Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Innalillah wainnailayh rajeehuun
 
Watoto hawana dhambi na Mungu atawaweka mahali pema peponi na watapata raha ya milele
 
Mkuu client kwa heshima ya wafiwa na wahanga kwa ujumla.
Nilikuwa nina ombi ubadili Avatar yako japo kwa siku hii moja tu (hii ya leo) kisha
utairudisha tena, maana umeleta uzi wa majonzi makubw aila avatar
yako ina umiza sana ukiiangalia na aina ya habari uliyoeleta hapa jamvini.


NB: ni ombi tu sio lazima.

 
Mungu awarehemu wafiwa wote
uongozi wa shule,,awatie moyo
pigo kubwa kwa familia
 
Dah mbaya sana hii,wapumzike kwa amani ndugu zetu hao.
 
Kifo sio kumwaga damu inatokana ajali ilivyo tokea mwngine kwa mshituko .plesha .kuumia ndani kwa ndani na N.K
 
Ile njia imekaa vibaya jaman.., watoto walikuwa wanaenda kufanya mtihani na st. Tumaini iliyopo karatu.

Ni mbaya sana, inauma sana. Hata kama wote tutarudi huko ila siyo kwa hivi jaman...

Uuh Mungu ndo ajuaye hatima yetu.
 
Hapo sio mwendo kas n miundo mbinu ya barabara na mvua hizi ndio balaa kabisa..Mungu tuepushie zimwi hili la ajali
Hiyo barabara imepita gari ngapi tangu asubuhi mbona hazijaanguka. Wacha kuminyana sababu kubwa ya ajali ni mwendokasi hizo zingine zina mchango mdogo sana kwa ajali
 
This is very painful. Inatia huzuni mno. Mungu awape subira wote walioathirika.
 
Mungu awasaidie wazazi wa wanafunzi zaidi sana familia za walimu.Wakati huu ni wakati wa majonzi sana sana kwa taifa...
 
Najaribu kuvaa uzazi hapo oooh mungu watie nguvu wazazi katika kipindi hiki kigumu pia warehemu marehemu
 
Umemlipia mtoto wako ada toka std 1 had 7 na huenda ndio tegemeo lako halafu ghafla unaletewa habari ya msiba. So sad!
 
Eee mwenyezimungu uwapunzishe marehem wote mahala pema na uwatie nguvu wazazi, ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu wanachopitia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…