wazi kabisa wanazingua tukiwalinganisha na madoctor wenzao? walevi, malaya na kiufupi hakuna kitu yaani. watz wengi wanapona kwa kudra za Mungu tu ila majority ni incompetent, hawana ari ya kutibu wanafanya tu kwa mshahara. (though sio wote, wapo wale wazoefu wanajitahidi ila majority ni vuruvuru tu). binafsi nikikuta asehemu doctor au polisi anafumuliwa na wenye madaraka, hata huwa siumizi moyo kufikiria. wengi wanastahili.

Kwa ujumla sekta nyingi na majanga
 
Back
Top Bottom