Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Nimepata habari isiyo na shaka kuwa gari aina ya coaster limeua watoto karibu wote waliokuwa wanaelekea mjini Karatu kwa ziara ya kimasomo, taarifa zinasema wamebaki watoto(3) tu wengine wamefariki, shule inaitwa Lucky Vincent Nursery & Primary School ipo Arusha ni medium schools,kwa wenye updates tunaomba mtupe

Picha: Soon ntaziapload ni ajali ya mda huu
Mungu awalaze mahali pema peponi
----------------------

UPDATE: Coaster ina jumla ya abiria 30 na wote wanasadikiwa wamefariki,maiti zimepelekwa hospitalini na watu wameondoka eneo la tukio,mvua inanyesha

UPDATE: Picha zinakuja soon ripota yuko eneo la tukio..

19a4fcd1c935e4c031670cd880a46bc5.jpg

.........................
UPDATES:Magari ya polisi yametanda kila kona na maiti zimebebwa na magari ya polisi
Tayari kuhifadhiwa
...................
UPDATES:Ni watoto wanne(3) wanasadikiwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasi wasi vifo vikaongezeka
UPDATES:Lucky vincent nursery school bus
62d62ef75dec257e496254f5cfb2808e.jpg

UPDATES:Shughuli za uokozi
a198eaa3cab45eec73b51943888b0a63.jpg

UPDATES:Gari lilikuwa na abiria 30 wanafunzi 25,waalimu (4) wote wa kiume na dereva 1
UPDATES:Kati ya majeruhi watoto watatu(3) wawili wako mahututi kabisa na mmoja amepasuka ubongo
UPDATE:Maajabu ya ajali hakuna damu zozote zilizotapakaa licha ya watu wengi sana kufa!
Watoto hawana dhambi na Mungu atawaweka mahali pema peponi na watapata raha ya milele
 
Mkuu client kwa heshima ya wafiwa na wahanga kwa ujumla.
Nilikuwa nina ombi ubadili Avatar yako japo kwa siku hii moja tu (hii ya leo) kisha
utairudisha tena, maana umeleta uzi wa majonzi makubw aila avatar
yako ina umiza sana ukiiangalia na aina ya habari uliyoeleta hapa jamvini.

upload_2017-5-6_12-6-39.jpeg

NB: ni ombi tu sio lazima.

 
Mungu awarehemu wafiwa wote
uongozi wa shule,,awatie moyo
pigo kubwa kwa familia
 
Kifo sio kumwaga damu inatokana ajali ilivyo tokea mwngine kwa mshituko .plesha .kuumia ndani kwa ndani na N.K
 
Ile njia imekaa vibaya jaman.., watoto walikuwa wanaenda kufanya mtihani na st. Tumaini iliyopo karatu.

Ni mbaya sana, inauma sana. Hata kama wote tutarudi huko ila siyo kwa hivi jaman...

Uuh Mungu ndo ajuaye hatima yetu.
 
Hapo sio mwendo kas n miundo mbinu ya barabara na mvua hizi ndio balaa kabisa..Mungu tuepushie zimwi hili la ajali
Hiyo barabara imepita gari ngapi tangu asubuhi mbona hazijaanguka. Wacha kuminyana sababu kubwa ya ajali ni mwendokasi hizo zingine zina mchango mdogo sana kwa ajali
 
This is very painful. Inatia huzuni mno. Mungu awape subira wote walioathirika.
 
Mungu awasaidie wazazi wa wanafunzi zaidi sana familia za walimu.Wakati huu ni wakati wa majonzi sana sana kwa taifa...
 
Najaribu kuvaa uzazi hapo oooh mungu watie nguvu wazazi katika kipindi hiki kigumu pia warehemu marehemu
 
Umemlipia mtoto wako ada toka std 1 had 7 na huenda ndio tegemeo lako halafu ghafla unaletewa habari ya msiba. So sad!
 
Eee mwenyezimungu uwapunzishe marehem wote mahala pema na uwatie nguvu wazazi, ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu wanachopitia
 
Back
Top Bottom